Walioshinda Zabuni TANESCO wakimbilia Mahakamani!

Kama habari iliyoandikwa na mwandishi Exavery Mzuzu wa Dira ya Mtanzania itakuwa kweli, basi sakata la zabuni ya mafuta TANESCO litachuma mapesa mengi kuliko linavyodhaniwa kuokoa. Mwandishi huyu anaripoti kuwa makampuni yaliyoshinda zabuni kabla ya kutenguliwa na katibu mkuu Maswi yamekimbilia mahakamani kudai fidia. Sasa sijui hili suala kisheria limekaaje, maana hawa PUMA walichofanya ni kuchungulia wenzao wametoa offer kiasi gani halafu wao wakashuka chini yao. Je hii siyo unfair competition?

Pia hivi hatuoni kuwa kuna madhara makubwa sana kama tutaruhusu individuals kuingilia michakato ya kisheria kwa kigezo cha kuokoa "maslahi ya taifa?" Kitendo hiki hiki tunachokiona ni cha kishujaa leo hii, baadaye kitatuumiza vibaya sana. Ni uzalendo huu huu ndio uliogeuka mwiba mchungu kwa Mh. Lowasa. Kwani ilikuwa ni lazima mshindi wa zabuni apatikane kama makampuni yaliyoomba yalitoa bei kubwa? Sheria za manunuzi ya umma zinasemaje kuhusu hili? Kwa nini zabuni isingetangazwa tena ili kuruhusu makampuni zaidi kushiriki (wakiwemo PUMA)?

Kauli aliyotolewa na waziri kuwa wanaodhani bodi haitaingiliwa wanajidanganya inaiweka wapi bodi. Je, kautamaduni haka kakijichimbia mizizi si ndio itakuwa loophole ya ufisadi? Tunashangilia leo bila kujua nini kinakuja kesho. Si lazima itokee kwa waziri aliyepo sasa, inaweza kutokea hata katika wizara nyingine pia, na tutapaswa kuwaelewa na kuheshimu uzalendo wao.

Suala jingine la msingi kabisa hapa: kama kweli PUMA nao walishiriki zabuni ya kwanza na bei yao ikawa juu hadi walipogundua wameshindwa ndipo wakashusha, walitaka kufanya ufisadi pia? Vipi kama makampuni mengine nayo yangepewa nafasi ku-bid kwa kigezo kuwa mshindani wao PUMA kashusha bei, je kuna uwezekano tungewezapata bei chini zaidi ya hiyo 1460/=?

Disclaimer: Mimi si msomi wa sheria za manunuzi au sheria kwa ujumla. Hii ni tafakuri yangu tu.

As long as mkono yupo kwenye hilo sakata, ni lazima waende mahakamani, kwani si ndio huko anakopatia hela yake kwa kushirikiana na majaji wapuuzi.
 
Lakini pia mkumbuke kuwa ki-mkataba anayetakiwa kununua mafuta kwenda IPTL ni serikali wala si TANESCO walikuwa wanafanya hivyo kuhalalisha wizi na kurahisisha migawo.kwa maana nyingine hiyo tender ni batili pia kwani TANESCO alijitwalia jukumu lisilo lake
Hili ni jipya sasa. Kama hili unalosema ni la kweli basi tuna tatizo kubwa zaidi.

Shida yangu kubwa katika suala hili ni kampuni ya PUMA kutoshindanishwa na makampuni mengine kabla ya kupewa zabuni hiyo (hata kama anayenunua ni serikali na sio tanesco!).
 
Kama nilivyomuelewa waziri, alisema kuwa Puma walikuwapo kwenye bidding ya kwanza na kwa bei hiyo hiyo ya chini wakatoswa.Haya makampuni mengine wakapewa kwa mkataba wa 1500 Tshs kwa lita arround there, lakini ilipofika kwenye malipo wakawa wanalipwa 1800 tshs kwa lita. Nadhani tatizo liko hapo maana yake walikiuka mkataba tayari. Labda tufuatilie tena kuujua ukweli kwenye hili.

Ndugu yangu Ndukidi kuna mahali nimemweleza mleta thread Nyenyere kwamba lazima kuna mambo ambayo yamejificha ambayo sisi hatuyajui. Kwakuwa sitaki kuamini kwamba katibu mkuu Maswi aliamua kubatilisha zabuni hiyo na kuwapa Puma bila kujiridhisha kama taratibu zilifuatwa.
Kama maelezo yako ni sahihi basi hapa kuna mengi yaliyofichika katika zabuni hii ambayo kama kweli wanakwenda mahakamani, basi yatawekwa hadharani na ndipo tuatajua nani ni nani katika sakata hili.

Kama walishinda zabuni kwa bei ya sh.1,500 kwa lita lakini wakalipwa Tsh.1,800 basi hapo ni wazi kwamba kulikuwa na harufu ya rushwa, na huenda PUMA walienguliwa kimizengwe toka hatua za awali ili kukamilisha dili.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: SMU
Mr. Maswi is not the CEO of TANESCO. Which law gives him the powers to vary the decision of TANESCO's tender award? Haya shauri zetu!!
 
Mr. Maswi is not the CEO of TANESCO. Which law gives him the powers to vary the decision of TANESCO's tender award? Haya shauri zetu!!

Ki-mkataba mwenye mamlaka ya kununua mafuta na kusupply IPTL ni serikali kupitia Wizara ya nishati na madini
 
Kama ulisikiliza vizuri siku waziri nanfanya majumuisho ya hotuba yake alisema hivi: KI-mkataba mwenye mamlaka ya kuuza mafuta IPTL ni wizara ya nishati na madini.Na akasema kuwa mkataba waliweka kama silaha yao ya mwisho kuitoa ktk sakata hili wengi hawakujua kuwa si TANESCO anajulikana ki-mkataba kuwa ni mnunuzi isipokuwa ni wizara,kwa maana nyingine TANESCO walikuwa wanatumika kurahisisha wizi
 
Kama ulisikiliza vizuri siku waziri nanfanya majumuisho ya hotuba yake alisema hivi: KI-mkataba mwenye mamlaka ya kuuza mafuta IPTL ni wizara ya nishati na madini.Na akasema kuwa mkataba waliweka kama silaha yao ya mwisho kuitoa ktk sakata hili wengi hawakujua kuwa si TANESCO anajulikana ki-mkataba kuwa ni mnunuzi isipokuwa ni wizara,kwa maana nyingine TANESCO walikuwa wanatumika kurahisisha wizi

Kwa hiyo mawaziri waliotangulia wana kesi ya kujibu!
 
Vipi unaogopa mahakama? yes hofu yako ina maana saana but haina msingi sana, issue hapa ni wanasiasa ccm na wafanyabiashara ccm, na Waathirika ni Maskini watanzania,tusubiri tuone, may be ni upepo tu coz tanzania kila siku lazima issue ya kifisadi itoke
 
Hii yote ni kitu gani kama siyo vita ya wenye nguvu wachache kupigania rasilimali za watanzania kwa manufaa binafsi? UDHAIFU wa serikali kushindwa kununua mafuta yenyewe ndio unaotufikisha hapa. Hii public and private partneship(PPP) imevaa joho lingine la ufisadi. System hii inaanzishwa tena bila kufanya utafiti wa efficiency yake huku lengo likiwa kuwapa ulaji mafisadi wachache kwa kigezo cha kufanya kazi na private sector.
 
Hii ya mahakamani ndio itakuwa nzuri. Mahakamani maswali mengi ya msingi yataulizwa. Tutajua mengi zaidi!!
Nahisi kwamba kinachojulikana mpaka sasa ni tip of an iceberg.
 
Tena ni WIZARA YA NISHATI NA MADINI.

Watanzania wenzangu mgogoro hapa siyo Wizara ama Tanesco analipa pesa za mafuta,kiini cha tatizo ni Mkataba mzima kati ya Serikali/Tanesco na IPTL. Naiona Dowans nyingine ikikamua pesa za bure za walipa kodi wa nchi hii.
 
Nilidhani tungeangalia uwezekano wa kuzirudisha bilioni 6 za kila mwezi zilizokwapuliwa na mafisadi hawa kwa kipindi chote hiki kwa kuwa mkataba walioingia na TANESCO ambao ni batili tokea mwanzo kumbe bado tunaleana tu!
 
Bodi kitu gani bana? Bodi ya korosho ya M/kiti Ana si yala tu mapesa? Inamsaidiaje mkulima. Bodi ziwe na wataalamu siyo wanasiasa
 
Maswi hakununua mafuta bali alielekeza yanununliwe PUMA, serikali kama financier ingependa kupata value for money though wizara haikuwa mnunuzi. RITA walielekezwa waishauri TANESCO watumie section 42 ya emergency procurement baada ya kuonekana hitaji la kuwasha mitambo ya IPTL ambayo iko chini ya RITA lakini Mhando akafanya mchakato wa kawaida wa kuitisha tenda kabla ya maelekezo kutoka RITA, note that Maswi baada ya kufahamu kuwa PUMA wana bei ya chini alielekeza mafuta yanunuliwe kwao under emergency situation ambapo bodi ya zabuni haihusiki.

Cha kutazama hapa ni kama TANESCO walipeleka taarifa PPRA kulingana na Section 31(3) ya PPA 2004 na pia kama taarifa pia ilipelekwa kwa Paymaster General ili baadaye uchunguzi ufanyike kama kweli kulikuwa na emergency situation na kama haikuwepo njia nyingine ya ushindani ingetumika mafuta yangenunuliwa kwa bei gani? na kama itakuwa ya chini ya iliyotumika, ile tofauti ya total amount itabidi Mhando ailipe.

Kwa ujumla msimamizi wa manununzi ya taasisi ni Accounting Officer kwa hivyo yeye ndiye atawajibika kama hakufuata sheria ya manunuzi. Wizara ilitoa pesa na yeye alipaswa kuzingatia sheria na vingenevyo kushauri yapasayo kufanywa but in total value for money iwe achieved na si emergency situation itumike kuwaambia wazabuni niwekee za kwangu knowing that ni lazima mafuta yanunuliwe because there is an emergency!!!!
 
Ninachoona hapa ni vita vya kupigania maslahi binafci.. Inanikumbusha kasheshe ya kuchelewa project ya vitambulisho vya taifa pamoja ni hii ya karibuni iliomuondoa Nundu na Mfutakamba.. Masharti na vigezo havizingatiwi kabisa..!
 
Back
Top Bottom