Walioongopea Kamati Watakiona - Dr. Mwakyembe

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
Wakati Wajumbe watatu wa Kamati ya Richmond, Stela Manyanya, Lucas Selelii na Mohamed Mnyaa, wako Marekani na tayari wameshapita DC ubalozi na leo wanaelekea Texas kuonana na kina Gire, kupeleka mashahidi wa uongo wakiwa chini ya kiapo, gazeti la Tanzania Daima ambalo halijawekwa katika internet limesema kwamba kuna mashahidi wametengenezewa ushahidi kabla ya kwenda ktk kamati na kwamba waliandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Nishati na Madini.

Sasa kamati imebidi iongezewe muda hadi Desemba 31....
 
Ni hiviiii, PMO waliandaa mashahidi, wakawapa semina na jinsi ya kwenda kusema katika kamati... huo upande mmoja... upande wa pili, Spika ameona kuna umuhimu wa kuwaita tena mashahidi ambao ushahidi wao chini ya kiapo umegongana na unaonekana unaweza kuwa wa uongo... Sasa Mwakyembe anasema wanaweza kuchukuliwa hatua, hata ikibidi kufungwa jela
 
Hawa watu wanadhani tuliwatania kuwa hii Kamati siyo ya Ushauri (LOL) hii kamati ni mahakama, na kama hamuamini ngoja muone watu wakipelekwa lupango ndipo watajua embe ni tunda!!
 
Wacha tusubiri kidogo tuone hiyo taarifa ya kamati ndio tuwezekujua nini kinachoendelea,but wanaoweza kufuatilia kwa karibu zaidi basi tunawaomba wafanye hivyo tusijetukadanganywa.
 
Mwanaakijiji, nitaamini nitakapoona vigogo husika wakipelekwa mahakamani na siyo vijidagaa tu.
 
Lakini jamani mie nadhani kuna umuhimu wa kufahamu nani wanaohujumu magazeti kama TZ Daima na Raia Mwema kila yanapokuwa na habari nzito.I was surprised kwamba kwanini hadi muda huu TZ Daima haliko mtandaoni.Ni hujuma ndani ya magazeti hayo au.....?Wataalam wa IT mnisaidie hapo
 
Yaani siamini, pamoja na yote tuliyozungumza huko nyuma bado tiktak zinaendelea? lakini ukweli utajulikana tu, hata wafiche namna gani. Lazima tuzae nao mwaka huu, tumechoka kuwa kichwa cha mwendawazimu!
Naamini Mwakyembe na Lucas Selelii watafanya kazi yao kama kawaida, nawaaminia sana!
 
Mfa maji haachi kutapa!

Yaani kwa PM bado wanaamini kumfundisha mtu kusema uongo ni rahisi tu?? subiri sasa ukweli ujitenge ndo watakapo jua kitunguu siyo mboga bali ni kiungo cha kupikia mboga!
 
Scooter Libby somebody right thurrr,

Ila tu wasitumie tactics kushift attention kutoka kwenye real deal kutupeleka kwenye perjury.
 
Habari hizi ni za uhakika, na Dr. Mwakyembe amewaambia hili "litakuwa fundisho kwa watumishi wote wa serikali ambao wanachukulia zoezi hili kimzaha mzaha".
 
Tusubiri kwanza, maanake hawakawii kutupiga changa la macho hawa. Bottom line Seleli na Mwakyembe ni"Wenzao" hivyo watawalinda unless wawe wameamua kukiacha chama cha wenyewe yaani sisiem.
 
Nafikiri this time kuna mtu ataumbuka tu. Kama PM angekuwa na uwezo wa kuwafuata akina Mwakyembe asingetumia strategy hii ya ki-primitive kiasi hiki. Nadhani Lowasa ameshindwa kuwaingia wanakamati. Itabidi ajiuzulu tu mwenyewe kuficha aibu. Ni mtendaji mzuri lakini rushwa inamfanya akose akili kabisa.
 
Muulize kama watakuwa na uhuru wa kushauri misamaha ya kodi iwe specific zaidi kwani kwa sasa ina mianya mingi ya rushwa au perception ya rushwa which is just as bad.
 
Nimefanya mahojiano na Dr. Mwakyembe muda mfupi uliopita na amejibu baadhi ya maswali ambayo watu wanayo.. MoD.. unaweza kuiunganisha hii na ile ya Halisi kuhusu "Breaking News - Kamati ya Richmond BALAA". Nitawawekea mahojiano hayo muda si mrefu ujao bila ya kuya edit, cut au mixing.. !
 
Mwanakijiji,

kama hukutaja vyeo vyote na kazi zote za Mwakyembe inabidi umpigie simu tena ili ufanye hivyo.

Just a reminder!
 
Hawa watu wanadhani tuliwatania kuwa hii Kamati siyo ya Ushauri (LOL) hii kamati ni mahakama, na kama hamuamini ngoja muone watu wakipelekwa lupango ndipo watajua embe ni tunda!!

It is about time, people understand the meaning of "Kula Kiapo."

Let's wait and see.
 
Back
Top Bottom