Walioambukizwa virusi vya Ukimwi wajitangaze’

mdau wetu

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
548
58
WATANZANIA wametakiwa kujenga utamaduni wa kujitangaza hadharani mara wanapopimwa na kubainika kuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Mwito huo umetolewa na kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu, Mtumwa Khalfan, wakati akitoa ujumbe wa mbio hizo mara baada ya Mwenge huo kuwasili Manyoni juzi na kuanza kwa siku mbili mkoani Singida.

Mtumwa alisema licha ya kubainika kuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi, baadhi ya watu wamekuwa wagumu kujitangaza na kusababisha wakose fursa na huduma mbalimbali.

Kutokana na hali hiyo, Mtumwa alisema ni vyema wanaoishi na virusi vya Ukimwi waache kujinyanyapaa badala yake wajitangaze hadharani juu ya hali ya afya zao.

Alisema kuwa hatua hiyo itasaidia watambulike vyema na jamii ya eneo husika na kuwa rahisi kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali na wadau wengine.

Mwenge wa Uhuru umemaliza mbio zake mkoani Singida jana na utakabidhiwa kwa uongozi wa Mkoa wa Tabora leo.

Ujumbe wa mbio za Mwenge mwaka huu ni Miaka 50 ya Uhuru chini ya kauli mbiu ya Tumethubutu, Tumeweza na Tunazidi Kusonga mbele.
 
Back
Top Bottom