Waliotegemea malipo ya uzeeni ujanani sasa tena basi! Ufafanuzi kutoka Mamlaka - SSRA

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,752
5,494
Ufafanuzi Kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhitibi wa Hifadhi ya Jamii

UFAFANUZI KUHUS FAO LA KUJITOA KATIKA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII.

Ufuatao ni ufafanuzi mfupi kuhusu marekebisho ya Sheria za Mifuko hasa kuhusu fao la kujitoa.

1. Kama mtakumbuka Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili, 2012. Sheria hiyo tayari imeshasaininiwa na Mheshimiwa Rais na imeanza kutumika rasmi. Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini mwetu bila kubagua sekta yoyote ile.

2. Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa (withdrawal benefits) yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko atapata mafao yake pale atakopfikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.

3. Kwa kuzuia fao la kujitoa mwanachama anapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye Sheria ya SSRA kipengele cha 38.

4. Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni wakati ambapo nguvu ya kufanya kazi tayari imeshamwishia. Mafao ya kujitoa yanapunguza na hata kuondoa kabisa kinga ya mfanyakazi pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.

5. Tunawaomba muwaelimishe wafanyakazi umuhimu na madhumuni ya mafao ya hifadhi ya jamii. Hifadhi ya jamii ni nyenzo mahususi iliyowekwa kuwasaidia wafanyakazi kuendesha maisha yao wakati wanapokuwa wameishastaafu tayari. Umasikini wa kipato wakati wa uzee ni mojawapo ya changamoto ngumu kukabiliana nazo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Tunawasihi tena muelimishe wafanyakazi kuhusu jambo hili. Tafadhali msisite kuwasiliana na Mamlaka pale ufafanuzi zaidi utakapohitajika

6. Kwa kuwa marekebisho hayo yamesainiwa na kuanza kutumika rasmi kama sheria, mafao ya kujitoa hayawezi kutolewa tena na wafanyakazi watakaoacha kazi kwa sababu ya marekebisho ya kipengele hicho watakuwa hawajaijitendea haki wao wenyewe na pia itakuwa ni kunyume cha Sheria. Mamlaka inaandaa kanuni za mafao ambayo lengo lake ni kuboresha maslahi ya wanachama, kanuni hizo zitajadiliwa na wadau wakiwemo vyama vya wafanyakazi na waajiri ili kupata maoni yao.

7. Tafadhali muwaelimishe wafanyakazi kwamba pamoja na kuzuia fao la kujitoa, mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya Madini yataendelea kutolewa kama kawaida. Mafao hayo ni Kama vile kuumia kazini pamoja na fao la ulemavu

8. Tumesikia kwamba tayari kuna hofu imejijenga kwa wanachama kuhusiana na fao la kujitoa. Ikumbukwe kwamba baadhi ya Mifuko ilikuwa inatoa fao hilo kinyume cha Sheria kwani katika Sheria zao hakuna fao la kujitoa. Tunapenda kusisitiza kwamba wanachama wawe watulivu wakisubiri miongozo.

9. Tunapenda kuwahakikishia kwamba katika hili maslahi ya wanachama yatalindwa na hakuna mwanachama atakayepunjika kutokana na utaratibu huo. Mamlaka imepanga kutembelea wafanyakazi wa sekta ya madini katika juma la kwanza la mwezi Agosti 2012 ili kutoa ufafanuzi zaidi kwa wanachama wote.

Tunatanguliza shukrani za dhati kwa ushirikiano.

Wenu.
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii

Irene Isaka
MKURUGENZI MKUU
 
Bila kuwa na sheria ya Unemployment Benefits (au inayofanana na hiyo) hili sio wazo zuri hata kidogo.
 
1. je wakiniachisha kazi inakuwaje?
2. kwa wale wanaoacha kazi je mafao yao ndio hawatayapata tena au wakifikisha hiyo miaka 55 wakiwa hai wanaweza kupewa??
3. hiyo sheria haitendi haki kama ni hela yangu ya mshahara ninayokatwa nina haki ya kuichukua pale nitakapoacha kazi kwasababu ni haki yangu nimeifanyia kazi siyo ya kupewa.
4. wakati mwanachama anaendelea kuchangia akiwa kazini aruhusiwe kukopa kwa riba nafuu badala ya kuwakopesha wakina manji ili imwezeshe kimaisha badala ya kwenda kuumizwa na sacoss na mabenk.
 
me nilipanga kuacha kazi pale michango yangu inapofika 15 mil. na hii inatimia mwakan nikiwa nia ni kuchukua hiyo pesa na kuanza kuendeleza biashara zangu.
nikiwa kijana wa miaka 30 sijatendewa haki kusubiri another 25 yrs. what if i didnt make it?
 
wakuu hii ni habari ya kuaminika. hakuna kijana anayependa kujitegemea kwa nguvu zae anapenda hii habari kabisa. ila baadhi ya makampuni tayari barua hii waeshatumiwa na huyu mkuu. sijui itakuwaje
 
3. Kwa kuzuia fao la kujitoa mwanachama anapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye Sheria ya SSRA kipengele cha 38.

Naomba mwenye taarifa za hii mikopo atueleze jinsi ya kuipata.
 
Mi nashaang'aa hii nchi inavyoendeshwa,mbona mwezi wa nne mi nilisikiliza bunge na sijasikia kitu hiyo inaongelewa na mpaka kumpelekea rais kusaini.
Hapa itakuwa hawa jamaa wa serikari wamechota hela kwenye hizo fund wakashindwa kurudisha wkt watu wanadai hela zao ndo wakaona waitungie sheria.
Du!ama kweli hii nchi!
 
Huu ni ubabe uliopitiliza aisee.
Kwa kweli!!
Nashangaa hawa jamaa wanataka kujikopesha hela zetu, sioni sehemu waliposema what happens nikiamua kuacha kazi!!
Ina maana nisubiri mpaka 55?? Why na hela ni yangu? Hapa katikati kwanini nisichukue hela yangu?
 
Irene Isaka, mtoto wa kawaida aliyekulia Dodoma, na wazazi humble sana, LEO ANAJISAHAU KWAMBA HATUNA
UNEMPLOYMENT BENEFIT
ROBUST SOCIAL SUPPORT SYSTEMS
CORRUPT LOAN SYSTEMS
WEAK SECURITY FUNDS ADMINISTRATION

ANABEHAVE KAMA VILE TUKO DEVELOPED COUNTRIES?????

Roho imeniuma kiukweli na wala si kijeiefu!!!

Hivi milioni arobaini ya leo hii with my early fourties itakua na maana 20 years to come??? will they make neccesary adjustment kutokana na currency fluctuation??

sad!!
 
Life span ya mtanzania iko average ya 44yrs! Mafao 55yrs! Kazi tunayo!
 
Huu ni wizi wa mchana kweupee!!Yaani nikiacha kazi kabla ya miaka 55 hela mnayonikata kila mwezi mnaichukua nyie?Au labda sijaelewa vizuri?
 
Kuna mtu anakumbukumbu na hii sheria kuwa ilishapata baraka za bunge kweri? Ufuatao ni ufafanuzi mfupi kuhusu marekebisho ya Sheria za Mifuko hasa kuhusu fao la kujitoa.

1. Kama mtakumbuka Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili, 2012. Sheria hiyo tayari imeshasaininiwa na Mheshimiwa Rais na imeanza kutumika rasmi. Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini mwetu bila kubagua sekta yoyote ile.

2. Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa (withdrawal benefits) yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko atapata mafao yake pale atakopfikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.
 
Sijaelewa bado.....

2. Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa (withdrawal benefits) yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko atapata mafao yake pale atakapofikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.
 
Bado tunahitaji ufafanuzi mkubwa tu!kama nimeacha kazi nikiwa na 40yrs nitasubiri hadi 55yrs?ndio nichukue pesa zangu ama vipi?mbona hawakushirikisha vyama vya wafanyakazi na wafanyakazi wenyewe?kwa nini wanajipa mamlaka ya pesa zetu?ambalo ni jasho letu!!!unahitajika mjadala mkubwa sana tu!!hiyo sheria ndio itawatoa madarakani mapema zaidi ya muda!!haiwezekani wakae semina na kuamua hatma za pesa za wavuja jasho bila kuwashirikisha!kwa nini??kama wameshindwa kupata sehemu kukopeshana na serikali,wavunje hiyo mamlaka haina tija na itabidi hii issue tuiulize bungeni kupitia wabunge wetu mashujaa sio vilaza wapiga makofi!imejadiliwa lini?au ndio wanatudhihirishia kuwa hawana shida na kura za wafanyakazi???
 
Duu hii kali, kusubiri mpaka miaka 60? Wanamapenzi mema kweli na sisi, mimi ndio kwanza nina miaka 29, nisubiri tena 31yrs hata kama nikiacha kazi kesho. Hivi hili lilipita bungen kweli au lilipita kwa mlango wa nyuma? Wabunge wetu mlipitisha kweli hili? Hela zetu wanafaidi wengine, sisi hata mkopo hatupati? Hapa hakuna haki. Mi nilijiwekea target nikifikisha mil kadhaa naacha kazi naenda kudraw naanzisha mradi wangu. Ndoto yangu yote leo imepotea. Shame on u...!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom