Walimu Watakapoanzisha Kampeni Rasmi Madarasani Kuing'oa CCM

Sijui na huko kwenye MAKAMBI ya JKT je hizi sumu hazijafika? Na huko kuna BUNDUKI na MABOMU sijui itakuaje? Lile somo la siasa watafundisha za vyama vyote au litaachwa? TAFAKARI

Hali ni mbaya zaidi kule,kuna wakufunzi wataalam wa kutoa sumu juu ya serikali vibaya. Nimepiga hiyo kozi ya nikiwa kikosi cha 835Kj,yatosha kumuomba Allah kwa 2015
 
Nimekuwa mwana CCM maisha yangu yote. Nimeipigia serikali ya CCM kura siku zote, lakini baada ya hii patashika, inanibidi nijitafakari.

Baada ya kufika nyumbani mithili ya saa mbili usiku jana 16/07/2013, mwanangu anayesoma darasa 5 hapa jijini Dar, alikuwa na shauku kubwa sana ya kuongea na mimi. Kitu ambacho hakikuwa kawaida yake. Baada ya kuvua nguo za kazi, aliniita sebuleni na kuniuliza, baba huko tayari kuongea na mimi? Nikamuuliza kuna nini, alinijibu namaongezi na wewe. Kwa wasiwasi wasi mkubwa nilitii ombi la binti huyu.
Mwanangu aliniuliza maswali mengi yaliyonitoa machozi. Maswali yake yalikuwa kama yafuatayo

  1. Baba, kwanini hatupati chakula cha kutosha?
  2. Kwa nini hauna gari wakati unaowapigia kura wana magari ya kifahari?
  3. Kwa nini kaka Issa alifeli form four na sasa hana kazi, wakati watoto wa mafisadi waliofeli wanafanya kazi benki kuu?
  4. Kwa nini hospitalini lazima uonge ndio tutibiwe?
  5. Kwa nini unapewa fulana na sahani ya pilau kisha kuuza kura yako?
  6. Tanzania haijawahi kuwa na udini, iweje leo tugawanywe kwa udini?
  7. Baba, duka lililokuwa la mama kariakoo amepewa mchina, je wachina watachua hadi nyumba tunayokaa?
  8. Kwa nini serikali haitaki kuwalipa walimu wetu vizuri?
  9. Kwa nini polisi wanawaua raia badala ya kuwalinda?
  10. Baba serikali ya CCM imekusaidia nini?
  11. Kwa nini hauwazomei mafisadi?
  12. Wamefundishwa kwamba CCM ni Chama Cha Magaidi wakiongozwa na Mwigulu Nchemba
Huku akiwa na daftari lake na kalamu mkononi, akiyasubiria majibu yangu? Nilishikwa na ghanzi. Nilishindwa kumjibu. Nilimuuliza kwa upole, haya mambo umejifunza wapi?

Bila woga alinijibu, kwamba wamefundishwa shuleni jinsi ya kulikomboa Tanzania kutoka mikononi mwa mafisadi. Wamefundishwa kuwazomea mafisadi wanaopita mabarabarani na kesho lazima warudi na majibu shuleni
Mkuu, isije ikawa wewe ndo unafundisha haya masomo wana jf? Tupe majibu basi uliyompa mtoto ili tukiamini.
 
Hilo mbona dogo? Walimu wawafundishe kuipopoa kwa mawe misafara yao inayotumia magari lukuki, mafuta mengi kwa kodi zetu, huku wanafunzi wakikalia mawe badala ya madawati na watoto wa vigogo kusomeshwa shule za "academic" huku wao wakiambulia zile za "St. Kayumba".

Swali lingine: Baba, mbona wewe ukiugua unaenda kutibiwa kwenye Kituo cha Afya, lakini akiugua kiongozi wa Serikali anapelekwa India au Uingereza?
 
Niliwahi kuhudhuria mafunzo ya kikazi kwenye Chuo kimoja huko Nyanda za juu kusini, ambapo mafunzo hayo yalikuwa yanatolewa na wakufunzi wachuo hicho. Wakufunzi hawa kila anayeingia, anafundisha na baadae kuna sehemu ya story kama kawaida. Wanayoongea,kuponda na kulalamika juu ya serkali, binafsi yalikuwa mpaka yananifanya nisipende story zile kwa machungu. Sasa nikawa najiuliza hawa kama haya wanayaongea hata kwa wanafunzi wao madarasani, nini hatima ya ya taifa hili.
Nyasirori,

Kwa kuwa SISI ndio tulioiweka Serikali madarakani, kisha Serikali hiyo imeamua kutusaliti, kuvunja Katiba na kufungamana na mafisadi, tuna kila hali ya kuichukia na ikiwezekana, kuiondoa madarakani.

Unasahau harakati za ukombozi wetu wakati wa Mwl. Nyerere kuudai uhuru kutoka kwa wakoloni? Walimu ndio daima chanzo cha harakati za ukombozi; wamedharauliwa kiasi cha kutosha na wana haki zote za kuwafundisha watoto kuwazomea viongozi na kuichukia CCM, na hilo ni DOGO kuliko mengi ambayo wangeweza kuyafanya. Ni awamu ya kwanza tu. Safari imeanza. Tunaweza tusifanikiwe kuichukua nchi 2015, lakini 2025 haiko mbali pia. Mungu yupo na daima husimamia upande wa haki!
 
Last edited by a moderator:
hongera walimu

Mie natoa hongera zangu ziwaendee walimu wa Kenya bana, wakisema Nooo ni Noooooo! leo serikali imefunga shule zote kwani waliwadanganya kuongeza mshahara wao wakati wa kampeni na mpaka leo hakuna kitu...hao ndio walimu si watanzania wanaotishia nyau na akina mkoba wao
 
badala ya kulaumu chadema kwa hili, tungejitafakari vizuri, tukisharekebisha haya, chadema wasingekuwa na sauti. CHADEMA wanapata wafuasi wengi kwa vile serikali iliyoko madarakani imeshindwa kukidhi matarajio ya wananchi wengi.

boresha kidogo hapo kwenye red pasomeke: imechoka
 
Tunasubiri daftari la kujiandikisha,hii kitu ipo toka siku nyingi.Lkn ccm walivyolewa hawashtuki milele
 
Tunasubiri daftari la kujiandikisha,hii kitu ipo toka siku nyingi.Lkn ccm walivyolewa hawashtuki milele

Moja ya watu wanaongoja uboreshaji wa daftari la wapiga kura kwa hamu kubwa ni mimi hapa! elimu ya uraia niliyoitoa kwa miaka hii nangoja kwa hamu nipate mrejesho kwa vijana wangu, naamini wameiva hasa!
 
Niliwahi kuhudhuria mafunzo ya kikazi kwenye Chuo kimoja huko Nyanda za juu kusini, ambapo mafunzo hayo yalikuwa yanatolewa na wakufunzi wachuo hicho. Wakufunzi hawa kila anayeingia, anafundisha na baadae kuna sehemu ya story kama kawaida. Wanayoongea,kuponda na kulalamika juu ya serkali, binafsi yalikuwa mpaka yananifanya nisipende story zile kwa machungu. Sasa nikawa najiuliza hawa kama haya wanayaongea hata kwa wanafunzi wao madarasani, nini hatima ya ya taifa hili.
.HATIMA YAKE NI LAZIMA NCHI HII IRUDI WALIONYONGWA. HUWEZI KUWA MGOMBEA CCM BILA KUHONGA MSURURU WA WALA RUSHWA WAKONGWE NDANI YA CCM. MASKINI HANA UBAVU WAKUPIGIWA KURA ATAAMBIWA KAFIE MBALA ---- WEWE. CCM HAINA NAFASI NA WENYE FIKRA ZA KUMKOMBOA MTZ. DAIMA KWAKE NI MWIKO. ILI UVAANAE NA CCM NI LAZIMA UWE MNAFIKI UWE NA UWEZO WA KUWAPELEKA VIONGOZI KUWACHANJA KWA WAGANGA KIENYEJI KUNGARISHA nyota zao. ndo maana maprofesa kama wa deep water wamaeingia na kupata ubunge. ni lazima uwqe na hela ndo maana moja wa makambako kaupata kwa hela zake kwa uchache tu ni lazime uwe fisadi. ni lazima uwe na uwezo wa kutetea mafisadi pamoja na wakwapuaji wa maliasili toka nje
 
Hii ndio child abuse, mtt mdogo kama huyo kumuingiza

kwenye siasa na kumtia chuki ni ni kitu kibaya sana kwa

maisha yake, nashangaa hapa watu wazima wanafurahia

cc zomba
 
Huyo mtoto ni wa ajabu. Kwanini hakukuuliza maswali yafuatayo:

(i) Baba kwani una nyumba ndogo ambako unapeleka mahitaji yetu na kutunyong'onyesha?
(ii)Baba kwani wewe unanenepa na sisi tunakonda.Mtoto wa jirani ameniambia kuwa wewe kazini huwa unanunua nyama na kula wali wakati sisi tunakula maharage?
(iii) Baba kwanini wewe unachelewa kurudi nyumbani karibu kila siku?
(iv) Baba kwanini wewe unakunywaa bia huko baa na wenzako wakati sisi hata fedha ya soda hatuna?
(v) Baba kwanini wewe hujisomei nas umeridhika na masha na wala hujihangaishi kwa kufanya kazi kwa bdii?
 
Wee ndugu yangu unatuandikia thread ya mbulula wako,haya mnunulie kadi ya cdm Majungu yako ya kisiasa unampandikiza mtoto '"NAJILAUMU SANA KUCHANGIA FICTION KWENYE JAMVI LA HESHMA KAMA HILI" uktaka kujua nimechukiaje,nijibu uone..


Unanifurahisha kwa maneno yako. Shida ni kuambiwa ukweli? Mnakuwa wapenzi wa CCM hata ukweli mnajifanya ni Hadithi? Kwa nini msifanyie kazi mapungufu mnayoambiwa na wananchi? Kwa utaratibu huu uchaguzi ujao mjue hamna chenu.
 
na bado maana miongoni mwa sehemu nzur za kuzitumia kuhutubia jumuiya ya watu wengi wanakuja na kwenda kupiga kura ni kwa wanafunz mana unafanya ni sehemu ya somo haihitaji kibali cha polisi baada ya miaka mitatu kazi inakuwa imeisha mana kila mwaka wanaohitimu kwa kufuzwa ukwel wa mafisadi ni weng san
 
Back
Top Bottom