Kwa maoni yangu, wahusika wakuu katika kuchochea mgomo wa madaktari nchini ni wanasiasa (WABUNGE). Nasema ni wabunge kutokana na urafi na ubinafsi wao unaotokana na kujiongezea mishahara na posho kila mara huku watumishi wa umma ambao ndio wanafanya kazi kubwa katika ujenzi wa taifa wakiambulia mishahara kiduchu na mazingira magumu ya kazi. Nasema hawa waishiwa ndo chanzo kikuu cha mgomo huu kwa sababu, hebu angalia, mgomo wa mwezi wa pili mwaka huu ulikua baada ya taarifa kuvuja kuwa waishiwa hawa wamejiongezea posho na mshahara. Angalia mgomo unaoedelea sasa nao ukiangalia umekua baada ya taarifa kuvuja kuwa waishiwa mjengoni wamejiongezea tena mshahara kwa kazi ya kusinzia na kuzomea wanaopinga uozo kwa hoja. nawasilisha.