Lakini hata sisi watumishi wa umma tuna matatizo. Wanasiasa wana matatizo lakini sisi matatizo yetu ni makubwa sana. Tukishapata kazi hatufikirii ufanisi wa vitengo vyetu so long as mshahara unatoka serikalini on monthly basis. Hao hao watumishi wa umma tukiacha kazi serikalini tukaenda let say mgodini kwa mkaburu au IPP kwa Mengi tutafanya kazi kama punda. System yoyote yenye ufanisi ni lazima ifanye assessment kati ya mshahara inaomlipa mfanyakazi wake na faida anayozalisha huyo mfanyakazi. Lakini sekta ya umma Tz mzembe analipwa sawasawa na mwenye bidii kwenye kazi hiyo hiyo, we unategemea nini?
Hizi zote ni rewards systems. Zinapaswa kujengwa na mtu anayetaka kula jasho la mfanyakazi. Hamna mtu nayefanya kazi bila msukumo. Kunabaadhi wanataka mabadiliko, lakini kunawale wanaofanya kazi kutaka kutambulika, kukumbukwa - na kunawale wanaotaka uchochezi ili fikra ifanye kazi. Sasa kama reward yangu mimi ni mshahara tu - watu wengine hawafanyi ziada ambazo unaziona nchi zingine.
Cha msingi hapa kwanza lengo ni kupandisha ubora wa huduma inayotelewa - n a uafanya hivyo kwa kuwazawadia watoa huduma - maana watu wanapofanya kazi hawasukumwi na pesa tu - ila muonekana wao katika jamii zao, ama kufurahisha nafsi zao ama kuleta mabadiliko. Sasa, dhamani ya kazi inapoishia kwenye pesa tu ni tatizo