Monasha
JF-Expert Member
- Apr 2, 2011
- 561
- 422
Kutokana na mabadiliko ya kiuchumi duniani pamoja na mabadiliko ya tabia nchi ambapo joto limeonegezeka duniani na kutokuwepo kwa mvua za kuaminika uchumi wa ngombe hauwezi tena kuhimili kuendesha maisha na badala yake jamii ya Wamasai imeanza kujishugulisha na kilimo ili kufidia pengo.
Wamaasai siyo tu wameingia katika kilimo pekee bali wameanza taratibu kuingia katika nyanja zote kama ilivyo kwa watanzania wengine na kuishi katika makazi ya kudumu.
Wapo ambao wamehamia mijini kufanya biashara za kazi za sanaa za mikono ikiwamo ususi wa nywele na nyingine nyingi. Hata hivyo wako ambao wamebaki kwenye maeneo yao na kuendesha kilimo cha mazao ya chakula na biashara.
Sio kwamba tumeacha kufuga hapana, lakini pamoja na kufuga tumeamua kulima mazao ambayo tumegundua yanaweza kutusaidia kwa chakula na ziada kuuza ili kuongeza kipato mbali ya kutegemea ufugaji, anasema Sabaya Lwelyen mkazi wa kijiji cha Engalaoni, Wilayani Arusha.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Ngorika, Mkoani Arusha, Kisoisoi Nangenoi anasema kuwa moja ya mazao ambayo wameanza kulima siku za hivi karibuni ni pareto.
Amesewa walianza kulima pareto miaka miwili iliyopita baada ya kupata hamasa kutokana na kuwepo kwa soko la uhakika katika eneo lao ambalo pia pia linafaa sana kwa kilimo cha zao hilo la pareto.
Walikuja kuhamasisha kilimo cha pareto, lakini mwanzo hatukukubali kiurahisi tukihofia soko lake lakini pia hatukuwa na ujuzi wa kilimo cha pareto. Hivyo tukaamua kuwaachia wenzetu wachache ambao walipojaribu kulima wamepata manufaa kutokana na kuiuza bila usumbufu, anasema Nangenoi.
Anasema kufuatia mafanikio makubwa waliyopata wenzi wao kwa kulima pareto, wananchi wengi walihamasika na kukubali kutenga maeneo kwa ajili ya kuanzisha kilimo cha pareto.
Amesifu uwepo wa soko la uhakika wa pareto, ambapo mkulima analipwa mara moja na hakuna ubabaishaji kama ilivyo kwa baadhi ya wanunuzi wa mazao mengine katika eneo hilo.
Nimetenga ekari mbili kwa ajili ya kulima Pareto. Ninachosubiri kwa sasa ni kuletewa mbegu ili nipande kwa sababu nimeona manufaa ambayo jirani yangu amekuwa akiyapata, anasema Solomoni Loshloiza, mkazi wa Mukulate.
Hiyo ni kwa wale wamasai wanaoishi maeneo ya Arusha.
Lakini wenzao tunaoishi(jamani mwenzenu mi masai) maeneo ya Ngorongoro tunapata tabu sana hasa kwenye suala la kilimo kwani eneo hili wanadai ni la hifadhi na hivyo hakuna kilimo kinachoruhusiwa katika eneo hili.
Kweli eneo hili ni la hifadhi lakini mbona toka enzi za ukoloni wamasai hawa wa ngorongoro wamekuwa wakilima pamoja na kuishi na vivutio vyote bila ghadhabu yoyote???
Haya tumenyimwa kutumia ardhi yetu, sasa wewe unategemea tutaishije??
Wengi wetu (wamasai) wameishia mijini kutafuta kazi mbalimbali na hasa za ulinzi. Leo hii mmasai anajulikana kama "MBWA MKALI" Jamani huu ni udhalilishaji.
Na hii yote ni kutokana na serikali kushindwa kutafuta solution ya kudumu.
Kusema eneo lile hakuna kilimo kwa sababu ni HIFADHI, ni kweli lakini Hawa uliowakuta katika eneo lile utawafanyaje???
Wana JF naomba mawazo yenu