Albert Msando
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 1,019
- 171
Walimu wapya leo hii wameandamana hadi ofisi za Manispaa Arusha kudai malipo yao. Taarifa zilizopo ni kwamba malipo hayo yamechelewa kulipwa kwa sababu Serikali kuu haina fedha hivyo ikaiomba Halmashauri ya Manispaa Arusha iwalipe. Kutokana na Halmashauri ya Manispaa kutokuwa na fedha ikaamua kuwalipa nusu ya malipo yao jambo ambalo walimu hao wamelipinga.
Huu ni uzembe na unyanyasaji. Hizi kelele za serikali kukuza elimu ni siasa. Huwezi ukawa na matokeo mabaya ya mitihani halafu bado unaendelea kunyanyasa walimu!
Malipo ya Dowans ni haki kulipwa haraka lakini ya walimu masikini ambao wanajitolea jasho na damu kufundisha watoto masikini wa kitanzania hawana haki ya kulipwa mapema!
Wanakula nini? Wanalala wapi walimu hawa? Wanafikaje kwenye vituo vyao vya kazi?
Haya sio mambo ya kuvumiliwa hata kidogo. Walimu wasiachwe pekee yao kama yatima! Wanaharakati wawasimamie haki zao, vyama vya siasa viwapiganie!