Wana bwabuki mko wapi ndugu zangu

naivasha

Member
May 13, 2011
94
29
Kwanza nawasalimu wana JF wote, salaam. Lakini pia nawasalimu ndugu zangu wa BWABUKI, nawakumbuka sana na nawapenda. Mko wapi ndg zangu? Nawakumbuka pia walimu wetu enzi hizo, Rutatina, Kahwa, Masalu, Focus.... Mimi nilisoma pale bwabuki sekondari mwaka 1987 -1990. Mwaka 1987 wakati naanza kidato cha I shule hii ilikuwa ndo inatimiza miaka miwili. Ninakumbuka wakati huo kidato cha I tulikuwa na mikondo mitatu yaani A, B na C wakati kidato cha II walikuwa A na B. Shule hii iliendelea kupata idadi kubwa ya wanafunzi na kupata maendeleo bora ikiwa ni pamoja na matokeo bora kabisa ya kitaaluma japo ilikuwa shule ya wazazi, sawa na shule za kata za sasa hivi, ikiwa na matatizo ya walimu, vifaa vya kufundishia, vyumba vya madarasa, mazingira yasiyo rafiki kujisomea nk hali ambayo haukuzuia vijana kupasua hanga la kitaaluma kiushindani sawa au zaidi ya vijana wa Ihungo, Nsumba, Maua, Umbwe n.k. Piai changamoto hizo hazikuwaathiri vijana wa enzi za miaka ya 1986 - 1990. Kila nikitafakari, darasa letu lililohitimisha kidato cha iv vijana wapata 90 kwa waliopo sasa hv kila mmoja nasikia anaendesha maisha yake sawia kwa msingi wa elimu ya BWABUKI. Mpooo ndg! Nawapongeza wazazi wetu walioanzisha na kulea shule hii. Wengi tumepita hapa.
Nimeona niwasalimie ndg zangu wa bwabuki kwani ninashindwa kuwasiliana nanyi kwa njia na namna nyingine tofauti. Nawakaribisha kwa mawasiliano na mashauriano na ikibidi kujikumbusha hili na lile kwa enzi zetu bwabuki.
Asanteni sana
 
Back
Top Bottom