Waliotimuliwa Chadema waomba huruma ya korti

Sijapata kuona majitu majinga kama hawa Madiwani, wanasingizia kuwatumikia wananchi, kumbe wanataka kutumikia matumbo yao!
Na kama lengo lao ni kuwatumikia wananchi kwani ni lazima iwe ndani ya vikao vya halmashauri? Shenzi yao!
Nitamshangaa sana hakimu katika hili!

Mkubwa!
Makini sana!

Nikivamia ktk mitambo mikubwa,ntaibofia kitufe cha LIKE!
 
Wote hawa pamoja na akina Hamad nikujipotezea muda na pesa zao, kwani chama kina sheria zake na taratibu zake, na si rahisi kutengua uamuzi ambao ulishatolewa katika kikao kinachotambuliwa na chama.

Hata wenyewe wakirudishiwa haki za madai yao watajisikiaje ndani ya chama? Ni kupoteza muda tu.
 
Mussa Juma, Arusha
MADIWANI watano wa Jiji la Arusha waliotimuliwa uanachama na Chadema, wameomba Mahakama Kuu kuwarejesha kutumikia nafasi zao wakati wakisubiri uamuzi ya kesi ya msingi kupinga kufukuzwa kwao.


Katibu wa madiwani hao, John Bayo, alisema waliwasilisha maombi hayo Mahakama Kuu jana, ili wananchi waliochagua waendelee kupata haki yao ya kuwakilishwa.


“Katika maombi yetu tunaomba Mahakama Kuu, iturejeshe kutumikia wananchi wakati kesi ya msingi ikiendelea, kwani wananchi tunaowakilisha wanakosa uwakilishi kwenye baraza la madiwani,” alisema Bayo.


Bayo alisema kesi hiyo inatarajiwa kutajwa Januari 19, mbele ya Jaji Fatuma Massengi na tayari walalamikiwa wamepewa hati ya kuitwa mahakamani.


“Kama unavyoona muda huu natoka kuwapelekea walalamikiwa ambao ni Chadema na (Freeman) Mbowe, hati ya kuitwa Mahakama Kuu Januari 19 na tumempa nakala Kaimu Mkurugenzi wa Jiji,” alisema Bayo.


Aliongeza kuwa wanaamini mahakama itawarejeshea udiwani wao wakati shauri lao likisikilizwa, kwani ni haki yao kuendelea na majukumu ya kusaidia wapiga kura wao.


Madiwani wengine waliofukuzwa na kata kwenye mabano, ni aliyekuwa Naibu Meya, Estomih Mallah (Kimandolu) Charles Mpanda (Kaloleni), Reuben Ngoi (Themi) na Diwani wa Viti Maalumu, Rehema Mohamed.


Kufukuzwa kwa madiwani hao, kulitokana na kukaidi agizo la kamati kuu ya chama hicho, kuwataka kujiondoa katika mwafaka wa uchaguzi wa Meya wa Arusha na madiwani wa CCM na kuomba radhi kwa kuingia mwafaka bila ridhaa ya chama.


Hata hivyo, madiwani hao waligoma kujiondoa katika mwafaka na kuomba radhi, wakisisitiza kumtambua Meya wa CCM, Gaudence Lyimo na kufikia uamuzi wa kugawana nyadhifa mbalimbali ni halali.

"Mwananchi" -Hamadi Rashid Aibana CUF mahakamani



- Waiotimuliwa CHADEMA waomba huruma ya mahakama


Unazi, unazi, unazi na uchonganishi basi!
 
#1 rutashubanyuma 2012-01-11 08:30
ninaamini wanahoja ya kimsingi kabisa.........waendelee kutumikia wananchi hususani vyama vya siasa havina demokrasia........iwaje diwani awasikilize makao makuu ambao hata hawakumchagua..........

Kwani walichaguliwa wakiwa wagombea binafsi?
 
Hawa wa ajabu kweli,yani mpaka leo bado wana matumaini ya kuwa wana CDM? Pambafu zao waende wakale jeuri yao sasa

wanajaribu kusafiria nyota za kina hamad rashid na kafulila, hawana lolote na usikute magamba wameshawatupa mithili ya kondoumu ilokwishatumika
 
Wote hawa pamoja na akina Hamad nikujipotezea muda na pesa zao, kwani chama kina sheria zake na taratibu zake, na si rahisi kutengua uamuzi ambao ulishatolewa katika kikao kinachotambuliwa na chama.

Hata wenyewe wakirudishiwa haki za madai yao watajisikiaje ndani ya chama? Ni kupoteza muda tu.

njaa haina adabu mkuu
 
Back
Top Bottom