Wameniibia na Vijisenti Kidogo........Malima

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,145
13,216
Hii kauli ameitoa Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mh. Kigoma Malima wakati akitoa tathmini ya vitu alivyoibiwa ambavyo ilikuwa ni fedha taslimu dola 4000 na Tsh 1.5m, akisema kwake yeye ilikuwa kama vijisenti tu (pocket money) vya kumsaidia akiwa njiani.............kauli kama hii (vijisenti) iliwahi kutolewa na Mh. Andrew Chenge na kuzua majadiliano makali miongoni mwa jamii.
 
ni kweli $4000 pesa ndogo sana
eti eeeh!!!!! huo nimshahara wa dakatari kwa miezi sita mkuu na chenjia inabaki, kwa mwenzetu ni pocket money, evry case has its own merit
 
Hivi ni kweli mkuu alivunjiwa? au ali import ka mzigo na mambo yakamgeuka. Natamani maelezo yanyooke kidogo. Ni kama mgeni wake alijilipa mapema na kusepa..
 
Waziri aibiwa mamilioni hotelini Moro Send to a friend
Saturday, 10 March 2012 10:40
0digg
malima%20adam.jpg
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima​
Venance George, Morogoro
NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima ameibiwa vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh23.3milioni katika Hoteli ya Nashera mjini hapa.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Hamisi Seleman alisema kwamba uchunguzi wa tukio hilo lililotokea jana alfajiri unaendelea na kwamba taarifa za awali zimeeleza kuwa mtu asiyejulikana alivunja dirisha la chumba namba 125 alichokuwa amepanga Naibu Waziri huyo kisha kuingia ndani na kuiba vitu hivyo.

"Vitu alivyoibiwa ni pamoja na laptop tatu, aina ya Dell zenye thamani ya Sh5.6 milioni. Vinasa sauti viwili vya digitali na headphone zake zote ambavyo thamani yake ni Sh milioni moja, simu tatu, ya kwanza Nokia C6 ya Sh500,000, Nokia E200 ya Sh250,000 na Blackberry yenye thamani ya Sh5.5 milioni," alisema kamanda huyo na kuongeza:

"Vitu vingine ni pete mbili za almasi zenye thamani ya Sh2.5 milioni, Dola za Marekani 4,000 ambazo ni sawa na Sh6.5milioni, fedha taslimu Sh1.5 milioni, kadi mbili za benki, mabegi matatu ya nguo, baraghashia mbili zenye thamani ya Sh50,000 na nyaraka mbalimbali za Serikali."

Kaimu kamanda huyo alisema kuwa polisi waliokwenda kufanya uchunguzi wa awali walibaini kuwa mtu aliyeiba vitu hivyo hakuwa amevaa viatu kutokana na nyayo za miguu yake zilizoonekana nje ya chumba alichokuwa naibu waziri huyo.

Hata hivyo, Kaimu Kamanda huyo ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Morogoro, alisema mwizi aliyeiba vitu hivyo hakuiba bastola na bunduki aina ya SMG alizokuwa nazo Naibu Waziri huyo ambazo zilikuwa sehemu ya wazi.

Alisema kuwa mpaka sasa polisi inawashikilia walinzi watatu wa hoteli hiyo kwa mahojiano zaidi kwa madai kuwa wao ndiyo wenye dhamana ya ulinzi katika eneo hilo.

Seleman alisisitiza kuwa mtaalamu wa kamera za ulinzi za hoteli hiyo pia anaendelea kufanya utafiti ili kubaini kama kuna picha zilizonaswa na kamera hizo wakati wa tukio hilo.

"Ukitazama vizuri katika picha za kamera hizo kuna kivuli cha gari inaonekana upande wa barabarani, lakini bado haionyeshi wazi ni aina gani ya gari, hivyo tunaendelea kuchunguza," alisema bila kufafanua kama kamera za ndani zilipata picha hizo.

Viongozi kadhaa wa serikali mkoani humo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, Katibu Tawala, Mgeni Baruani na maofisa kadhaa wa usalama wa Taifa, walifika hotelini hapo kufuatilia tukio hilo.

Uongozi wa hoteli hiyo uliwazuia waandishi wa habari kumwona Naibu Waziri huyo ukidai kuwa alikuwa na mazungumzo na viongozi wengine. Hata hivyo, baada ya kusubiri kwa nusu saa, waandishi waliwasiliana kwa simu na Bendera ambaye alikuwa na Naibu Waziri huyo na kuwaruhusu kwenda kumuona.

Lakini wakielekea huko, walizuiwa na walinzi wa hoteli hiyo wakiongozwa na msimamizi wa nyumba, Advent Kweka na kuwataka warejee mapokezi kwa maelezo kwamba Malima angekutana nao hapo.

Muda mfupi baadaye Mkuu wa Mkoa akiongozana na Katibu Tawala wa Mkoa na maofisa wengine wa Serikali, walifika mapokezi na kuwaambia waandishi kuwa isingekuwa vyema kwenda kumwona chumbani kwake kwa vile huko ni mahali pa faragha zaidi.

"Sisi tumepata taarifa na tulikuja kumpa pole. Siwezi kuwa msemaji wa jambo hili kwa vile mwenye kupaswa kulitolea ufafanuzi ni Naibu Waziri mwenyewe au hata meneja wa hoteli ambaye ndiye mhusika mkuu kwa vile tukio hili limetokea katika hoteli yake," alisema Mkuu wa Mkoa.

Meneja wa Hoteli ya Nashera, Yustini Mtua hakuwa tayari kulitolea ufafanuzi zaidi kwa maelezo kuwa polisi walimzuia kutoa taarifa yoyote mpaka hapo uchunguzi utakapokamilika.

"Kwa sasa sitapenda kusema kitu chochote kwa vile hivi tunavyozungumza sasa polisi wanaendelea na uchunguzi wao na wamenikataza kutoa taarifa zozote mpaka hapo uchunguzi unaoendelea utakapokamilika," alisema meneja huyo.

Kauli ya Malima

Baadaye jioni, Malima aliwaambia waandishi wa habari kuwa alifika hotelini hapo majira ya saa 5.30 usiku na kwa muda wa saa moja alikaa katika baraza akizungumza na mkewe na jamaa wengine kwa simu kisha kuingia chumbani ili akaoge.

"Lakini kabla ya kufanya hivyo, nilisikia katika luninga taarifa muhimu ya uchaguzi wa urais wa Urusi nikaghairi kwenda kuoga na kwenda sebuleni kutazama taarifa hiyo," alisema.

Alisema akiwa sebuleni hapo wakati akitazama taarifa hiyo, alikuwa pia akiandika mambo mbalimbali yaliyojiri katika mikutano yake na wananchi aliyoifanya mchana katika Tarafa ya Matombo, Morogoro na kupitiwa na usingizi.

Malima alisema alishtuka saa 10.45 alfajiri na kujikuta angali sebuleni na alipoingia chumbani kwake alikuta dirisha la chumba hicho likiwa wazi na pazia likiwa limesogezwa na kadhaa vimeibwa ndipo alipolazimika kutoa taarifa kwa uongozi wa hoteli hiyo.

Hata hivyo, Naibu Waziri huyo alisema tukio hilo linatatanisha kwa vile mtu aliyeingia ndani ya chumba chake kuiba inaonekana kama alikuwa mwenye taarifa za kutosha juu yake kutokana na jinsi alivyofanikiwa kubenjua komeo la dirisha hilo na kisha kuingia ndani bila ya kuhofu chochote.

Naibu Waziri huyo alitumia pia fursa hiyo kukanusha baadhi ya taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii inayodai kwamba ameibiwa vitu vyote na mwanamke ikiwa ni pamoja na nguo zake zote na kubakiwa na nguo za ndani.

Alisema kuwa nguo zake hazikuibwa isipokuwa suruali moja aina ya Jeans na kwamba hadi saa 8:00 mchana, alikuwa amefanikiwa kupata begi moja lililokuwa limetelekezwa katika eneo la Chuo cha Mifugo (LITI) likiwa na baadhi ya vitu vikiwemo pasipoti mbili za kusafiria na kadi za benki.

"Aliyeniponza ni huyo kaka yangu Edward Mdoe, mimi siku zote huwa nikija hapa huwa nalala vyumba vya juu sasa nilipotoa oda ya chumba niliambiwa chumba ninacho lala siku zote kina mtu, nikawaambia wamwambie atoke, lakini nilivyoambiwa yuko kaka yangu huyu nilisema basi nitalala chini," alisema.

Waziri aibiwa mamilioni hotelini Moro
Send to a friend

Duh hapo kwenye RED anamaanisha ana passport mbili za kusafiria zote za kwake au huwa anatembea na ya mkewe pia au ni za nchi tofauti, nataka kujua tu wadau....
 
Si bora yeye ni vijisenti kweli ukilinganisha na zile Chenge alikua anaongelea. Hawa watu hawana akili kabisa ya kuongea mbele ya hadhara wanajifikiria wao wenyewe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom