Wamasai jijini dar

supermario

Member
Dec 2, 2011
48
15
Wamasai ni watanzania wenzetu na wanaotambulika ulimwenguni kuliko kabila lolote lile la kitanzania kutokana na utamaduni wao kuanzia jinsi wanavyoishi hadi mavazi yao.
Tatizo langu linakuja pale wale ndugu zetu wa kimasai wanapotoka na kuja mjini. leo nimepanda daladala ambalo ni usafiri wa umma. Muda mfupi wakapanda wamasai sita wote na marungu na masime na mafimbo wakiwa na nguo zao za asili. ivi ni salama kweli kwa hawa ndugu zetu kuwa wanatembea na hizi silaa huku mjini? tena hawana ngombe wa hakuna hatari ya simba wala mnyama pori yeyote yule?
kwani haiwezekani na kufanya kitu watu wa rome kule italia husema ukiwa roma fanya waroma nanachokifanya. Yani wakiwa huku mjini kama hawawezi kuvaa nguo za kawaida basi hata zile silaha waziache home.

Kwa bahati mbaya umemchoma mtu na sime kwenye daladala inakuwaje sasa?

Wana jf hili swala mnalionaje?
 
acheni ukabila nyie wazungu manaofuata mila za kimagharibi na kuona tamaduni zenu kama uhalifu..pumbavu zenu..mnajiona mekuwa wazungu sana sio..uzungu wenyewe hamuuwezi maskini wa fikra nyie..
 
Utakapo chomwa na sime ndani ya daladala ndo utaona faida ya uzungu pimbi wewe! Ukabila umetoka wapi? wewe unaona sawa mtu kutembea na panga mjini? mbona wewe hutembei na lako pimbi wewe!
 
Utakapo chomwa na sime ndani ya daladala ndo utaona faida ya uzungu pimbi wewe! Ukabila umetoka wapi? wewe unaona sawa mtu kutembea na panga mjini? mbona wewe hutembei na lako pimbi wewe!

Mimi kwa mtizamo wangu, na hasa experience ya kuishi jirani na hawa wamasaai, hakuna haja ya kuwa na woga kuwahusu wao katika hali ya kawaida!

Wamasaai wamekuwa hivyo tangu ustaarabu ulipoingia mjini Arusha na Nairobi Kenya! Kwa upande wa Kenya, pamoja na kuwa kati ya makabila yaliyostarabika, (akina prof. Saitoti nk), hata kama amevalia suti anabeba sime + rungu lake!

Wao kwao hawawezi kutembea bila vifaa vyao hivyo, japo huwa wanajisikia kutokuwa na nguvu wanapozikosa!

Muda wote, wao binadamu wenzao si tatizo kwao, ila kwa hisia tu wanaamini pengine kwa tabia yao ya kuhama hama, hawana uhakika baada ya safari yao ya siku kama wataishia kwenye kichaka, pori au mwitu ndio maana wako standby kupambana na simba na wanyama wengine wakali!

Wale wa mkoa wa manyara wanahofia zaidi kukutana na wakurya ambao kwao ni wezi wao sugu wa mifugo yao!

Hivyo hakuna haja ya kutukanana kuhusu hawa jamaa, tuwe tu na amani tunapokutana nao! Maanake hata EL anatembea nazo hizi silaha awapo makwao
 
Back
Top Bottom