Wana-CCM mnasemaje? MSIMAMO WA KINGUNGE NA MABADILIKO YA KATIBA YA CCM.

Kipeperushi

Senior Member
Aug 17, 2011
167
33
Tunafahamu kwamba mzee Kingunge ni miongoni mwa makada na wanasiasa wakongwe wa CCM. Kwa mujibu wa mzee Kingunge kikao kilichokaa kupitisha mabadiliko ya katiba hakikuwa na mamlaka ya kikatiba ya kufanya maamuzi hayo. Inasemekana kwamba kikao hicho kilitakiwa kutoa mapendekezo yaliyotakiwa kupelekwa kwenye Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM; ikiwa ndio kikao pekee chenye mamlaka ya kikatiba ya kupitisha mabadiliko ya katiba ya chama. Swali langu kwa wana-CCM ni hili:- Mnataka kutuambia kwamba katika kipindi chote ambacho mzee Kingunge amekuwa anakitumikia chama cha CCM hakuwa anajua anachokifanya mpaka leo híi aonekane kama ni mtu aliyekurupuka juu ya msimamo wake?
 
Mgogoro wa Ki-Katiba kuitafuna zaidi CCM japo mabadiliko yaliopitishwa na chama hicho yana malengo mazuri sana kuliko ka-kijimtazamo finyu ya wale wanaohisi kuja KUPOTEZA NAFASI ZA KUJILIMBIKIZIA MADARA kama kawaida ndani ya cham hicho.
 
Kingunge yupo sahihi mabadiliko makubwa ktk katiba ya CCM yanapitishwa na mkutano mkuu siyo NEC wala CC. Hata hivyo kwa chama kilichozozeeka na kuchoka kama CCM kikifanya maamuzi kinyume na katiba yake sijambo la kushangaza!
 
Of course ni Mkutano Mkuu ndio unapitisha mabadiliko ya Katiba ya CCM. Ibara ya 105:4 ya katiba hiyo inaelezea baadhi ya kazi za Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa kwamba: "Kubadili sehemu yoyote ya Katiba ya CCM kwa uamuzi wa theluthi mbili za
Wajumbe walio na haki ya kupiga kura kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili kutoka Zanzibar."

Sasa naamini kilichofanywa na vikao hivi vya chini mapendekezo tu ila yatapatiwa nguvu kwenye Mkutano Mkuu ambao utabadilisha Katiba hiyo. Ila kama watu wanafikiria mabadiliko yameshapita au wameshayafanya hapo kuna tatizo.
 
Nilifikiri ni kina sisi tuu tusio na interests kwenye siasa ndio huwa hatusomi katiba za vyama, kumbe mpaka wenye chama wenyewe!.

Naombeni wenyekumbukumbu watukumbushe lile azimio la Zanzibar lilipitaje bila baraka za Mkutano Mkuu?.

Kwa wanaoujua Mkutano Mkuu wa CCM, the real powers lies with CC na NEC, huo mkutano mkuu ni just li ruber stamp fulani tuu halina lolote!.
 
Dhambi ya kukiuka katiba na kuvunja sheria ni mbaya sana. Mkisha wafanyie wengine mtafanyiana na wenyewe pia.
 
Tunafahamu kwamba mzee Kingunge ni miongoni mwa makada na wanasiasa wakongwe wa CCM. Kwa mujibu wa mzee Kingunge kikao kilichokaa kupitisha mabadiliko ya katiba hakikuwa na mamlaka ya kikatiba ya kufanya maamuzi hayo. Inasemekana kwamba kikao hicho kilitakiwa kutoa mapendekezo yaliyotakiwa kupelekwa kwenye Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM; ikiwa ndio kikao pekee chenye mamlaka ya kikatiba ya kupitisha mabadiliko ya katiba ya chama. Swali langu kwa wana-CCM ni hili:- Mnataka kutuambia kwamba katika kipindi chote ambacho mzee Kingunge amekuwa anakitumikia chama cha CCM hakuwa anajua anachokifanya mpaka leo híi aonekane kama ni mtu aliyekurupuka juu ya msimamo wake?

Kama ukimsikiliza mzee Kingunge unapoteza muda wako.
 
Mapendekezo yakipelekwa kwenye mkutano mkuu (toka kwa hawa) huwa yanapingwa kweli?? Mara nyingi mie naona wanayapitisha tu.
Kingunge anahofia kunyang"anywa meno??!
 
Ni demokrasia pana kwa kingunge kuwa na uamuzi wake kama ilivyotokea kwa Zitto kabwe alipotaka kugombea sambamba na Mbowe katika nafasi ya Uenyekiti jina la Zitto likaondolewa.

Posho za bunge pia ziliwagawa wabunge ndani ya chadema na ndani ya CCM.
 
Sijawahi kumuelewa kingunge kama ana maslahi wa taifa hili. Mzee huyu haeleweki hata siku moja. CCM walifanya vizuri kutokumsikiliza.
 
yeye si mshauri wa raisi sasa vipi hawakuelewana,kama unshauru mtu hafuati unaachana na hiyo kazi
 
Of course ni Mkutano Mkuu ndio unapitisha mabadiliko ya Katiba ya CCM. Ibara ya 105:4 ya katiba hiyo inaelezea baadhi ya kazi za Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa kwamba: "Kubadili sehemu yoyote ya Katiba ya CCM kwa uamuzi wa theluthi mbili za
Wajumbe walio na haki ya kupiga kura kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili kutoka Zanzibar."

Sasa naamini kilichofanywa na vikao hivi vya chini mapendekezo tu ila yatapatiwa nguvu kwenye Mkutano Mkuu ambao utabadilisha Katiba hiyo. Ila kama watu wanafikiria mabadiliko yameshapita au wameshayafanya hapo kuna tatizo.
Mzee Mwanakijiji, nasikia kwenye katiba pia kuna kipengele kwenye kazi za NEC kinachoruhusu NEC kubadili vifungu vya Katiba, na baadaye kujulisha tu Mkutano Mkuu, hivyo mabadiliko hayo ndiyo tayari, Congress itajulishwa tu na wao hawana njia bali kubariki. Na kuhusu msimamo wa Kingunge, ni mawazo yake na yanaweza kuwa na mantiki nyingi tu, lakini kama nilifuatilia vizuri yaliyojiri kwenye NEC na taarifa zilizotolewa ni kwamba NEC kwenye kikao cha Novemba mwaka jana ilisharidhia wazee kuondolewa NEC na waNEC kuchaguliwa wilayani. Kikao cha juzi kilikuwa cha taarifa tu za taratibu hizo siyo tena maamuzi. Kingunge alitakiwa ayaseme hayo kikao cha Novemba mwaka jana. Asingetakiwa kurudisha wajumbe nyuma kwenye maamuzi yaliyokwisha amuliwa.
 
Back
Top Bottom