Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,988
- Thread starter
- #21
Yeye Nyerere aliruhusu wagombea wa aina gani?
wa vyama na binafsi! na akaheshimu matokeo yake.
Yeye Nyerere aliruhusu wagombea wa aina gani?
Mkuu kama ndivyo basi dawa ni kurekebisha mfumo mzima wa Upigani kura za maoni na sio kupachika kiraka nje ya tobo kama style ya nguo tukidai tunaziba pengo hilo.
Mimi sitazami wagombea Binafsi kwa kuitazama CCM au kwa nini CCM hawataki wagombea binafsi isipokuwa natazama utaratibu wa kisiasa (demokrasia) ktk kuwepo wagombea binafsi. Hawa wote wanaodai kuwa wagombea binafsi wanachukua nafasi hiyo kwa sababu wanajua hawawezi kupita ktk uchaguzi wa ndani CCM. Sasa kwa nini wanabakia CCM hali wanaweza kwenda vyama vingine wakapita uchaguzi ikiwa wananchi wanawakubali?..Au onyesha utofauti wako na CCM kiitikadi bila shaka tutakuwa nyuma yako kukubali kama alivyojitangaza Rev. Kishoka.
Kama unataka kugombea Ubunge au kiti chochote cha kisasa ni lazima uwe na mtazamo tofauti na mpinzani wako kiitikadi laa sivyo tunapelekea kuamini kwamba Ni mtu anayeweza kutuwakilisha na sio sera za mtu huyo. Yale yale ya kitumwa kuamini wazungu (watu weupe) ndio wanajua kuliko weusi pasipo hata kueleza tofauti ya uwezo wao. Tukumbuke tu kwamba siasa na itikadi ni Ubunifu wa mirengo ya kuboresha maisha ya jamii zetu, sasa ikiwa tuna watu 10 wenye itikadi sawa na tuwape nafasi za wagombea binafsi hali mchango wao hauna tofauti na ule wa mgombea wa CCM tunakuwa tunapoteza muda na fedha za wananchi.
Ni sawa na utaratibu wa Taxi kuchukua abiria, kama unalo gari na unataka kulifanya Taxi nenda kasajili ktk jumuiya ya wana taxi kisha fanya biashara zako lakini sio kuomba haki ya kila mwenye gari aruhusiwe kusanya anapopenda kwa sababu tu kuna matatizo ktk mfumo wa jumuiya ya wanaTaxi. Hutaki Taxi ingia kwenye Daladala hutaki pia jaribu kufikiria kuanzisha njia usafiri mwingine utakao pingana na jumuiya zilizopo na sio kuomba kibali cha kusanya.
Wonna be a Politiacian, be a Politician kwa kujiunga na chama unachokubali sera zao au pingana na itikadi za vyama vilivyopo.Leo hii tuna vyama zaidi ya 20 tena chini ya sheria kama hii tukiachia hapo unafikiria tutakuwa na wagombea wangapi?..
Uchaguzi wa CCM tu umetuonyesha jinsi gani watu walijitokeza kugombea hali nimegundua kwamba CCM yenyewe haina hata wananchama zaidi ya millioni moja kutokana na hesabu ya wapiga kura. Matokeo yote ya kura za maoni za CCM ni ishara nzuri kwetu kutonyesha jinsi watu tulivyokuwa walafi wa madaraka badala ya uwakilishi wa wananchi kupitia chama.
wa vyama na binafsi! na akaheshimu matokeo yake.
Aliikuta halafu akaharamishaAliruhusu halafu akaharamisha
Aliikuta halafu akaharamisha
Ubaya wake unakuja kwamba unataka kutunga sheria kwa sababu ya kile kinachotokea leo CCM/Chadema. Kumbuka Mgombea Binafsi ni sehemu ya Demokrasia sasa huwezi kuuweka utaratibu huu kwa sababu ya kufidia matukio kama haya ya watu kuhama CCM kuingia Chadema.Mkandara fikiria hivi, leo hii kuna watu wa Chadema wametemwa/watatemwa ili kupisha watu wengine. Watatemwa si kwa sababu walishinda vibaya au kwa rushwa bali kwa sababu watu wengine wanahitajika (kwa mfano Mpendazoe kupewa Segerea japo alishindwa). Yule aliyeenguliwa akiamini kuwa bado anakubalika na wananchi wengi (zaidi ya wanachama) anatakiwa aidha akubali tu au atafute mahali pengine pa kugombea. Sasa, matokeo yake ni kuwa mtu ANALAZIMISHWA kujiunga na chama kingine ili AGOMBEE.
Na hili tutaliona kuanzia J'pili hii, baada ya majina ya vigogo kuthibitishwa kutupwa na KK basi wataanza kukimbilia hasa Chadema (sources zangu zinanithibitishia kuwa kuna vigogo wameomba Chadema wasitangaze baadhi ya majimbo wagombea wake ili wasubiri kupata matokeo ya KK). Watu hawa kama ni waumini wazuri wa CCM wanabakia kujiuliza, je wasubiri miaka mitano mingine au waruke na waingie upinzani ili wagombee mwaka huu?
Kwa vile dirisha liko wazi kwa karibu siku nne tu (August 14-19) basi ni wazi kimbilio itakuwa ni kuwa wapinzani. Lakini si kwa sababu wanaamini au ni wapinzani kweli; la! bali ni kwa sababu ya nafasi (opportunity). Lakini kama kungekuwa na wagombea huru/binafsi wanachamah hao wanaoenguliwa wangeweza kusimama wenyewe (binafsi) bila KULAZIMISHWA kuhama vyama vyao. Na wakishinda bado wanabakia ni wanachama wa vyama vyao.
Kwanini hili ni baya?