Wameishia wapi hawa??

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,958
7,512
Ni takribani miezi sasa imepita tokea yatokee ya akina Jairo,Luhanjo,Ngereja,Chami,Maige na wenzao waliopigwa chini kufuatia tuhuma za kukiuka sheria za utumishi wa umma na kupelekea Taifa letu kukumbwa na machungu lukuki,sasa leo naombwa kujuzwa hawa watu wako wapi leo na ni hatua zipi za kimahakama zilizokwisha kuanza kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa... na kama hapana hatua zozote basi na tuamini waliondolewa kimizengwe na hivyo warudishwe kwenye utumishi wao
 
naona wewe mgeni nchi hii...hiyo imetoka tena utasikia wamepewa vitengo sehem flani
 
Ni takribani miezi sasa imepita tokea yatokee ya akina Jairo,Luhanjo,Ngereja,Chami,Maige na wenzao waliopigwa chini kufuatia tuhuma za kukiuka sheria za utumishi wa umma na kupelekea Taifa letu kukumbwa na machungu lukuki,sasa leo naombwa kujuzwa hawa watu wako wapi leo na ni hatua zipi za kimahakama zilizokwisha kuanza kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa... na kama hapana hatua zozote basi na tuamini waliondolewa kimizengwe na hivyo warudishwe kwenye utumishi wao

Hao hawawezi kuchukuliwa hatua zozote za kimahakama kwani wametimiza kazi waliyotumwa na aliyewateua,na zaidi ya hayo walichotengeneza mkuu naye amepewa mgao wake.
 
Mkuu Rweye, hii ndiyo Tanzania, yenye kuwa na wananchi wanaoshangilia jambo "kushadadia jambo" kwa kelele na mguvu zote halafu siku mbili kimyaaaaa wamelala, the truth is hata kama wewe ukifanya huo ubadhirifu/kutoheshimu misingi ya utawala bora,..tutafanya yafuatayo;

1. Tutataka kujua ukweli ni upi( kwa Tume, huku ukiendelea kulipwa)

2.TUTAKUOMBA kujiuzulu na unaweza kukataa.

3.Wakati uchunguzi unaendelea unaweza kuihama nchi na taarifa zikaja kwamba

4.Baada ya kama wiki mbili hivi, tutakuwa tumeshasahau kwani kuna jambo/mambo ambayo yatatokea "BORA" kuliko hilo la kwako.

5.Tutaachia hapo na kusema haki haikutendeka, tusubiri uchaguzi na viongozi fulani tutawatoa kwani wao ndio wasababishi.

6.Uchaguzi utafika(tutapewa pesa, vijinguo, ) TUTASAHAU tena kama ilivyo kawaida yetu na kwa kuwa hilo jambo ni "BORA" kwa wakati huo.

7. And the vicious cycle will continue.

Hadi akili yetu ikikaa vizuri(kujifunza umakini, kutanguliza mambo ya msingi, n.k) TUTEGEMEE mengine mengi tu zaidi ya hayo.
 
Ni takribani miezi sasa imepita tokea yatokee ya akina Jairo,Luhanjo,Ngereja,Chami,Maige na wenzao waliopigwa chini kufuatia tuhuma za kukiuka sheria za utumishi wa umma na kupelekea Taifa letu kukumbwa na machungu lukuki,sasa leo naombwa kujuzwa hawa watu wako wapi leo na ni hatua zipi za kimahakama zilizokwisha kuanza kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa... na kama hapana hatua zozote basi na tuamini waliondolewa kimizengwe na hivyo warudishwe kwenye utumishi wao

wanakula vyao walivyopora watanzania taratiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiibu! bila bugudha
 
Mkuu,
Daudi Balali bado anaishi!! Kama huamini muulize De'Levis. Anaishi kisiwa flani analindwa kuliko DHAIFU, anatafuna pesa bila hofu!! Ila siku alizotoa nahisi zinakaribia!!
 
Hii nchi inaliwa tu. Hata kama watasimamishwa, hayo ni maneno tu hata kwenye kanga yapo. Watakula nchi hadi 2014 tu. 2015 lazima kieleweke tu.
 
Ni takribani miezi sasa imepita tokea yatokee ya akina Jairo,Luhanjo,Ngereja,Chami,Maige na wenzao waliopigwa chini kufuatia tuhuma za kukiuka sheria za utumishi wa umma na kupelekea Taifa letu kukumbwa na machungu lukuki,sasa leo naombwa kujuzwa hawa watu wako wapi leo na ni hatua zipi za kimahakama zilizokwisha kuanza kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa... na kama hapana hatua zozote basi na tuamini waliondolewa kimizengwe na hivyo warudishwe kwenye utumishi wao
Quota yao ya ulaji ilitimia

sasa zamu ya akina Muhogo
 
Nimeona mahali maige anauza lile ghorofa letu. Sijui ni hela ya biya imeisha ama anaogopa kufilisiwa chadema ikiingia madarakani?
 
Unafikiri Serikali ya JK iko tayari kuendelea kuvuana nguo? naamini wamejifunza kwa Prof. Costa Mahalu
 
Kwa kawaida mila zetu sisi watu wa pwani huwa hatuna maamuzi ya moja kwa moja, huwa tunasubiri kuona upepo unako elekea ndio tunasema. huwa tunaogopa, Maana tusije kuonekana wabaya kwa wakosaji. Kwa maana nyingine ni tabia za kinafiki. We can't call a spoon a spoon, we wait until some people call a spoon a spoon.
 
Back
Top Bottom