Wamasai Wakisakata Kabumbu....

Ni hatari hii. Maana shuka likimkaba mtu au kukwama mguuni utasikia mtu kavunja mbavu. Nashauri serikali Edward Lowassa awanunulie vifaa vya michezo waondokane na hii hatari. Pia waangalie wanapocheza mpira wakitokea wezi wa mifugo watawaacha kwenye mipira na kuondoka na ng'ombe.

Unanikumbusha kule Afghanstan kipindi cha taliban kuna timu ilialikwa kuja kucheza mechi ilitokea india ama Pakistani wakaingia na Vibukta juu ya magoti wakawa wanawashangaa wenzao wa afghanstan chini wamevalia Panjab wakiwasimanga watachezaje mpira na nguo hizo,wakaja jamaa wa Taliban wakawacharaza viboko na vibukta vyao kwa kuwaambia kwanini wanacheza uchi!usishangae ya wamasai pengine wanogopa fimbo!
 
Mmmh, kweli mazingira yanamfanya binadamu awe chochote.

Mpira wenyewe naona kama jiwe
Bado na sime kiunoni.
 
Mpira wenyewe mbona kama ni mdogo sana, si wataishia kukanyagana sana.
 
Apo ukiwa refa lazima na wewe uwe na AKA47! vinginevyo hayo masime halali yako!
 
Hahahahaa, mambo ni kama Bolivia President, Evo Morales ambaye ukimchezea rafu, chunga sana mayai yako......

 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom