Walimu wagoma na kuandamana Mwanza

nyangasese

Senior Member
Aug 21, 2011
129
22
Leo mnamo majira ya mchana mamia ya walimu katika jiji la mwanza wameamua kugoma kufundisha na hatimaye kuandamana kuelekea katika ofisi za halmashauri ya jiji kudai haki zao ikiwa pamoja na kutorekebishiwa mishahara yao tangu 2009 pamoja na madai mengine ambayo waliahidiwa kulipwa mwezi uliopita.kwa taarifa zaidi fuatilia taarifa ya habari star tv usiku huu
 
tafahamika tu..wao si wanadhani nchi inaongozwa kwa vitisho sasa wangoje waone ....kuna siku nchi itasimama hii....halfu tuone hao wanaowaita vyombo vya dola watafanya nini ..unajua calculation zingine ni rahisi sana ..kama hivo vyombo vya dola vinawatii mbona kawe kwenye kambi 4 za jeshi na makazi/kambi kubwa kabisa ya polisi JK na CCM yako mlizidiwa mkashindwa hata kuiba kura maana difference ilikuwa kubwa sana..sasa hiyo ni indication kuwa hata hao mnaowaita dola hawawapendi wanavizia siku tu wawatwange ngumi ya kisogoni.....
 
Mwanzo mzuri...Misri,Tunisia na Libya ilianza kama mchicha ikaja kuwa mbuyu....watawala wetu waache kujifanya viziwi na wasiojali...wanatuharibia nchi jamani.
 
wagome kabisa kada zote.......haya makundi mawili yakigoma kwa dhati kabida (madaktari na wali) jk lazima ang'oke
 
Mwanzo mzuri...Misri,Tunisia na Libya ilianza kama mchicha ikaja kuwa mbuyu....watawala wetu waache kujifanya viziwi na wasiojali...wanatuharibia nchi jamani.

This current government has demise written all over its disgusting face.
 
Hii ilingojewa sana.
Pinda leo tukungoje tena TBC? Utasoma profile ya nani leo?
 
Hivi kero kubwa ya mwalimu wa Tanzania ni madeni anayoidai serikali?Hivi mwalimu ukilipwa hayo madeni utakuwa na ridhiko la kazi yako?Mshahara wenu unawatosha?Mna mazingira mazuri ya kazi?Mnathaminiwa na serikali?Mnafurahia nyaraka kandamizi za serikali dhidi ya maslahi yenu?Mnakubaliana na CWT inavyowadhulumu huku yenyewe ikibaki kuwa chama cha madeni ya walimu?Waigeni wenzenu madaktari.Anzisheni mgomo ambao unamadai ambayo yanamgusa kila mwalimu.Sio kila siku madeni yenu tu,tumechoka!
 
Mh, nchi hii italipuka muda si mrefu!!
Maamuzi yenyewe ya hawa watu vichwa vya nazi?

Sioni atakae okoa jahazi hili, nani? nani? hakuna mwenye upeo wa kuingoza tanzania kwa sasa kutoka CCM!
 
Amakweli mpaka walimu nao wameanza kugoma baada ya kuona wakina MGAYA wamenunuliwa wapo kimyaaaaaaaaaaaa.....TUCTA na CWT hivi hamuoni wafanyakazi wenu wanashida achilia mbali posho na mishahara kuongezwa hilo mlishindwa lakini ata malimbikizi yao tena tokea 2009 nyie mpo kimya so mnawasubiri waandamane then ndo mjitokeze kuwasemea......
 
Hivi kero kubwa ya mwalimu wa Tanzania ni madeni anayoidai serikali?Hivi mwalimu ukilipwa hayo madeni utakuwa na ridhiko la kazi yako?Mshahara wenu unawatosha?Mna mazingira mazuri ya kazi?Mnathaminiwa na serikali?Mnafurahia nyaraka kandamizi za serikali dhidi ya maslahi yenu?Mnakubaliana na CWT inavyowadhulumu huku yenyewe ikibaki kuwa chama cha madeni ya walimu?Waigeni wenzenu madaktari.Anzisheni mgomo ambao unamadai ambayo yanamgusa kila mwalimu.Sio kila siku madeni yenu tu,tumechoka!

Ninawashangaa sana hii serikali ya kidhalimu, wanafiki wakubwa, Kama mtu hana taaluma yeyote na anatolewa tanzania kwenda kufajia ofisi ubalozini na analipwa zaidi ya 1,800,000 kwa mwezi, na bado hapo kuna wapishi wa balozi, bado mfanyakazi nyumbani huyu ni mtu mmoja anaitumia hela ya watanzania, kama wanahela nyingi namna hiyo kwa nini washindwe kuwalipa madaktari na walimu hela ya kutosha.

Ninasema tena hii CCM itatutesa sana na itatudhalilisha sana na tutahangaika mpaka tutachoka lakini mchawi wetu ni huyo CCM Kitendo cha kuuwa vile viwanda vyetu nitalilaani na ninaomba ikiwezekana tuungane wote kila mkoa tudai virudi. Uchumi hauwezi kukuwa kama hakuna viwanda, hela zote za watanzania zinaishia dubai, japani, Kenya badala ya kuzunguka hapa nchini. Yule mhindi aliye kwenda kungoa ngoa viwanda vyote kule moshi mtumeni tena akangoe na ile mikahawa tunamsubiri.
 
Leo mnamo majira ya mchana mamia ya walimu katika jiji la mwanza wameamua kugoma kufundisha na hatimaye kuandamana kuelekea katika ofisi za halmashauri ya jiji kudai haki zao ikiwa pamoja na kutorekebishiwa mishahara yao tangu 2009 pamoja na madai mengine ambayo waliahidiwa kulipwa mwezi uliopita.kwa taarifa zaidi fuatilia taarifa ya habari star tv usiku huu
What?Mwanza ,ok nilikuwa nje ya jiji mapema saaaaana asubuhi,now on may back to rock city nitawajuza
 
Back
Top Bottom