Waliouza maziwa ya watoto yenye sumu wanaswa

Pilipilihoho

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
202
145
Watu 9 wamekamatwa kwa tuhuma za kuuza maziwa ya watoto yenye sumu nchini Uchina.

Maafisa wa afya nchini Uchina wanasema wamewakamata watu hao katika kilele cha moja kati ya kashfa kadha kuhusu usalama wa wateja.
Waliokamatwa ni kati ya genge ambalo lilinua maziwa ya unga kwa bei rahisi na kisha kuyaweka kwenye makopo ya chapa ghali.

Polisi mjini Shanghai wamechunguza kisa hicho tangu Septemba mwaka jana.

Baadhi ya watu wamelalamika kuwa habari hizo zimechelewesha kutolewa.

Mwezi uliopita, wakuu waliwakamata watu kadhaa wanaotuhumiwa kuuza chanjo ghushi na zisizofaa.


Chanzo: BBC Swahili
 
huko hukumu yao inajulikana watanyongwa tu hawana mchezo ndio maana wanakuja kutuchezea huku..
 
Back
Top Bottom