Elections 2010 Waliotangaza kura feki Tunduma wapata dhamana

buckreef

JF-Expert Member
Mar 19, 2010
309
40
Waliotangaza kura feki Tunduma wapata dhamana
Saturday, 30 October 2010 Mwananchi

Stephano Simbeye, Mbozi

VIONGOZI wawili wa Chadema, kata ya Tunduma, wanaokabiliwa na kesi ya kutoa taarifa za uongo kuhusu kukamatwa ‘karatasi za kupigia kura, wameachiwa kwa dhamana na kutakiwa wasijihusishe na siasa.

Washitakiwa hao ni pamoja na Victor Mateni ambaye ni Mtunza Hazina wa Chadema kata ya Tunduma, na Joseph Machemba ambaye ni Mwenyekiti wa mtaa wa Sogea, Tunduma wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.

Hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya Rahimu Mushi akitoa masharti ya dhamana aliwataka kila mshitakiwa awe na wadhamini wawili na fedha kiasi cha Sh 1 milioni kwa maneno.

Aliongeza kueleza sharti lingine kuwa hawatapaswa kujihusisha na masuala ya Kisiasa yanayoweza kuleta machafuko na kusababisha uvujifu wa amani, na kuwa kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Novemba 4,mwaka huu.
Aidha washitakiwa hao walisimama kizimbani kwa mara ya kwanza Oktoba 20 mwaka huu kujibu shitaka la kutoa taarifa za uongo kwa Mtumishi wa Idara ya Forodha aitwaye Jovita Kanimba Charles ambapo dhamana dhidi yao ilizuiliwa.

Ilidaiwa kuwa Oktoba 17 mwaka huu mshitakiwa Victor Mateni, alipata taarifa kutoka kwa mwenyekiti wake Joseph Machemba wote viongozi wa chama hicho kata ya Tunduma kuwa kuna lori lilikuwa limebeba karatasi feki za kupigia kura zilizowekewa alama (Vema) kwa mmojawapo wa wagombea ngazi ya urais.
Habari hizo zilienea haraka nchini na kumfikia mgombea wa urais kupitia chama hicho Dk Willibrod Slaa ambaye aliamua kutangaza taarifa hizo kwenye mkutano wake wa kampeni.

Dk Slaa alisema gari hilo lilikuwa limepakia vipodozi pamoja na karatasi la kura zilizochakachuliwa.

Hata hivyo vyombo vya dola kupitia polisi wa Mkoa wa Mbeya walikanusha taarifa hizo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom