Walimu watangaza mgomo nchi nzima

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,314
33,108

Thursday, 01 December 2011 20:42
mukoba-gratian-top.jpg Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana , kuhusu mgomo wa walimu nchi nzima utakaoanza mwezi Januari kama Serikali haitatimiza makubaliano yaliyofikiwa ya kuwalipa madai yao. Picha na Venance Nestory

Raymond Kaminyoge
CHAMA Cha Walimu Tanzania (CWT), kimetangaza mgomo wa walimu nchi nzima kuanzia Januari mwakani ikiwa ni hatua ya kuishinikiza Serikali iwalipe walimu deni la malimbikizo ya stahili zao mbalimbali, linalofikia Sh49.6 bilioni.

Hatua hiyo imekuja baada ya Serikali kushindwa kutimiza ahadi yake ya kuanza kuwalipa walimu fedha hizo tangu Novemba mwaka huu. Rais wa CWT, Gratian Mukoba alisema jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na wandishi wa habari kuwa Serikali iliahidi kuwalipa walimu Novemba hadi Desemba mwaka huu ili kumaliza deni hilo.

“Natangaza kuwa shule zitakapofunguliwa mwezi Januari 2012, sisi walimu tutaendelea kuwa likizo mpaka kero zetu zitakapotatuliwa,” alisema Mukoba. Alisema tangu Juni mwaka huu, CWT na Serikali wamekuwa na vikao kadhaa kuhusu madai hayo na ikafikia uamuzi wa kuwalipa walimu katika kipindi cha miezi miwili ambayo ni Novemba na Desemba mwaka huu.

“Kumbe Serikali haikuwa na nia ya kweli kutaka kutulipa, waliona tunaweza kugoma katika kipindi cha mitihani ya taifa wakatudanganya,” alisema. Alisema kwa kuwa Serikali haina nia ya dhati katika kulipa madai hayo, wameamua kufikia uamuzi wa kutoendelea kufundisha.

Mukoba alisema wakati mishahara na posho za wabunge zikizidi kuongezeka, walimu wanashindwa kulipwa madai yao ya msingi. “Tunawaomba wazazi watuunge mkono katika mgomo huu ili watoto wenu wapate elimu sahihi,” alisema Mukoba. Kwa mujibu wa Mukoba, madai hayo yanayowahusu zaidi ya walimu 3,000 ni ya kuanzia mwaka 2008.

Alisema kero nyingine inayowafanya walimu wagome ni waraka kandamizi uliotolewa na Serikali mwaka 2007 unaowashusha vyeo walimu wanaojiendeleza kielimu. “Serikali ilikubali kuufuta waraka huo baada ya kuridhika kwamba ulikuwa unawakandamiza walimu, lakini hadi sasa unaendelea kutumika, haujafutwa,” alisema. Mukoba alisema waraka huo umelenga kuwakatisha tamaa walimu ili wasijiendeleze kielimu.

Aidha, Mukoba alisema walimu wanakaa kwa muda mrefu bila kupandishwa vyeo ingawa wanastahili kulingana na sifa zao. “Walimu tumekosa nini, kwa nini kilio chetu hakisikiki na Serikali? Iweje tunadanganywa kila siku? Sasa ni lazima tuchukue hatua,” alisema Mukoba. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawamba hakupatikana jana kuzungumzia tishio hilo la mgomo baada ya simu yake ya mkononi kutopatikana kabisa.

chanzo: Walimu watangaza mgomo nchi nzima
 
Hagomi m2,hawa watu hawana umoja na wamekosa msimamo mara ngapi wamesema wanagoma na hawajagoma
 
baada ya CDM kuchemka pamoja na wazee wa katiba sasa kaka miyeyusho mwenyekiti mukoba anaendeleza popularity haya tuone cinema hiyo nyingine :lol:
 
Jamani tusiwabeze walimu tuwaunge mkono maana wananyanyaswa sana!
 
Safari hii magwanda hawataki mgomo, sijui nani atawa"support".
hawa waalimu hutumika kipindi cha kampeni tu after that wanakuwa left-overs -- wasubiri uchaguzi mdogo wa madiwani kule arusha wapate perdiem za kuhesabu kura za CCM.
 
Safari hii magwanda hawataki mgomo, sijui nani atawa"support".

Mimi hapa ndo huwa nakukubali!

Walimu wanalilia stahili zao, habari za magwanda zinahusika nini hapo. Kwanini kuwakejeli walimu hawa, wamekukosea nini???!!!
So, wewe unaunga mkono wabunge kuongezewa posho badala ya serikali kulipa kwanza wadai wake kama vile wastaafu wa EAC, walimu, na wafanyakazi wengine wanaoidai serikali? Kwa kweli umebarikiwa busara za hali ya juu. Safi sana.

Siungi mkono mgomo, ila naunga mkono wapatiwe stahili yao.
 
Waalimu hata wachinjwe kugoma ni mwiko kwanza wengi wao hawajielewi na wala hawajui haki yao..... hawana umoja hata siku moja
 
Jamani walimu wenzangu mbona mwanichekesha?mwenzenu mgomo nilianza toka 2008 mpaka madai yangu yatakapo tatuliwa,sasa wenzangu mnasubiri tena hadi 2012.Kumbuka mgomo sio kwenda barabarani tu goma kisaikolojia,kama una vipindi 50 kwa wiki fundisha 5 tu kisha nenda kaongeze kipato sehemu nyingine.
 
Safari hii magwanda hawataki mgomo, sijui nani atawa"support".


Hata kulipa walimu nako mmeshindwa? Mmebaki magwanda magwanda mbona mtajibeba na roho zenu mbaya kudhulumu watanzania. Pesa mmeishiwa na sasa ukameruni lazima mtaukubali tu. Mmeshindwa hata kulipa watumishi mishahara? Ney Bollo Kwishney
 
Ni haki yenu kupata mafao yenu lakini HAMWEZI KUGOMA kwa sababu hamna ujasiri! Wanasiasa wanawajua kuwa wengi wenu ni waoga, hamjitambui ingawa mnafundisha wanafunzi kujitambua, hamjui haki zenu, mna vyeti bandia kwa hiyo ajira yenu ni kama upendeleo na hamna ujanja mwingine wa kuishi ndiyo maana hata darasa la saba na MEMKWA wa serikali na bunge wana uwezo wa kuwashika masikio na kuwachezea wapendavyo. Leo hii mwalimu wa digree anazidiwa masurufu na afande wa anayejua kusoma na kuandika tu, ambaye hajui shule alisoma wapi! Si utani huo? Nini maana ya kusoma kama ambao hawakusoma wenye kufanya kazi katika sekta nyingine za umma au za serikali wanapeta huku nyie mkifa na vumbi la chaki, madeni na maisha mabovu? Ndiyo maana mtawala mmoja wa UDOM aliwahi kuwatukana "instructors" wake kuwa wanchomzidi ni "UMASKINI na UREFU wa kimo!" Jifunzeni kwa wenzenu vinginevyo watoto wenu watakuja wawe makuli.
 
Tatizo walimu ni waoga, wakitishiwa kidogo tu hunywea kama vile kobe anavyorudisha kichwa ndani akistuliwa. Mkoba wenzako unaowatetea wanakusaliti na hawana confidence!
 
Hawa jamaa huwa wananiacha hoi kama mbwa koko mikwara mingiiiiiiiii mwisho wa siku wanaingia darasani kushika chaki
 
Hawa wajinga hawa, huwezi tangaza mgomo baada ya mwezi mmoja, mgomo ni wa siku hiyo hiyo, au kesho!
 
Back
Top Bottom