Walimu wawasha moto mpya,Wataka mishahara ya 900,000/-

correct me if am wrong......i think the time for a revolution to happen is near......anyway walimu mtaweza au mtafyata mkia?wenzenu tumetishiwa hadi kufukuzwa kazi lakini msimamo upo palepale
 
Waalimu kufanikiwa kwenu badilisheni hao viongozi wenu
muwe na msimamo kama madokitas. La sivyo itakuwa
historia yenu hiyo hiyo ya kila siku.
 
after all, wanaotakiwa kuboresha sehemu ya kazi ni kanisa through MoU public funds hawakufanya hivyo wamekula pesa...kama kawaida makanisa kwa ufisadi..

Naona vyombo vya habari hawataki kuandika kuhusu cssc (christian social services commision) walivyoshindwa kuboresha mazingara ya kazi KCMC, na Bugando wameanza kuisingizia serikali..lol

Muhimbili, Rufaa Mbeya zinaendeshwa na kanisa lipi?
 
Natamani uitishwe mgomo mkubwa zaidi wa wanataaluma wote kutoka sekta zote kupinga serikali kugharamia siasa zaidi ya maradufu ya jinsi inavyogharamia taaluma!Huu ni wakati wa TUCTA kuunganisha wafanyakazi wote na kudai mabadiliko.Ni wakati wa kuionya serikali kuwa taaluma ni bora kuliko siasa.
 
hawana issue...kazi yao huwa ni kutishia wakubwa nyau.
december 2011 walitangaza kugoma na kwamba wasingeingia madarasani come Jan 2012 mwisho wakaahirisha kwa kuonjeshwa pipi.

in my opinion, wabadilishe uongozi kwanza...huyo rais wao Gratian Mukoba is bloody useless.
 
Hivi kwa nini mipolisi haigomi? Na inalipwa kiduchu sana eti kulinda Bank posho Tsh.5000/= anang'atwa na mbu usiku kucha anaambulia buku 5 gomeni na nyie wekeni chini mabunduki na mabomu ya machozi piganieni haki zenu ili nanyi mfaidi keki ya Taifa inayo liwa na wachache katika nchi hii.
 
Huyu kiongozi wa nchi nahisi yuko mbioni kukimbia nchi kama mambo yenyewe ndio haya!
 
Maisha magumu kwa kila mtanzania.wahadhiri vipi na nyie hamgomi?maana mziki wa wanafunzi wahadhiri wakigoma pale magogoni patachimbika

Kama ni noma na iwe noma. Tutagoma hadi kieleweke, tatizo ni kwamba tunakosa uvumilivu kwa vile tunajua fedha serikalini zipo ila zinatuliwa na wajanja wachache kujinufaisha at the expense of the majority who are very very poor. The solution is to force for our rights.
 
maisha magumu kwa kila mtanzania.wahadhiri vipi na nyie hamgomi?maana mziki wa wanafunzi wahadhiri wakigoma pale magogoni patachimbika

we c umejiita mhadhiri kwenye post moja leo, ukasema hutaingia kutoa lecture? Unamwuliza nani sasa wahadhiri kugoma, wakati wewe mmojawao? Kwa udsm ungetupa udasa wanasemaje, sema hujatwambia unalecture wapi
 
Mh sasa hao madai yao mpaka mwezi wa 7 huko...kwanini wasiingie tu mtaani in this moment wakatoa support kwa madaktari??
 
Hivi kwa nini mipolisi haigomi? Na inalipwa kiduchu sana eti kulinda Bank posho Tsh.5000/= anang'atwa na mbu usiku kucha anaambulia buku 5 gomeni na nyie wekeni chini mabunduki na mabomu ya machozi piganieni haki zenu ili nanyi mfaidi keki ya Taifa inayo liwa na wachache katika nchi hii.

Wagome vipi wakati wanavyanzo vingine vya mapato!Wenzako uniform tu zile tayari ana uhakika wa 50,000 kwa siku!!Hakuna wezi wadogowadogo kama polisi ndugu yangu!!Yupo koplo huku anajenga hekalu uswahilini kwetu!!
 
walimu nao muhimu wagome tu hii itaonesha jinsi serikali isivyoshughurikia mambo
wazee wa east afrika nanyi pia gomeni wote wagome tu sio mbaya tutapata sababu ya kuitoa serikali hii madarakani maana imeshindwa
 
Back
Top Bottom