Wamiliki wa baa Zanzibar watakiwa kuzilinda

Zimmermann

JF-Expert Member
Sep 28, 2010
2,790
1,232
Mwandishi wa Polisi, Zanzibar
JESHI Polisi visiwani Zanzibar, limewaagiza wamiliki na wafanyabiashara wa baa visiwani humo, kuchukua tahadhari kwa kuweka walinzi imara katika maeneo yanayozunguuka nyumba za biashara hiyo, ili kuepuka matukio ya uchomaji wa baa zao.

Rai hiyo ilitolewa jana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Aziz Juma Mohammed, alipokuwa akizungumza katika hafla ya kutunuku vyeti vya sifa na zawadi kwa askari polisi waliozima matukio ya kihalifu na kukamata silaha. Kamanda Aziz alisema matukio ya watu kuchoma moto baa, yanaweza kuzuilika kama kila mfanyabiashara wa baa ataweka walinzi imara wanaoweza kukabiliana na watu wanaojichukulia sheria mkokononi.

Hata hivyo Kamanda Aziz alisema polisi kwa upandewao wataendelea na juhudi za kufanya doria za mara kwa mara katika maeneo mbalimbali na kutafuta taarifa za kiintelijensia ili kuwabaini na kuwakamata wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.

Alikiri kuwa ingawa kuna matukio ya moto yanayotokana na ajali za kawaida, lakini baadhi ya matukio yanafanywa kwa makusudi na watu wachache ama kwa sababu za imani zao za kidini au visa.Kamanda huyo alisema polisi wataendelea kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kuwa wamekuwa wakishiriki katika vitendo hivyo.Alisema hiyo inatokana na ukweli kwamba wote ni wahalifu wanaopaswa kufikishwa mahakamani.
Source: Mwananchi
 
hivi hao wahalifu ambao wameshiriki kuchoma moto wamechukuliwa hatua gani? Pia kwa kauli hii ya polisi inaonekana wazi kuwa hawana nia ya dhati ya kulishughulikia hili
 
Sasa Polisi tunawalipa ni kwa kufanya kazi gani! Kama kumlinda raia na mali zake ambayo ni wajibu mkubwa wa kazi yao wanaanza kuikacha, basi warudi tu vijijini wakalime maana watakuwa hawana wanalolifanya. Wangekuwa wanajeshi labda tungesema tuwaache kwa kuwa tunahofia kama tutavamiwa hatutakuwa na jeshi la kulinda mipaka. Lakini kwa la polisi kukacha majukumu yake ya msingi, linatia shaka.
 
kuzilinda!!! au kuziondoa, ndio chanzo cha maasi, pombe haramu, nasema haramu haramu haraaaaaaaaaaaaaaamu nasema ondoeni uchafu wenu.
 
kuzilinda!!! au kuziondoa, ndio chanzo cha maasi, pombe haramu, nasema haramu haramu haraaaaaaaaaaaaaaamu nasema ondoeni uchafu wenu.
Woyowoyo acheni unafiki, kama wewe hunywi pombe usiingilie starehe za wenzako, mbona mimi sipendi watu wanaokunywa soda lakini siwachukii wauza soda? kwanini sasa unichukie mimi nijinyweae tubia twangu. Wengi wenu Zanzibar hawana pesa za kunywa pombe hivyo hawapendi kuona mtu anakunywa pombe na si sababu ya Imani.
 
Back
Top Bottom