Walokole wataja Rais wamtakaye

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,834
155,781
KANISA la Tanzania Assembles Of God (TAG) limetaja sifa za rais wanayemtaka katika Uchaguzi Ukuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.

Akitoa msimamo wa kanisa hilo Mbeya mwishoni mwa wiki, Askofu Mkuu wa (TAG), Dkt. Barnabas Mtokambali alisema kuwa, rais ambaye mapato yake yanatokana na fedha chafu za ufisadi, ambaye pia hana uchungu na umaskini wa Watanzania, hana nafasi katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Dkt. Mtokambali aliongeza kuwa kiongozi yoyote ambaye ameamua kujitosa kuwawakilisha wananchi asiwe mwenye ubaguzi wa kidini wala itikadi yake ya kisiasa, na kwamba msimamo wa kanisa si kuchagua chama
bali kumchagua mtu ambaye anafaa.

"Msimamo wetu si kuchagua chama, bali tunamtaka mtu ambaye ana uchungu na maisha ya Watanzania bila kujali itikadi zake za chama na dini yake," tunamtaka mtu si chama cha siasa," alisisitiza Dkt. Mtokambali na kuongeza:

"Siku hizi mambo ya kuchagua chama yamepitwa na wakati, tunaangalia mtu bila kujali chama, tunaangalia uwezo wa mgombea anayetaka kupata kura kutoka kwa watu wa Mungu kama anatokana na mapato ya aibu na fedha za rushwa na ufisadi, watu wa aina hiyo hawana nafasi," alisisitiza.

Alifafanua kuwa chama chochote ambacho kitasimamisha mtu mwenye uadilifu na mwenye hofu ya Mungu kitapata ushindi mkubwa bila kujali kuwa mtu huyo ametoka katika chama kipi cha kisiasa.

Dkt. Mtokambali alisema kuwa iwapo kuna mtu ambaye atajitokeza kuutaka urais au uongozi wowote kwa njia za nguvu za giza, hana nafasi na kwamba kiongozi wa aina hiyo ni sawa na muuaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi asiyeitakia mema nchi yetu.

Kadhalika alisema kuwa mtu au chama chochote ambacho kimejipanga kusababisha vurugu katika uchaguzi mkuu hakitapata nafasi hiyo kwa kuwa viongozi wa dini nchini
wamefanya maombi na yoyote atakayethubutu kuwa chanzo cha vurugu laana ya Mungu itamuangukia.

"Tunamtaka kiongozi ambaye ana uchungu na nchi yake zaidi ya dini yake au chama chake cha kisiasa, tutamuunga mkono kwa nguvu zote na atashinda kwa
kishindo," alisema huku akishangiliwa na waumini wa dini hiyo jijini Mbeya.

Source: Majira
 
Back
Top Bottom