jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 24,989
- 22,521
Mkuu,cha kwanza cha kutizama,ni kuona ni nani na nani wanasapoti mipaka ipi na kutambua vs kutoitambua, tuanzie hapo maybe...vijinchi kama vyetu kwenye dunia ya sasa,viongozi wake waki "bweka",lazima kuna "handlers" behind, so cha muhimu ni kufuatilia hayo kwanza.Pamoja na kwamba ninaunga mkono njia za kidiplomasia zaidi katika kumaliza utata wa mgogoro wa mpaka kati yetu na malawi lakini pia mimi mtazamo wangu ni kuwa JWTZ kuhakikisha kwamba inalinda mipaka yetu ndani ya ziwa nyasa kama serikali inavyotambua kwamba ni katikati ya ziwa.
Sasa ikitokea mtu yeyote, chombo chochote, ama kampuni yoyote inayofanya utafiti ama shughuli yoyote iwe ya kiuchumi ama kijamii ndani ya ziwa nyasa imevuka/wamevuka mpaka na kuingia ndani ya eneo la Tanzania inabidi idhibitiwe/wadhibitiwe.
Kwa kufanya hivyo sidhani kwamba tutakuwa tumetangaza ama kuanzisha vita, hapo tutakuwa tunalinda mipaka yetu na sidhani kama kuna mtu ama jumuiya ya kimataifa itatushangaa ama kutucheka.
Kwasababu mkuu siyo siri, gharama za vita tutakopa(exclude life costs), na tutakopa kutoka kwenye taifa linalosapoti "point of view" yetu kuhusiana na huo mpaka...Na taifa/mataifa ambayo yanaweza kutuback kwenye either UN ama mahakama za kimataifa nk.
Ndo dunia inavyoenda kwasasa...