Waliogawa Sanda Nachingwea ili Kudhibiti M4C Wafariki Dunia!

mtoa sanda Mathias mpewa sanda Fahida, mkiambiwa mnatumika mnapiga kelele, toka lini mkristo akampa mwislam zawadi ya sanda?
 
Kifo kwa mwanaadam ni jambo la kuhuzunisha, linahusika zaidi na mipango ya Mungu, sio la kufurahia wala kubeza.

Lakini kuna mazingira mengine ingawa inawezakuwa ni mere coincidence lakini kwa akili za kawaida za kibinaadam, mtiririko wake unaweza kumkosesha mtu raha.

Ikumbukwe kuwa wiki iliyopita, siku moja kabla M4C haijaingia Nachingwea, Mh Mbunge wa jimbo hilo Bw Chikawe alikuwa akigawa sanda kwenye misikiti ya Kata za jimbo lake kwa kutumia wasaidizi wake, Msimamizi mkuu wa shughuli hiyo alikuwa Ndg Fahida Mpoyo ambaye ni Diwani wa Kata ya Stesheni akisaidiana na Ndg Amani Rahisi maarufu "Bata".

Siku walipokamilisha shughuli hiyo ya kugawa sanda hizo jioni, usiku wake Chadema ikapata msiba mzito wa Muasisi wake Mzee Bob Makani, kwa hiyo Operation Sangara ikasitishwa, haikuingia Nachingwea kama ilivyopangwa, ingawa viongozi wachache walienda kuomba radhi kwa wananchi kwa dharura iliyotokea.

Cha kusikitisha wagawa sanda hao walijiona kama washindi fulani kutokana na kauli walizozitoa. Baada ya mazishi ya Mzee Makani J'5 iliyopita, juzi Ijumaa Mkuu wa kugawa sanda Mh Diwani Fahida Mpoyo, alifariki dunia, kwa hiyo Kata ya Stesheni, Wilaya ya Nachingwea iko wazi, cha kushangaza, (Mungu si Athumani) leo hii Ndg Amani Rahisi aka Bata, nae kafariki dunia, hivi tunavyoongea maiti yake bado iko kitandani ikisubiri kukamilishiwa faradhi zake.

Mtiririko huu wa misiba umezua Taharuki kubwa hasa kwa waliohusika na ugawaji wa sanda hizo, hasa muhusika mkuu aliezigharimia! Kwani kwa simple calculations za Law of Probability, unaweza ku determine anaefuatia anaweza kuwa ni nani. Tumuombe Mungu aepushe kusitokee maafa zaidi.

"WHAT GOES ROUND, COMES AROUND!"

Wahenga walipata kunena kuwa "Mwosha huoshwa"
 
Je mkuu unaweza kutudadavulia lengo la mgawa sanda nini kilimsukuma kufanya hivyo na waliokuwa wanagawiwa ni wafiwa kwa utaratibu upi je aliyetoa msaada kama ametumwa afanye hivyo tutajuaje mie hainingi akilini kushiriki kugawa sanda watanzania maswala ya kifo tunayaheshimu sana yanapoingizwa kwenye vyama na wanaotumiwa wasijiulize ni mahitaji ya wapiga kura tunajidhalilisha hao wanaopotea hawakuchanganya na za kuambiwa
 
Kama ni kweli, Mungu hadhihakiwi! Ukose kugawa misaada ya kuwasaidia walio hai, ugawe misaada kwa ajili ya wafu?
 
"Hakuna uchawi wala uganga utakaoinuka katika israel" hesabu 23:23

"kila silaha itakayoiunuka kinyume nawe haitafanikiwa"

hizo hapo ni ahadi za Mungu alizosema na kuhaidi kwetu maana neno lake ni kweli na amina na zaidi lina pumzi yake Mungu.
 
Mh Fahida siku ya Alhamisi iliyopita, alikuwa kwenye shughuli zake kama kawaida, jioni alirudi nyumbani, usiku alienda kulala lakini Ijumaa asubuhi akakutwa amefariki kifo cha kawaida. Ilipofika J'2, "Bata" aliyekuwa akisaidia ugawaji wa sanda hizo, mida ya mchana, alianza kulalamika kuwa anaona vitu asivyovielewa mbele ya macho yake, kama maruweruwe hivi, ndugu zake wakamchukua ili wafanye mipango ya kumpeleka kwa "wataalam" lakini cha kushangaza aliwatoroka ndugu zake hao, walianza kumtafuta, mida ya saa 10 jioni wakamkuta amejinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali yake.

duu nikweli jamani ?? Maana nilikuwa napita tuu .lakini nimeshindwa .imebidi nikae nihoji .cdm ina mkono wa Mungu vile !!
 
Anaefuatia ni yule alikuja na wazo la kugawa Sanda hizo ama Mfadhili wa Sanda hizo
 
Mböna hii ishu ni nzito ila mimi sijaisikia, hivi ni kweli? Kama ni kweli haya ni mambo ya aibu kubwa. Ila naömba Mungu awasamehe.
 
Back
Top Bottom