Waliouawa Moshi ni majambazi kweli?

Polisi bana!
Yaani watu wana bunduki na bastola kadhaa halafu wanaenda kuiba sinki?
Ee Mungu utuokoe na hili lijambazi kuu la majuu
 
Nimeenda kushuhudia mwenyewe kwakweli inatia shaka mmoja ni kondakta wa gari za marangu mwingine ni mkaazi wa mbuyuni fundi baiskeli hawa nawafahamu vizur pas na shaka wengine watatu siwafahamu.Tetesi nyingine kuna askar wa JWTZ amejeruhiwa na wanaodhaniwa majambazi kwenye eneo la tukio.Pia waliohusika na operesheni walitoka moshi mjini

Huyu wa Mbuyuni atakuwa amefikaje hap?
 
Polisi si wa kuwaamini tena si wakweli hata kidogo tumeshuhudia mauaji ya namna hiyo watu wakiwa hawana hatia.......haiwezekani kila siku majambazi wawe wakifa na silaha washindwe hata kumjerui polisi mmoja. hizi huwa mbinu ili polisi waonekane wanafanya kazi ila ukweli hapo wameviligaviliga tu.
 
News Star Tv zimeonesha majambazi wa5 wameuawa Moshi.
Nachelea yasijekuwa mambo km ya Zombe na wafanyabiashara wa madini wa Mahenge kwa sababu:
1. Waliouawa ni wa5 ila wamekutwa na mapanga nane na bunduki na bastola kadhaa.
2. Kwamba walikuwa wanaiba sink la chooni kwenye nyumba fulani, wakalifanyie nini?

Sina imani na polisi, isije kuwa watu wameuawa na kuporwa, wakisingiziwa ujambazi.
Kama kuna eye witnesses watiririke na kuelezea scenario ilivyokuwa i.e. Kama kulikuwa na fire exchange, etc
...............NI JUKWAA LA SIASA.
 
news star tv zimeonesha majambazi wa5 wameuawa moshi.
Nachelea yasijekuwa mambo km ya zombe na wafanyabiashara wa madini wa mahenge kwa sababu:
1. Waliouawa ni wa5 ila wamekutwa na mapanga nane na bunduki na bastola kadhaa.
2. Kwamba walikuwa wanaiba sink la chooni kwenye nyumba fulani, wakalifanyie nini?

Sina imani na polisi, isije kuwa watu wameuawa na kuporwa, wakisingiziwa ujambazi.
Kama kuna eye witnesses watiririke na kuelezea scenario ilivyokuwa i.e. Kama kulikuwa na fire exchange, etc.
...................ni jukwaa la siasa.
 
Mtandao wa ujambazi,wizi wa magari Moshi-Arusha umeziibitiwa kwa kiwango kikubwa,miaka ya nyuma illikuwa hofu kubwa kutembelea hii mikoa.
 
...................ni jukwaa la siasa.

Tatizo la watu wengine humu hawajui kuwa Polisi wamepewa risasi za kuua watu na huwa wanakwenda kulenga shabaha hivyo picha inayokuwa kule mbele ni kichwa cha mtu. Ukilenga kwenye kichwa umefaulu, Hivyo basi kaa ukijua kuwa hakuna hata Polisi anayefundishwa kulenga pembeni endapo anamuona anayehusika. Uwezekano wa kufa wote ni mkubwa kama wamepigwa kwa risasi kwani askari analenga sehemu ambayo amefundishwa. Risasi zote hizo zinaagizwa toka nje ya nchi na zingine zinatengenezwa hapo morogoro zote ni kwa kumlenga binadamu. Nini kifanyike sasa ni sisi raia kujiepusha na vitendo ambavyo vitapelekea askari aamini kuwa tunafanya uhalifu kwa kufanya yaliyo mema. Hilo sinki la choo labda ulikuwa ni mwanzo tuu wa mwendelezo wa tukio na kama ni usiku je mwenye mali yake(sinki la Choo) angetokeza angeponaa. Wezi wa usiku ni hatari sana kuliko wa mchana. Kuna kitu kinaitwa probable consequense. Kwamba tukio la usiku ni likely kutokea na kifo endapo mwenye mali atatokea tofauti na mchana. Tusianze kuangalia upande mmoja tu kwa kufikiria sinki la choo tufikirie je walishamaliza kutekeleza wizi wao au walikutwa katikati ya tukio au mwanzo, au je walimtafuta mwenye mali wakamkosa kwa hasira wakaamua kuchukua sinki la choo au walikuwa wanachukuwa ili waone reaction ya mwenye sinki. Fuatilia hao watu ilikuwaje wotw wakawa eneo hilo kwa wakati mmoja. Je huyo kondakta alishapark gari na je fundi viatu alishafunga ofisi yake? je wanaishi wapi, wana ndugu maeneo hayoo. Kwa nini wauwawe wao na hali kuna watu wengine wanaume maeneo hayoo? TAFAKARI na chukua hatua acha kulalama, itafika wakati watu watakosa kabisa imani na polisi hata pale wanapofanya kazi ya maana na ikumbukwe kuwa siyo kila polisi anafanya hayo mnayofikiri. Hata ndani ya CCM kuna ambao siyo mafisadi na pia ndani ya chadema siyo wote ni safi kuna wengine wapo ili kuhakikisha cdm inasambaratika kwa vile wametumwa. Jeshi la polisi litaendelea kuwa chombo cha kulinda usalama wa raia na mali zao. Swala ni kutafuta namna ya kulifanya jeshi hilo liwe la kisasa na weled.
 
Kama ningekuwa mkuu wa polisi nisingeweza kutoa taarifa kama hii...

Naamini akitokea mtu akawabana hawa polisi, in less than 72 hrs wanaweza kuwa na ripoti tofauti zaidi ya 3, na zote zinazoelezea tukio lile lile kama ilivyotokea kule Nyololo...

After all, DCI Manumbu said that "such incidents are bound to happen again in the future"!!
 
naombeni kujua maana ya JAMBAZI,MWIZI NA KIBAKA

JAMBAZI---Ni Mwizi Anayetumia Silaha Kujipatia Mali,Huyu Afe yeye au Ufe wewe
Mwizi-Ni Mtu anayeiba mali ya mtu mwingine,huyu anadhamiria kabisa leo naenda kuiba somewhere
Kibaka-Ni mdokozi tu,anaiba akiona kitu si kama alipanga leo naiba
 
Mkuu, nadhani walikataa kutii amri bila shuruti ila kuua ni hatua ya mwisho kabisa katika mafunzo ya jeshi. Kwa vile RPC kasema kulikuwa na majibizano ya risasi na askari basi tukubali jamaa walikaidi kutii amri bila shuruti.
 
Tanzania tunaelekea wapi ?
Majambazi wakiuawa na polisi mnasema hawakuwa majambazi
Wakiachwa mnasema polisi wanakula dili na majambazi
Ngoja ninyamaze nisije nikapigwa mawe
watu sijui wakoje polisi wakiuawa hamsemi aliyejeruhiwa hamsemi, mnajua siraha walizokutwa nazo, acheni ushabiki wa kisiasa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom