Wameambiwa waondoke katika chama au katika uongozi?

tatanyengo

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,134
280
Katika harakati za kujisafisha ili kuleta mvuto kwa wananchi, baadhi ya vigogo katika Chama Cha Mapinduzi wamepewa siku 90 kujiengua. Swali ninalojiuliza ni kwamba wameambiwa waondoke katika chama au ni katika nyadhifa mbalimbali walizonazo? Kama ni kujiengua katika chama ni chama gani kitakachokubali wajiunge nacho? Ngoja tusubiri kwani siku zinahesabika.
 
hakuna mwenye ubavu wa kuwaondoa.......CCM ni Mafisadi hivyo mwenye uwezo wa kuwaondoa ni wananchi kupitia chama tofauti na CCM...si Lowasa, Rostam Aziz na Chenge tu........kama Nape ameongopa mpaka kuwa taja majina unategemea nini
 
Jamani wote ni wezi, kuanzia wa ngazi ya chini hadi juu kabisa, na sio CCM tu, bali kila mkubwa kidogo mwenye nafasi, ni jamii nzima kuna muozo, tusimtafute msafi, Tanzania hakuna, tujaliwe kupata mtu moto moto hata kama kashaiba, lakini aboreshe taasisi na kuharakisha maendeleo. sio viongozi wa kulia lia au kuchekacheka, atoe JICHO NJE KUWAPIGISHA KAZI VITAMBI...
 
Wote wezi!!! Nadhani wewe waweza kutusadia zaidi kuwapata wengine ambao nao ni wezi mbali na CCM. Wote hao ndiyo tunaowatafuta usiku na mchana ili warejeshe fedha yetu. HEBU FAFANUA ZAIDI HAPO. Nimefurahi sana kusikia hivyo "Wote wezi!!" La.
 
Back
Top Bottom