Waliouawa Moshi ni majambazi kweli?

Msendekwa

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
442
168
News Star Tv zimeonesha majambazi wa5 wameuawa Moshi.
Nachelea yasijekuwa mambo km ya Zombe na wafanyabiashara wa madini wa Mahenge kwa sababu:
1. Waliouawa ni wa5 ila wamekutwa na mapanga nane na bunduki na bastola kadhaa.
2. Kwamba walikuwa wanaiba sink la chooni kwenye nyumba fulani, wakalifanyie nini?

Sina imani na polisi, isije kuwa watu wameuawa na kuporwa, wakisingiziwa ujambazi.
Kama kuna eye witnesses watiririke na kuelezea scenario ilivyokuwa i.e. Kama kulikuwa na fire exchange, etc.
 
Hapo ndipo utakapoona usanii wa jeshi letu la polisi... Arusha walishindwa hata kuwatupia jiwe wale waliomchinja kada wa CHADEMA Arumeru Mashariki lakini leo hii wanaua majambazi watano bila tatizo lolote. Nini kiliwazuia kuwashughulikia wale wa Arusha??
 
Du? Kusema kweli hili jambo limenishtua sana,kwani limenikumbusha mauaji kama haya yaliwahi kutokea tena benki ya nmb kilombero branch morogoro waliuawa 7.kusema kweli hawa majambazi wameunda kundi kubwa pande za marangu na wanasilaha nzito.haijapita mwezi waliua na kupora mfanyabiasha wa nyama kiasi cha sh milion10.kama kweli ndo wahusika basi sichelei kulipongeza jesh letu la polis
 
Tanzania tunaelekea wapi ?
Majambazi wakiuawa na polisi mnasema hawakuwa majambazi
Wakiachwa mnasema polisi wanakula dili na majambazi
Ngoja ninyamaze nisije nikapigwa mawe
 
Nimeenda kushuhudia mwenyewe kwakweli inatia shaka mmoja ni kondakta wa gari za marangu mwingine ni mkaazi wa mbuyuni fundi baiskeli hawa nawafahamu vizur pas na shaka wengine watatu siwafahamu.Tetesi nyingine kuna askar wa JWTZ amejeruhiwa na wanaodhaniwa majambazi kwenye eneo la tukio.Pia waliohusika na operesheni walitoka moshi mjini
 
Tanzania tunaelekea wapi ?
Majambazi wakiuawa na polisi mnasema hawakuwa majambazi
Wakiachwa mnasema polisi wanakula dili na majambazi
Ngoja ninyamaze nisije nikapigwa mawe

Haya manachama ya CDM majinga na hayeleweki! zao ni kupinga tu kila jambo!
 
Hivi kama ni majambazi haiwezekani mkajeruhi? Ni mpaka muwauwe wote? Tunataka ufafanuzi hapa!
 
polisi wa tanzania hawaaminiki kwa jema wala baya, CCM imewageuza wamekuwa kama chumvi iliyooza hainaga matumizi zaidi ya kutupwa.
 
News Star Tv zimeonesha majambazi wa5 wameuawa Moshi.
Nachelea yasijekuwa mambo km ya Zombe na wafanyabiashara wa madini wa Mahenge kwa sababu:
1. Waliouawa ni wa5 ila wamekutwa na mapanga nane na bunduki na bastola kadhaa.
2. Kwamba walikuwa wanaiba sink la chooni kwenye nyumba fulani, wakalifanyie nini?

Sina imani na polisi, isije kuwa watu wameuawa na kuporwa, wakisingiziwa ujambazi.
Kama kuna eye witnesses watiririke na kuelezea scenario ilivyokuwa i.e. Kama kulikuwa na fire exchange, etc.

Mkuu hawa Polisi siku hizi wanaweza kufanya chochote na wakatoa maelezo wanavyopenda. Huwa hata sina imani nao hata kidogo
 
Kama ni majambazi hivi ni lazima wafe wot! Kwa nini msimjeruhi hata mmoja ili muwe na ushahidi? Hii siyo sawa kila jambazi anauwawa tu! Tena wa tano!
 
Kwani Adhamu ya Jambazi / Kibaka Lazima iwe Ni kifo? Hii Inatia shaka!! Leo Kuna ndugu zangu walikuwa pale Landmark wanahubiri Haki ya kuishi amayo naona sasa Jeshi la Polisi Halitilii maanani sana!! Kazi Yao Imekuwa ni Kuua Tuu!! Nawaomba Wafuatilie Hadi Haki Itendeke!! Wananchi wenye Hasira wakiua polisi wanasema tuache kuchukua sheria mkononi!! Je polisi Manavyoua Tusemeje?
 
Haya manachama ya CDM majinga na hayeleweki! zao ni kupinga tu kila jambo!

Suala sio u CDM, CCM au CUF, ni ukweli kuhusu tukio.
Majambazi wa 5, wenye bunduki na bastola, wenye mapanga 8,
wanaenda kuiba sink la chooni, wanakutwa na kuuawa bila wao kumjeruhi askari au kurushiana risasi!
Mwenye akili lzm ajiulize maswali, bila kubeza uwezo wa polisi wetu(waliomuua Mwangosi)
 
Haya manachama ya CDM majinga na hayeleweki! zao ni kupinga tu kila jambo!

Mkuu haya manachama ya CDM siyo kwamba yanapinga tu. Tatizo ni ukweli wa Jeshi lenyewe. Wenye imani na Polisi kwa sasa ni CCM tu. Angalia vitendo wanavyofanya. Yaani kwa sasa polisi haina msaada tena kwa jamii ya kawaida. Sasa hivi wananchiwanajilinda wenyewe bila kutegemea polisi tena
 
Nimeenda kushuhudia mwenyewe kwakweli inatia shaka mmoja ni kondakta wa gari za marangu mwingine ni mkaazi wa mbuyuni fundi baiskeli hawa nawafahamu vizur pas na shaka wengine watatu siwafahamu.Tetesi nyingine kuna askar wa JWTZ amejeruhiwa na wanaodhaniwa majambazi kwenye eneo la tukio.Pia waliohusika na operesheni walitoka moshi mjini

je kuwa kondakta kunamfanya aasiwe jambazi ama kuwa fundi baiskeli?
 
Hivi kama ni majambazi haiwezekani mkajeruhi? Ni mpaka muwauwe wote? Tunataka ufafanuzi hapa!
Naona sasa mpaka nyinyi Majambazi mnataka kuundiwa Tume na Kamati kwa uchunguzi wa kupata adhabu mnayostahili!
Acha ujambazi haraka..la sivyo ukiingia kwenye 18 wanaume hatutakujeruhi..jibu unalo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom