Wamachinga wavamia eneo la wazi lenye mgogoro Arusha

Filipo

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
9,342
5,536
Habari nilizozipata ni kwamba baadhi ya wamachinga wamevamia eneo la wazi lililopo Kilombero sokoni. Wameondoa bati zilizokuwa zimezungushwa na "mmiliki" ambaye aliuziwa eneo hilo kifisadi na aliyekuwa meya wa manispaa akishirikiana na aliyekuwa diwani wa Sombetini Musa Nkangaa. Itakumbukwa kwamba diwani huyo ambaye ni mmoja wa wanachama walio mfungulia G. Lema kesi ya kupinga ubunge wake alitimuliwa udiwani pamoja na aliyekuwa Meya kwa kuuza eneo hilo la wazi kwa mtu ambaye alianza ujenzi wa kituo cha mafuta. Leo asubuhi wamachinga waliokosa maeneo kwenye uwanja wa nmc wamevamia eneo hilo, wameondoa bati zilizokuwa zimezungushwa, kukata miti na kuanza kugawana eneo hilo. Katika kuuchoma uchafu waliouondoa eneo hilo, moshi mkubwa ulitanda na kulazimika kuitwa kikosi cha zimamoto kuja kuuzima. Askari wamejaa eneo hilo kwa sasa.
 
That is movement for change bana nafikiri ni wakati mzuri wa ccm kufaham ni aina gani ya watu wanaoishi ktk kizazi hiki bila hivyo ni vigumu kuwatawala raia usiowafaham
 
Back
Top Bottom