Kithuku, Hapa ndipo ninapokumbuka maneno ya hayati Mwl. Nyerere kuwa upinzani wa kweli kwa CCM utatoka ndani ya CCM yenyewe. Kwa hakika level ya upinzani Tz kwa sasa ni sawa sawa na hakuna wengi wa wanaojiita wapinzani ni watu waliozidiwa na tamaa au njaa kiasi kwamba wanakuwa wepesi kurubuniwa na CCM. Tumeshuhudia viongozi kadhaa waliokuwa katika vyama vya upinzani wakihama vyama vyao na kurudi CCM kwani wengi wao waliotokea huko. Ipo mifano kama akina Masumbuko Lamwai, Dr. Kaborouna wengi wenye nyadhifa na wanachama wa kawaida.
Pia suala la vyama vya upinzani kuungana bado ni kitendawili kwani hao viongozi wana ubinafsi na tamaa za kutaka kuingia ikulu kitu ambacho hata Nyerere alikishangaa sana. Na aliwahi kusema kuwa hata kama wananchi wameamua kusukuma gari la kiongozi wa upinzani kwa nderemo na vigerere wawaache tu kwani alijua kuwa hawatafika mbali na sasa tunashuhudia upinzani ukielelea kufa kifo cha asilia. Kwa hiyo hata huyo Odinga anachowashauri hao ndugu ni wastage of time and energy tu lakini nadiriki kusema upinzani Tanzani "MUFIRISI".....