Njoka Ereguu
JF-Expert Member
- Apr 7, 2012
- 821
- 335
Kwa ujumla hii thread imevuta hisia za wengi, na pia imetukumbusha mengi hata kufahamu wengine wamefariki kwa kweli hii mada imenipa faraja na huzuni.
Kengele yuko kwenye timu ya magamba, kaligombea kura za Maoni Ukonga akashindwa. Sasa ni mjasiriamali mzuri na ulabu wake kama kawaida. Lakini umeamsahau chacha Mwikwabe alikuwa rais kipindi cha 2000. Wengine wako kama Dr. Kitila, ni matunda pia, yoko huyo jamaa wa Ulabu, bosi Serengeti na hata Batungirehi, yuko huyo jamaa wa CUF, Makamu wa Sefu nk. list ni ndefu
Matiko Matare hakuacha kwa hiari ila alifukuzwa baada ya kuongoza mgomo mkubwa wa 1990 uliotikisa nchi kwani ulikuwa una lengo la kumwondoa Mwinyi madarakani. Sikumbuki kama Luhanga ndiye alikuwa VC. But I remember VC alikuwa Mmari. Luhanga ameanza 1991. Matiko alipelekwa kijijini kwao kwa helkopta ya serikali na kuwekewa kizuizi cha kutotoka kijijini kwao for 5 yrs. Baada ya 5yrs serikali iliendelea kumfuatilia sana kupitia idara ya usalama wa taifa hata alipokwenda kufundisha Musoma techical sec school (zamani maarufu kama musoma alliance) na baadaye mwembeni sec school hapo hapo musoma.baadhi ya watu waliokuwa wanamfuatilia ninawafahamu.Yeye nimewahi kuongea naye mara nyingi lakini nashukuru kwa kufahamu alipo sasa. Frankly speaking, yule jamaa ana uwezo mkubwa kichwani.
Umenena ukweli...Matiko amenifundisha musoma tech high school...kulitokea fujo kubwa sana...uongozi ukamtimua kuwa ndie anaetuhamasisha kugoma in 2004!
Wana JF, kuna Vijana wanaharakati enzi zile miaka ya 2000-2003, Chuo Kikuu cha Dsm tuliwahi kuwa na Viongozi shupavu sana ambao waliwahi kuweka ndani pamoja na kutimuliwa Chuo Kikuu cha DSM kwa kuongoza migomo ambayo tulifukuzwa chuo kizima na tukarudi nyumbani takribani miezi mitatu,
Uongozi wa DARUSO ulikuwa unaongozwa na msaliti mmoja aliyekuwa anaitwa Julius Kusaja, ambaye alijitoa kwenye mgomo na baada ya hapo katibu wake Mr. Gervas Mkili na Makamu aliongoza migomo mpaka wakawekwa ndani na baadaye wakatimuliwa, ila kwa baadaye tuligoma tena wakarudishwa Chuo.
Kati yao walikuwemo Zitto Kabwe, Gervas Mkili mwenyewe, Julius Rugemarila, Waziri fulani wa Fedha jina ilimenitoka, na wengine wengi. Lakini ni Zitto peke yake ambaye tayari matunda yake tunayona hadi sasa, ila wengine mlipotelea wapi baada ya Chuo maana mlikuwa very strong kuliko hata Zitto kama vile Gervas Mkili ( Shy/Khm) na Julius Rugemarila (Mwz/Bukoba).
Je kuna mwana JF yoyote ambaye anatarifa nao? tunapenda wajitokeze ili tuendelee na hii M4C ili tuweze kuwabadilisha wa Tz na kujihakikishia ushindi wa kishindo 2015, twendeni tukiunganisha nguvu kwa pamoja siyo msubiri tu 2015 baada ya ushindi ndo mjitokeze.
Ila yeye Kusaja nadhani yuko kigambagamba alitusaliti na akabakishwa UDSM utawala.
Nawasilisha ili ujumbe uwafikie michango yao ni muhimu sana.
HKigwangalla;4007387]mgomo wa mwaka 1999 - 2000 uliacha majeruhi wengi MUCHS akiwepo Dux, Alex Kazula na wengine wa mlimani kama akina Galan Mashenene...hawa ndg waliwekwa ndani kwa muda wa kutosha na benchi kwa muda mrefu, nadhani karibu a full academic year
Hebu DR. tufahamishe huyu bwana Galan Mashenene yuko wapi kwa sasa, nilipoteza mawasiliano naye Mwaka 2000, kama kuna mtu ana contacts zake naomba, ni rafiki yangu sana, huwa namtafuta si mpati.
James Mbatia alikua mmoja wapo na mangi mwenziwe Kimaro alikua pale Muhimbili sijui Kimaro kaishia wapi Mbatia naona bado yupo ngangariOh yeah, plz kuna wapiganaji makini wa miaka ya tisini katika vyuo vikuu waliopigania mfumo wa vyama vingi na kupinga cost sharing katika vyuo vikuu. Udsm,ardhi,sua,mzumbe na dar-tec. Kwa kweli walikuwa vichwa darasani na nje ya darasani lakini serikali kama kawaida iliwafrustrate kwa kuwafukuza vyuoni na kuwanyima kila nafasi ya kuendelea isipokuwa kwa wale ambao wazazi wao walikuwa na uwezo au majina na nafasi kubwa.
Wana jf wanao jua hawa mashujaa waliosahauliwa watuambie wako wapi na wanafanya nini sasa, kulikuwa na vichwa vya ajabu sana pale udsm na sua.
mzee ruksa alipata shida sana na vijana wale jinsi walivyokubalika na wasomi wenzao kwa maslahi ya taifa hili, waliweza kupindua serikali zao zilizokua vibaraka na kuunda serikali za vyuo imara. Waliadhibiwa kwa kutetea maslahi mapana ya taifa.
Anaye wafahamu atujuze tafadhali kwa manufaa ya kumbukumbu na historia ya mwanzo wa mapambano mapya ya ukombozi wa pili wa taifa hili baada ya uhuru.
Halafu watu wanasema mzee ruksa alikua mzuri. Mzuri kivipi kafunga wanafunzi wengi kuliko rais yeyote hapa Tanzania. Jamaa huwezi jua kama alikua mwalimu, nilidhani mwalimu tawapenda wanafunzi huyu jamaa sijui ni mwalimu wa madrasa sijui maana madrasa peke yake mwalimu anaruhusiwa kupiga watoto kama mbwaUDSM (Wanafunzi 10 waliofukuzwa tarehe 10 February 1992)
1. James Mbatia-Mbunge Simu: 0787 979068
2. Mosena Nyambabe-Mfanyabiashara (anakaa Ukonga Mombasa)-Amepambana mara 3 na Dr. Wanyancha katika ubunge huko Serengeti. Kwa mara ya mwisho aligombea kwa tiketi ya CUF.
3. Kelvin Mmari-Lecturer Oregon University huko Marekani. Ana uraia wa Marekani na kati ya wataalam wa kompyuta wanaoheshimika huko Marekani.
4. Fabian Lutalemwa-Sina habari naye tangia miaka ya 90.
5. Ludovick Bazigiza-Marehemu
6. Idrisa Ruta Alnoor-Marehemu
7. Jasson Kaishozi-Marehemu (Alikuwa wakili wa Serikali kesi ya Zombe)
8. Aroun Kimaro-Marehemu (Alikuwa Daktari Bingwa Zimbabwe na Mfanyabiashara mashuhuri. Alipitia mkono wa Mchungaji Mtikila)
9.Rwekamwa Rweikiza-Mhasibu. Alipata CPA mwaka 1996, nimesoma naye MBA pale UDSM na sasa anasoma digrii ya kwanza ya Sheria OUT. Vile vile ana PGDHRM ya IFM. Yuko Dar (Simu-0754 275 305)
10. Kimweri-Marehemu (Alimalizia Digrii yake ya uchumi Makerere University. Alifariki kwa ajali ya gari miaka ya 90 akiwa njiani kuelekea Zimbabwe kwa Kimaro)
Wengine
1. Matiko Matare-Aliongoza mgomo wa mwaka 1990 uliosababisha chuo kifungwe kwa mwaka mmoja. Aliacha UDSM kwa hiari kipindi kile ambapo kuliwa na njaa kali kule Musoma. Alimwambia mkuu wa Chuo (Luhanga) ampe nauli aende nyumbani kwa sababu hakuona haja ya kusoma wakati ndugu zake wanakufa kwa njaa, vingineyo angejinyonga. Wakati huo alikuwa mwaka wa 3. Mkuu wa Chuo alitii amri. Baadaye alijiunga OUT na kuwa mwanafunzi wa kwanza kumalizia digrii ya sheria kwa miaka 3. Baadaye alisoma MA (Distance Learning) hapo hapo OUT. Yuko Songea. Namba yake ni 0757 282151. Anajiandaa kurudi katika siasa kwao mkoani Mara.
DIT
1. Mtoka Mtwangi-Sina mawasiliano naye tangia miaka ya 90. Alimalizia Advanced Diploma yake Kenya Polytechnic College.