Walimu Wanaokwenda Kusoma Bila Ruhusa Ajira Mashakani

Na walimu wenye degree nao tuchomoke tukapate masters. Ila mziki wa masters si sawa nawa degree. Lazima tuchomoke walimu na kuweka vitega uchumi vya maisha yetu.
 
Mwl ukifuata utaratibu unapata ruhusa.inatakiwa kuandika barua mwez wa 2 il wakuweke kwenye bajet.ikifika muda wa ruhusa
 
Ikifika muda wa ruhusa unaomba unapewa bila shida.mm mwenyewe nimepata ruhusa ya shule 2012 nimeajiliwa sept 2009
 
Hata hivo unachosema ndicho nifanyacho,yaan nafundisha vipindi kwa mujibu wa wizara bila kujali kuwa wengine wanakosa kwa sababu ya uhaba wa walimu.
 
UOGA wako ndio umasikini wako,mpaka ufundishe mipindi mingi namna hiyo kwa hela gani unayolipwa kaka/dada?achana nao badala yake fundisha vipindi vinavyoendana na ajira yako kisha Fikiria kufanya shughuli nyingine zitakazo kuongezea kipato badala ya kulilia kwenda kusoma ndugu yangu elimu uliyonayo inakutosha sana,fikiria distance learning na kukomaa kuitafuta shilingi zaidi kwani hata ukisoma bado mizenguo kibao kwenye kada hiyo,ni maoni yangu kwako tu.

Kiukweli hicho ndicho ambacho nikifanyacho kwa sasa,ninafundisha vipindi kwa mujibu wa wizara bila kujali kwamba wanafunzi wengine hawapati kwani idadi ya walimu ni ndogo sana
 
Walimu mnaokwenda kujiendeleza katika vyuo vikuu na vyuo vingine mnapaswa kuomba ruhusa katika mamlaka husika. Bila kufanya hivyo, mtahesabiwa kama watoro kazini na hivyo kuiweka ajira yenu rehani. Naibu waziri wa Elimu Mh. Phillipo Mulugo atahakikisha kwamba utaratibu huo unazingatiwa.

Kwa uzoefu nilionao ni kwamba hata wale wanaoomba ruhusa wengine huwa wanatiliwa ngumu na wakubwa wao kuanzia kwa wakuu wa shule, maafisa elimu, wakurugenzi nk. Unaweza ukaambiwa shule ina mwalimu mmoja tu wa somo fulani sasa ukiondoka nani atafundisha au wewe hauko kwenye mpango mwaka huu na sababu nyinginezo.

Sasa ndugu zangu uamuzi ni wako: uende kusoma ajira ikome na ukihitimu uanze upya au ubaki shuleni usiende kusoma.

hayo nimaelazo ya mzigo na tusha utua, ikumbukwe kujiendeleza ni haki ya kilamtumishi ilikuinua kiwango cha utendaji kazini, hao waliopewa dhamana ya kutoa vibali wanatoa kwa upendeleo na rushwa, ipo siku tutachoka na serikari hii dharimu.
 
kweli best mi nina miaka 5 kazn lakin ni miongon mwa watu ambao mpaka sasa hakielewek kitu kuhusu ruhusa napigwa karenda tu chuo kinafungua trh 1 nilichopanga kufika trh 7 bado nafanya maamuz magum boom nimepata et wananizingua sasa liwalo na liwe!
kama umepata mkopo nenda kasome ukimaliza utapata ajira tu na sio lazima urudi serikalin ,hzo pension mnazojidanganya nazo hata private school zipo...au unasubr had serikal iwarudishe kufundisha primary
 
Back
Top Bottom