Waliotudanganya wafanyweje?

Mopao Joseph

Member
Jul 1, 2009
34
0
WALIOTUDANGANYA WAFANYWEJE?
Wananchi wa mara walilalamika sana kuhusu kitendo cha wahusika wa mgodi wa north mara kumwaga sumu kwenye mto tigeti ambao maji yake yanatumiwa na wananchi wenyewe pamoja na mifugo yao.
HOJA,
alienda naibu waziri akadanganywa nae akadangaya umma.
ikaundwa tume ya wataalam chini ya waziri wa........`MAZINGIRA`.
WALIOTUDANGANYA WAFANYWEJE?
nawakilisha!!!!!
 
WALIOTUDANGANYA WAFANYWEJE?
Wananchi wa mara walilalamika sana kuhusu kitendo cha wahusika wa mgodi wa north mara kumwaga sumu kwenye mto tigeti ambao maji yake yanatumiwa na wananchi wenyewe pamoja na mifugo yao.
HOJA,
alienda naibu waziri akadanganywa nae akadangaya umma.
ikaundwa tume ya wataalam chini ya waziri wa........`MAZINGIRA`.
WALIOTUDANGANYA WAFANYWEJE?
nawakilisha!!!!!

Kama serikali yetu ingekuwa inajali maslahi ya umma na kama ingekuwa inajali utawala bora, viongozi wote walioshiriki kudanganya kuanzia mkoani hadi wilayani wangewekwa pembeni kwa maslahi na ustawi wa umma lakini kwa serikali hii tuliyonayo hata tukishauri sidhani kama kuna hatua yoyote itachukuliwa.Labda tu tuendelee kupiga soga hapa na kutoa mapendekezo au maoni kwa ajili ya mustakabali wetu wa baadae, kwa kuwa tunao wajibu wa kuikumbusha serikali kutimiza majukumu yake ipasavyo, ingawa ilitakiwa serikali yenyewe itende bila kusubiri kukumbushwa au kuambiwa.
 
Hii serikali imeoza unafikiri hata tukisema wachukuliwe hatua waliodanganya watachukuliwa basi,watalindana-lindana mwishowe wananchi wanasahau na issue inakuwa imeisha wakati wapo waliopoteza maisha.
 
Kwanza kabisa Barrick inabidi walipe fidia kwa wote waliopoteza maisha ikiwa pamoja na kuendelea kutoa huduma kwa wote waliokuwa wakiwategemea kama watoto na wazee.

Pili Barrick itoe fidia na kusaidia matibabu a hali ya juu kwa wote waliopata athari kutokana na kunywa maji hayo.

Ilipe gharama zote za mifugo iliyokufa na kuathirika.

Viongozi wote kuanzia ngazi ya kata, tarafa, wilaya na mkoa wanatakiwa wawajibishwe na kushitakiwa kwa kuficha habari hizi kwa mujibu wa sheria.

Barrick ishitakiwe kwa kuleta maafa na madhara kwa jamii
 
yaani hali inatisha , ukiangalia watoto walivyoshikwa sijui mba, au fangasi yani vitu havieleweki utaona huruma.
Unadhani watafanywa nini? , tuko kwenye uchunguzi tume ziudwe mpaka ripoti itoke watu tumesahahu.
 
Back
Top Bottom