Wamasai,Wairaqw,Wabarabaig, Wasukuma, waambiwa warudi "makwao".

Taabu kubwa ni pale ukame unapotekea na mifigo kufa en mass!

Na kwa vile ni wahamaji..basi hata namna ya kuwasaidia wakipata shida..ni taabu sana!

Pia kuwapa huduma kama shule, afya na maji safi ni ngumu!
 
Ama kweli Binadamu hana shukran,
Yaani watu mnawasakama hawa wafugaji wakati nyie ndio walaji wakubwa wa nyama choma, supu na Kisusio.. sasa matumbo yamejaa wafugaji mnawaona hawana maana tena..
Jamani tatizo la ardhi ya Ufugaji linatokana na sheria mbovu za umiliki wa ardhi...period..
Je, sio sisi tuliosema Tanzania ni yetu wote hakuna mipaka wala mmiliki wa ardhi hii isipokuwa serikali?..sasa hawa leo wanapewa mipaka jamani ati waruddi makwao?..verdict imepita kwa sababu ni wagufaji, hivyo hawana ardhi!
Mbona nyumba mnagawa viwanja na msiruhusu kila mtu ajenge anapotaka, au kuwaambia Wandengereko warudi kwao Rufiji mnataka kujenga maghorofa maanake ukitazama nao ni wafugaji wadogo mijini..
Wakuu zangu, Lugha zinazotumika sii nzuri kabisa, hawa wafugaji hawana makosa kabisa na wataendelea kuishi karne ya 18 kwa sababu ya mfumo mbaya.

Kumbukeni ni hadi mwisho wa miaka ya 80, tumekuwa na hata kituo cha television, Computer na magri yalikuwa anasa, msemo wa naomba Lift ulikuwa kawaida kabisa!.. Sijawahi ona nchi za magharibi mtu akisubiri mtaani apewe lift na mtu asomjua!... ndio maisha yetu jamani kila kitu hatua kutokana na sheria butu zilizotufunga kamba za shingo..kisai kwamba mgugaji mwenye ng'ombe 3,000 bado ni maskini mlalahoi, kisha tunawaumu wafugaji badala ya system inayoshindwa kuelewa jinsi ya kuboresha utajiri huo.. Sisi sote maamuma, Tanzanite na vito kibao tumekuja vigundua lini? lakini muda wote tulivikalia na sio kwamba havikuwa na thamani..
Kila mkoa na kila wilaya wenye mifugo inatakiwa kuwa na sehemu za malisho au wafugaji wapewe ardhi kwa ajili ya malisho ya ng'ombe mifugo yao..
Ng'ombe wetu pamoja na hali ya hewa ni vitu ambavyo vinatufanya tuwe tofauti na Ulaya. Huwezi kumfugia Zebu au Ankole ndani ya chumba cha joto au baridi ukamlisha kwa kumkatia majani kama ng'ombe wa kizungu..
Kwa mtazamo wenu hata mifugo kama kuku, Kanga na bata hawatakiwi kabisa kurandaranda makazi ya watu..tena wanafungwa mijini tu ukienda nje kidogo ya mji kila nyumba ina kuku..
Ni maisha ambayo yanahitaji mwongozo, elimu na mfumo bora ktk kujenga mazingira bora badala ya kutumia maguvu na mitulinga kufikisha ujumbe.
In fact wananchi hao wa wilaya hiyo wataondoka hapo bila kufahamu sababu na kibaya zaidi wataendelea na ufugaji wao sehemu yoyote ile watakayo pelekwa kwani tatizo sio wao ila ni serikali kushindwa kutoa milki ya ardhi kwa wananchi wake...

Mkandara:

Naona unaleta Jazba tu hapa. Morogoro kama wilayani kilosa kuna wafugaji asilia. Kilosa ina idadi kubwa ya wagogo na wakaguru ambao wanafuga ng'ombe na kujishughulisha na kilimo.

Vilevile wakulima wa Morogoro ni wafugaji wa kuku, kondoa, mbuzi na bata. Na sehemu kubwa mahitaji yao ya nyama inatokana na juhudi zao na sio wafugaji.

Ni miaka ya hivi karibuni tu kundi la wamasai lilivamia na kuua wanakijiji 30. Huo unyanyasaji gani?

Unakuja bila kukaribishwa. Una vuruga mashamba ya watu na bado unaua watu.

Kama kwa tabia zao wanasaidia taifa, Morogoro sio mkoa pekee yake Tanzania. Wakaribisheni kwenye mikoa yenu.
 
:cool:
Mkuu Companero,Mr Ole Ndaskoi opinion on the livestock issue and overgrazing on farmers lands is wrong , dead wrong when it comes to what you are tring to potray.
The Masaai must learn to live in the present world.That Masaai kids would take 5000 herd of cattle to garze in low land to leave th high land fallow for fure use is now outdated and prehistoric.
If all the Masaai would have EACH 1000 herd of cattle, then Tanzania will not be enough for them and their cattle.I hope you can see where we are heading to-prehistoric land skirmishes in this 21st century.
Above all ,Mr Ole Ndaskoi and his bethren MUST CHANGE for better livestock husbandry.
We understand that there are people who simply love cattle as a form of wealth at the expense of the rest of the wananchi.
His uncalled for attacks on Hon Pinda is disgusting to say the least.

LG:

Companero hatachukua muda kusoma posti zako. Atakachofanya ni kurundika ma-posti ya watu hapa.
 
Wamasai jadi yao kuhamahama kutoka sehemu moja kwenda nyingine kulingana na sehemu ambayo wanaweza kulisha mifungo yao, na pia ikatokea sehemu hiyo mmoja kati ya hao wafugaji wa kimasai akafa basi pia kuhama na kutafuta sehemu nyingine yenye rutuba, je kweli hawa wanaweza kutengea ardhi?
 
LG:

Companero hatachukua muda kusoma posti zako. Atakachofanya ni kurundika ma-posti ya watu hapa.

Mkuu hiyo niliyoposti ni posti yangu, ni utafiti niliofanya kuhusu uhamaji yakinifu wa wamasai - baada ya muda nitalundika na posti ya utafiti wangu kuhusu Wabarabaig.
 
Lole Gwasika,
Mkuu Mkandara, si kweli kwamba wafugaji hawana ardhi, huo ni upotoshaji wa ukweli.
Ardhi wanayo tena kubwa sana .Tatizo ni kuwa wameiharibu kwa kuwa na mifugo mingi sana na ikisha haribika wao wanahamia ardhi nyingine.
Kuna majangwa mengi yaliyo jitokeza huko Arusha ,Mwanza, Shinyanga.
Mkuu tembelea sehemu hizo ili uweze kulijua tatizo linaloongelewa.
Umeshasema kuna MAJANGWA, kweli hao ng'ombe watafugika jangwani?..

Mkuu mimi natoka mitaa hiyo hawa Wamasai walikuwa wakiingia sana mikoa hiyo na walileta matatizo mengi sana ambayo ni nje kabisa ya madai yaliyotolewa hapa..
Kama ingekuwa (madai) Wamasai na hayo Makabila mengine wanafanya criminal acts ikiwa ni pamoja na kuiba mifugo, kuua watu na mengineyo machafu ambayo hayaambatani na nani mrithi halali wa ardhi fulani, ningekubali kabisa wawajibishwe kwa makosa yao...lakini hili la kuwahamisha ati kwa sababu wanaingia wilaya zenu warudi makwao!... noo mkuu hoja hii haikukaa sawa kabisa.
Hivyo kama raia yeyote wa Tanzania, wakosefu watafikishwa mahakamani kwa makosa ya vitendo vyao na sio kufuga ng'ombe wao wilaya ambayo sio makazi ya makabila yao..

Zakumi,
Mkuu hata mimi nimetoka katika familia kama yako tunafuga kuku, mbuzi, ng'ombe hata Uvuvi lakini sii wote tunaokula kile tunachofuga...Chakula chetu kila siku kama ni nyama tunaenda nunua ktk butcher hata kama tuna ng'ombe nyumbani..
nachopinga mimi ni ile mbiu yenu kuwataka wafugaji waondoke maeneo yenu kwa sababu ambazo hazina msingi ikiwa serikali yetu imeshindwa kutambua mazingira ya Ufugaji wetu na hata kujenga mfumo unaweza kukubalika..Hatua mnayopendekeza hapa haina tofauti kabisa na ile ya Nyerere kuhamishia watu vijijini isipokuwa tu tofauti ni kwamba hawa Wamasai ni wahamiaji na wamefanya hivyo kwa karne na Karne wakitafuta ardhi yenye rutba na mimea ya malisho..
Kuwepo kwao Tanzania ni tuzo kwetu na pekee wanabeba uzito mkubwa wa kuitangaza nchi yetu pamoja na kwamba watalii wengi hawaendi Umasaini wanakuja Dar na Zanzibar..Wenzetu Kenya Mawasai wamefika hadi kingo za mji wa Nairobi na mifugo yao.. na wanatumiwa kama tourist attraction Mtalii hana sababu ya kwenda mwituni..

Solution ya tatizo hili, ni swala la serikali kuanzisha ukulima wa mimea ya malisho kwa ng'ombe ktk maeneo yao au sehemu maalum za ufugaji jambo ambalo litawasaidia na sisi kuto bughudhana nao...Hdi leo hii generation ngapi zimepita Mawasai wamekuwa wakihama hama wakati inajulikana kabisa kwamba wanahama kutafuta majani ya kulisha ng'ombe wao..I mean century ya 21 bado tunawatazama tu kama sinema au sii raia wa nchi hii na Ufugaji bado umechukuliwa kama ni jadi ya watu sio biashara..
Mbegu na mbolea ya majani haya bei zake ni rahisi sana kuliko mimeo yoyote ya chakula na kizuri ni kwamba ukipanda mara moja huna haja ya kurudia tena kinachotakiwa tu ni maji kwa wingi, yakikatwa huota haraka sana..Hivyo, if we can plant a tree hadi mijini mbele ya maduka kwa sababu mzungu kasema tupande miti wakati nchi yetu Ki jiografia inaweza kuotesha miti bila hata kuhudumiwa tunashindwa nini kutumia elimu zetu ktk swala ambalo linahitaji elimu kutambua umuhimu wa malisho ya mifugo yetu.
Leo hii mnafuga ng'ombe watano wa kizungu na kuwakatia majani kama vile ni winter season kumbe nje ni nyuzi 40 above..hamuoni upuuzi tunaoufanya kwa maendeleo yetu wenyewe, lakini hawa jamaa ambao wana provide almost 80% ya nyama tunazokula ndio wenye matatizo!..
U know what we always find ways za kulaumu watu wengine, utasikia waislaam wakipiga kelele kuhusu Kengele za makanisani wakati wao wana Muadhini ambaye pia Wakristu hawapendi kumsikia..Above all that, ukiwauliza kinachopungua ktk maisha yao hawana la kusema na kwa nini wao wasihame basi kuepukana na makelele - hawana jibu, isipokuwa utasikia makelele bwnaa hawa watu hawana ustaarabu..Makelele ya two minute wakati mtu anaishi main road magari nayapita usiku na mchana haoni makelele isipokuwa yale yanayotoka upande wa pili asioupenda kiroho.. Acheni wakuu zangu jaribuni kujifunza kuishi na watu wengine ili nao watambue na kuheshimu fikra na tamaduni zenu...
Nilikuwepo!
 
Mkuu Mkandara , you are missing the point! Mmasaai akihamia mahali popote Tanzania ruksa.Tatizo hapa ni kuhamahama na mifugo , kufanya destruction on virgin land. Na hayo majangwa unayoyasema yametengenezwa na nani? kama siyo wao wenyewe.
Haileti logic yoyote kuwaruhusu hawa jamaa kuranda nchi nzima na kutengeneza majangwa mapya!
Lazima tuwe realistic na si mpaka mzungu aje kukwambia mambo ambayo ni dhahiri
 
Rogers, Peter J. (2004), Saskatoon on the Savanna: Discursive Dependency, Canadian-guided Agricultural Development, and the Hanang Wheat Complex, Tanzania.
<http://www.allacademic.com//meta/p_mla_apa_research_citation/0/7/2/5/7/pages72572/p72572-26.php>

Mvungi, Sengondo E. (2007). Study on Options for Pastoralists to secure their Livelihoods: Experiences in the Defence of Pastoralist Resource Rights in Tanzania: Lessons and Prospects Part A. (Report submitted to CORDS).
<http://www.tnrf.org/files/E-INFO-RLTF_VOL2-PART4_Mvungi-S_2008_Experiences_in_the_defence_of_pastoralist_rights_PART-B.pdf>

The Arusha Times/Nkwame, Valentine M. (2 - 8 August 2008). Bassotu farms controversy heats up: State House gives tall order.
<http://www.arushatimes.co.tz/2008/30/front_page_1.htm>
 
Lole Gwasika,

Umeshasema kuna MAJANGWA, kweli hao ng'ombe watafugika jangwani?..

Mkuu mimi natoka mitaa hiyo hawa Wamasai walikuwa wakiingia sana mikoa hiyo na walileta matatizo mengi sana ambayo ni nje kabisa ya madai yaliyotolewa hapa..
Kama ingekuwa (madai) Wamasai na hayo Makabila mengine wanafanya criminal acts ikiwa ni pamoja na kuiba mifugo, kuua watu na mengineyo machafu ambayo hayaambatani na nani mrithi halali wa ardhi fulani, ningekubali kabisa wawajibishwe kwa makosa yao...lakini hili la kuwahamisha ati kwa sababu wanaingia wilaya zenu warudi makwao!... noo mkuu hoja hii haikukaa sawa kabisa.
Hivyo kama raia yeyote wa Tanzania, wakosefu watafikishwa mahakamani kwa makosa ya vitendo vyao na sio kufuga ng'ombe wao wilaya ambayo sio makazi ya makabila yao..

Zakumi,
Mkuu hata mimi nimetoka katika familia kama yako tunafuga kuku, mbuzi, ng'ombe hata Uvuvi lakini sii wote tunaokula kile tunachofuga...Chakula chetu kila siku kama ni nyama tunaenda nunua ktk butcher hata kama tuna ng'ombe nyumbani..
nachopinga mimi ni ile mbiu yenu kuwataka wafugaji waondoke maeneo yenu kwa sababu ambazo hazina msingi ikiwa serikali yetu imeshindwa kutambua mazingira ya Ufugaji wetu na hata kujenga mfumo unaweza kukubalika..Hatua mnayopendekeza hapa haina tofauti kabisa na ile ya Nyerere kuhamishia watu vijijini isipokuwa tu tofauti ni kwamba hawa Wamasai ni wahamiaji na wamefanya hivyo kwa karne na Karne wakitafuta ardhi yenye rutba na mimea ya malisho..
Kuwepo kwao Tanzania ni tuzo kwetu na pekee wanabeba uzito mkubwa wa kuitangaza nchi yetu pamoja na kwamba watalii wengi hawaendi Umasaini wanakuja Dar na Zanzibar..Wenzetu Kenya Mawasai wamefika hadi kingo za mji wa Nairobi na mifugo yao.. na wanatumiwa kama tourist attraction Mtalii hana sababu ya kwenda mwituni..

Solution ya tatizo hili, ni swala la serikali kuanzisha ukulima wa mimea ya malisho kwa ng'ombe ktk maeneo yao au sehemu maalum za ufugaji jambo ambalo litawasaidia na sisi kuto bughudhana nao...Hdi leo hii generation ngapi zimepita Mawasai wamekuwa wakihama hama wakati inajulikana kabisa kwamba wanahama kutafuta majani ya kulisha ng'ombe wao..I mean century ya 21 bado tunawatazama tu kama sinema au sii raia wa nchi hii na Ufugaji bado umechukuliwa kama ni jadi ya watu sio biashara..
Mbegu na mbolea ya majani haya bei zake ni rahisi sana kuliko mimeo yoyote ya chakula na kizuri ni kwamba ukipanda mara moja huna haja ya kurudia tena kinachotakiwa tu ni maji kwa wingi, yakikatwa huota haraka sana..Hivyo, if we can plant a tree hadi mijini mbele ya maduka kwa sababu mzungu kasema tupande miti wakati nchi yetu Ki jiografia inaweza kuotesha miti bila hata kuhudumiwa tunashindwa nini kutumia elimu zetu ktk swala ambalo linahitaji elimu kutambua umuhimu wa malisho ya mifugo yetu.
Leo hii mnafuga ng'ombe watano wa kizungu na kuwakatia majani kama vile ni winter season kumbe nje ni nyuzi 40 above..hamuoni upuuzi tunaoufanya kwa maendeleo yetu wenyewe, lakini hawa jamaa ambao wana provide almost 80% ya nyama tunazokula ndio wenye matatizo!..
U know what we always find ways za kulaumu watu wengine, utasikia waislaam wakipiga kelele kuhusu Kengele za makanisani wakati wao wana Muadhini ambaye pia Wakristu hawapendi kumsikia..Above all that, ukiwauliza kinachopungua ktk maisha yao hawana la kusema na kwa nini wao wasihame basi kuepukana na makelele - hawana jibu, isipokuwa utasikia makelele bwnaa hawa watu hawana ustaarabu..Makelele ya two minute wakati mtu anaishi main road magari nayapita usiku na mchana haoni makelele isipokuwa yale yanayotoka upande wa pili asioupenda kiroho.. Acheni wakuu zangu jaribuni kujifunza kuishi na watu wengine ili nao watambue na kuheshimu fikra na tamaduni zenu...
Nilikuwepo!

Mkandara:

Hujui Historia yoyote kuhusu Morogoro lakini huchelewi kulipuka. Miaka ya 60 na 70, serikali iliwahamishia waMasai Morogoro.

Migogoro ilikuwepo mingi kati ya wenyeji na waMasai kuhusu wizi wa ng'ombe na wafugaji kulisha ng'ombe kwenye Mashamba.

Serikali iliwakatia waMasai sehemu ya kuishi na baada ya muda fulani kukatokea maelewano kati ya wamasai na wakulima. Na wamasai wengine wakaanza kuwa wakulima na kuwa wafanya biashara.

WaMasai wengi walikaa Morogoro kwa zaidi ya miaka 30, wanakula ugari, wali na wamejichanganya kiuchumi na watu wa Morogoro.

Lakini kutokana na ukame kuna wimbi jipya ambalo limekimbia mabadiliko ya hali wa hewa na kuhamia Morogoro hivi karibuni.

Na vilevile kuna waSukuma waliokimbia mauaji ya Wachawi Shinyanga na ku-settle mkoani Morogoro.

Hili kundi jipya halina respect, wanaiba ng'ombe, wanalisha mashamba. Na kutumia visima kwa mifugo bila kujali kuwa vinatumiwa na watu kwa matumizi.
Kwa mfano walivamia kijiji kimoja na kuua watu 30 wakati watu wakiwa wamelala. Kilichofanyika ni mkuu wa wilaya kusimamishwa kazi.

Matatizo waliyonayo hayana uhusiano wowote na wakazi wa Morogoro. Kwanini watu wa Morogoro have to pay the price.

Kama waMasai ni kivutio cha utalii, basi sehemu za kuvutia watalii sio kwenye mashamba ya watu.
 
Kuna mtu kasema wafugaji hawachangii chochote kwenye maendeleo ya nchi hivi huyo amesahau nyama choma ya nchi hii. Alafu world consumption of meat per person per year is 50 Kg. Bongoland it is currently 11Kg per year. Maybe thats why our brains do not work we lack protein.
 
Nazani issue hapa si kuwafukuza wafugaji, kinachotakiwa niserikali kuwatafutia maeneo ya kulisha ng''ombe wao na kuwapatia elimu ya ufugaji bora. ukweli ni kwamba serikali pamoja na halmashauri zetu huwa zinapata kodi kutoka kwenye mifugo hiyo kila mwaka hivyo si busara kwa watu kusema wafugaji wafukuzwe au wahamishwe kwa nguvu bila kutafutiwa maeneo yao maalum. Ni ukweli usiopingika kuwa nyama yote inayoliwa hapa Dar na miji mingine inatokana na hawa mifugo hivo sioni sababu ya kuwalaumu wafugaji wakati tunaenjoy nyama ya mifugo hao.Hata ubavu unaotumiwa na serikali wakati mwingine ni kwasababu wafugaji wengi hawana elimu.Kama mwarabu anaweza kutafutiwa eneo why not kwa watanzania halisi?
 
Ibrasule:

Kwani kabla ya kuja Morogoro walikuwa wanaishi wapi?
 
Mkuu Companero ,I respect original thinking a critique.
Sasa weye mzee umenijazia ma paphlet ya wenzio waliotoa mwazo yao ambayo kwa bahati mbaya si sahii.
Hakuna mtu anayewachukia wafugaji , ni ile tabia ya kuharibu ardhi na mazao ya wakulima ambayo inapingwa kwa nguvu zote.
Bado argument iliyopo ni wale wafugaji wapatiwe elimu zaidi ya ufugaji wa kisasa ,NA WARUDI KWAO kwenye ile ardhi waliyoiacha , ili wakaitumie vizuri zaidi.
Ku argue kwamba ardhi hiyo ya wafugaji walinya'ganywa is a non starter kwa vile kama ilivyo sehemu nyingine zote nchini serikali haikuchukua arhi yote kwa matumizi maalum au kwa wawekezaji.
Bado inabidi ujijibu swali hili, kila mfugaji akiamua kuwa na ng'ombe 1000 kila mmoja, je Tanzania patatosha?
 
Mkuu Companero ,I respect original thinking a critique. Sasa weye mzee umenijazia ma paphlet ya wenzio waliotoa mwazo yao ambayo kwa bahati mbaya si sahii. Hakuna mtu anayewachukia wafugaji , ni ile tabia ya kuharibu ardhi na mazao ya wakulima ambayo inapingwa kwa nguvu zote. Bado argument iliyopo ni wale wafugaji wapatiwe elimu zaidi ya ufugaji wa kisasa ,NA WARUDI KWAO kwenye ile ardhi waliyoiacha , ili wakaitumie vizuri zaidi.Kuargue kwamba ardhi hiyo ya wafugaji walinya'ganywa is a non starter kwa vile kama ilivyo sehemu nyingine zote nchini serikali haikuchukua arhi yote kwa matumizi maalum au kwa wawekezaji.Bado inabidi ujijibu swali hili, kila mfugaji akiamua kuwa na ng'ombe 1000 kila mmoja, je Tanzania patatosha?

Mkuu acha uvivu wa kusoma na acha kuendekeza kutoa visingizio, hayo yote ni mapamphlet yangu naam nimeyaandika mwenyewe, tena yako based on my fieldwork kwenye maeneo ambayo Wabarabaig wanafukuzwa baada ya kunyanganywa ardhi yao kule Hanang - Na haya hapa chini ndio matokeo ya kufukuzwa huko sasa sielewi unataka warudi "kwao" wapi wakati mlishawasukumia pembezoni kwenye makorongo huko "kwao":

UDADISI: Rethinking in Action: Shambani Hanang Kunani Pale?
 
Shambani Hanang Kunani Pale?

Namshukuru sana Jalia,
Kurejea Darisalama;
Arusha mpaka Manyara,
Mtafiti sikukwama.

Nimejawa na bashasha,
Mrejesho kuutuma;
Wanazuoni wa Taifa,
Usikilizeni umma.

Ardhi yao Wadatoga,
Iligeuzwa chauma;
Nafko lo ikajitwalia,
Ngano kuilima.

Barbaig do akacharuka,
Kortini akasimama;
Dola ikajitetea kijanja,
Sheria ikazifuma.

Ikaleta Operesheni Sogeza,
Wananchi kuwasukuma;
Vijijini wakaswekwa kisasa,
Wakache kuhamahama.

Ujima uendeshwao kiusasa,
Kikaazimia chama;
Utumike kujenga Tanzania ,
Maendeleo kupima.

Mwalimu akauita Ujamaa,
Tukaukubali pima;
Ukahubiriwa kwa harara,
Tukatazamia mema.

Tukalima kwa ushirika,
Pato kulichuma;
Ranchini tukafuga pia,
Kujipatia nyama.

Hatamu chama kikashika,
Utawala ukauma;
Nacho kikaihodhi Katiba;
Watu kuwazima.

Wafugaji wao wakaswagwa,
Kama wanyama;
Mpaka leo wanatangatanga,
Kutafuta neema.

Uchumi nao ukayumbayumba,
Shilingi ikazama;
Wakalisaliti Azimio Zanzibara,
Likapata kiyama.

Hatimaye Nafko ikafilisiwa,
Ikaupoteza uzima;
Wafugaji ardhiyo wakaililia,
Msafara wakatuma.

Kwao Wakuu wakafikia,
Risala wakaisoma;
Wakasihi ardhi kupewa,
Iwahifadhi daima.

Baadhi yao mashamba,
Wakuu wakasema;
Tutawapa enyi wazawa;
Mgawane mazima.

Ila mengine watayawekeza,
Hao wachuma;
Bila ajizi yakabinafsishwa,
Tena himahima.

Wakayanadi pia matirekta,
Navyo vyuma;
Hata maji wakayabinafsisha,
Nao wakachuma.

Wawekezaji yote hawajaweza,
Mashamba kuyalima;
Heri Nafko walivyoyakwatua,
Wanateta wakulima.

Tambua we mwanasiasa,
Unaleta zahama;
Kama kanzu kuichuuza,
Rasilimali mama.

Warudishieni rasilimali wana,
Nao ndama;
Wananchi tuweze kujifugia,
Na kulima.
 
Mkuu acha uvivu wa kusoma na acha kuendekeza kutoa visingizio, hayo yote ni mapamphlet yangu naam nimeyaandika mwenyewe, tena yako based on my fieldwork kwenye maeneo ambayo Wabarabaig wanafukuzwa baada ya kunyanganywa ardhi yao kule Hanang - Na haya hapa chini ndio matokeo ya kufukuzwa huko sasa sielewi unataka warudi "kwao" wapi wakati mlishawasukumia pembezoni kwenye makorongo huko "kwao":

UDADISI: Rethinking in Action: Shambani Hanang Kunani Pale?

Wala si uvivi wa kusoma , ila ni muelekeo wa logic yako isiyoeleweka.Above all bado hujajibu the basic contradictions katika argument yako
1)kila mfugaji akiwa na mgombe 1000 na akienda kule anakopenda Tanzania ingetosha?
2)Hawa watu kimsingi walitoka wapi?hawakutoka hewani, na ile ardhi yao kule walikotoka ikoje kule Arusha ,Hanang Kiteo, Shinyanga, sehemu za Tabora.Ni dhahiri kwa macho yetu tunaona "dust bowls "zinatengenezwa mbele ya macho yetu. Ni lazima tujifunze kujijibu maswali magumu na kuyapatia ufumbuzi.

Bado si ustaarabu kwa leo kuwa na ngombe 5000 na kuranda nao nchi nzima ukiharibu mazingira, I would have expected pamphlets zako kutoa summary ya mapendekezo yako. Sijui kama zina mapendekezo ya ufugaji boroa kwa hawa ndugu na vile vile namna ya kuirudisha ardhi waliyoiharibu katika uoto wake wa asili.
Kulaumu tu hatua zikichukuliwa hatua kurectify tatizo hili kila mtu anaweza , it is only the clear thinker who has the best solutions.
Najua haita kupendeza sana kama wewe ni mfugaji lakini huwezi kuishi maisha ya miaka 400 iliyopita katika karne hii ya 21.
 
Companero,

Tunataka hapa arguments na sii mabandiko..summarise ua thoughts and make even a few statements!

Sasa wote tukiweka kazi zetu je hapa patatosha kweli?
 
Back
Top Bottom