Waliopenya CCM Singida watajwa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797


na Jumbe Ismaily, Singida


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida kimetangaza majina ya wanachama walioteuliwa kugombea nafasi mbalimbali kwenye jumuiya za chama hicho.


Katibu wa CCM Mkoa, Naomi Kapambala, alisema kuwa majina ya wagombea hao yaliteuliwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa kilichofanyika juzi.

Aliwataja walioteuliwa kugombea nafasi ya uenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi katika Wilaya ya Iramba kuwa ni Joseph Kidondela, Monica Samwel na Selemani Nyamswa wakati Amina Emmanuel, Asha Mohamed na Ukende Mkoma wanagombea Halmashauri Kuu ya CCM wilaya.


Wagombea uenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Singida Mjini ni Jenipha Miano, Hawa Athumani na Neema Omari, wakati Halmashauri Kuu ya wilaya ni Zainabu Abrahamani na mkutano mkuu wa wilaya ni Maria Mkumbo.


Vijana waliopendekezwa kugombea nafasi ya uenyekiti ni Ahmed Makame, Athumani Rajabu na Ziyana Mtue wakati mkutano mkuu wa wilaya ni Belinda Matalu, Mary Mkoma na Athumani Rajabu huku Halmashauri Kuu ya wilaya ni Emmanuel Yindi, Simon Mpinga na Muungano Senyangwa.


Kapambala aliwataja waliopenya kugombea nafasi mbalimbali kwa jumuiya ya wazazi wilaya mpya ya Ikungi kuwa ni Anthony Itambu, Mussa Mkanga na Shabani Mtakii kwenye uenyekiti wakati Halmashauri Kuu ya wilaya ni Hamisi Nyawita,Yusufu Mwandani na Christina Samweli.


Uenyekiti wa UWT walipenya Helena Ayubu, Christina Petro na Theresia Nkuwi wakati Halmashauri Kuu ya Wilaya ni Magreth Stephano na mkutano mkuu wa wilaya ni Secilia Hongoa na Chiku Mwanja.


Kwa UVCCM ni John Kughanji, Ntandu Ntandu na Yuna Mwangu, Halmashauri Kuu ya ni Jafari Dude, Mdai Mjau na Gertrude Gwae na mkutano mkuu ni Elias Samweli, Ramadhani Mangu na Shabani Mangida.


Alisema kwa Wilaya ya Manyoni waliopendekezwa nafasi ya uenyekiti kupitia wazazi ni Hemed Hamada,Yahaya Masare wakati Halmashauri Kuu ya wilaya ni Pili Kasika na Geofrey Carata.


UWT wilaya walipita Elizabeth Bajile, Neema Mwitikizi na Mwanahawa Yussufu wakati Halmashauri Kuu ni Ashura Ngande na Asnath Mwanasi huku Mwanne Abubakari akigombea Halmashauri Kuu ya wilaya.


Kapambala aliwataja wagombea wa UVCCM kuwa ni Faraji Idd, Angelo Madundoo na Jeni Likunde wakati Halmashauri kuu ni Siwega Hassani na Peter Mussa na mkutano mkuu ni Omari Jumanne, Gervas Simon na Samia Salumu.


Katika Wilaya mpya ya Mkalama ni Linza Linza na Msafiri Matilya nafasi ya uenyekiti wa wazazi wakati Halmashauri Kuu ni Tyatawelu Makuza, Juma Mandi na Salumu Rashidi huku UWT nafasi ya uenyekiti ni Elipendo Mchafuko, Mariamu Kahola na Magreth Kinota.


Wengine waliopendekezwa Halmashauri Kuu ni Habiba Kununta na Hadija Magolanga wakati mkutano mkuu ni Mariamu Kitala na Elipendo Machafuko kwa UVCC, Halmashauri Kuu waliopita ni Mohamed Jumanne na Hamoud Omar na mkutano mkuu wilaya ni Julius Adamu.


Kwa Singida vijijini waliopita nafasi ya uenyekiti ni Japheth Ghambilu, Alexander Mbogho na Yussuf Kwimba wakati Halmashauri Kuu ni Mussa Nkungu na Rashidi Mkuya.


UWT nafasi ya uenyekiti ni Hadija Kissuda, Salima Kundya na Neema Ifande wakati Halmashauri Kuu ni Elizabeth Sima huku mkutano mkuu ni Fatuma Hanti, Rozalia Kitiku na Mwajuma Mwiru.


Kwa UVCCM nafasi ya uenyekiti ni Elias Sidadi na Shabani Mang’olo wakati Halmashauri Kuu ni Elias Sidadi, Shabani Mang’olo na Hawa Ibrahimu, huku mkutano mkuu ni Kusiana Hanje, Mohamed Jawi na Rose Mahanja.


 
Mbona Silioni Jina la Mwengulu Nchemba? nitafurahi kama halipo... Ni Mbaguzi!!!
 
Huyo Maria Mkumbo hana uhusiano na mh.Lameck Mkumbo aka Mwigulu Lameck Mchemba(first class economist) wadau mwenye info atujuze tafadhari,ila mh.Lameck Mkumbo siku hizi amepotea yale makeke yake sijayasikia toka watu wafunue mafaili yake(registers za shule za msingi)
 
Sema toka asababishe kifo cha mpiga kura wake na ile ishu ya kujiandikia Sms kwa kutumia ule mtambo wao na kujua kuwa imefahamika na Marando&the team.
 
Back
Top Bottom