mtendaji wa kijiji
JF-Expert Member
- Jul 3, 2012
- 533
- 114
hebu wasitishie na wafanye ukweli\, wakiogopa vitishio vya serikale kamwe hawatafanikiwa
Huku chama cha walimu kikiwa bado kimya kuhusiana na mgomo wa walimu.Walimu mkoani Dodoma wameanza mgomo huo kimya kimya katika shule mbalimbali za mkoa huu.Nikiongea na baadhi ya walimu ambao hawakutaka majina yao kutajwa hadharani wamesema hawatasubiri tamko la CWT kwani wao ndio wanaoathirika kwa kiasi kikubwa.Wametoa wito kwa walimu nchini kote kupigania haki zao wenyewe na wameomba kuungwa mkono katika swala hili na pia wamewaomba walimu kuacha woga kwani woga ndio yatakuwa mateso yao.
wakaze buti sana manake hawakawii kusalitiana sababu kunawanao jikomba komba huko juu.
mwaka 1993 wakati ule nilikuwa darasa la tatu waliweza wakiongozwa na mheshimiwa magreth sitta, na kati ya mafanikio yao ni kukataa kuwa ualimu ni wito... that time my dad alikuwa mmoja wa viongozi waliandaa yale maandamano pale tambaza na azania... juzi nikamuuliza this time mtaweza? alichoniambia '' nyie madaktari mmeanza sisi tutamalizia bado sijazeeka baba yako'' lets wait and see
Wawe makini kwani Serikali haitachelewa kuwafuta kazi wote na kuajiri walimu wapya kwani walimu ni wengi sana.
Kwa walimu this is a pipe dream maana wengi ni waoga na hasa walimu wa shule za msingi ndio kabisaaa maana wao ndio victim wa vyeti vya kufoji na so hata maamuzi yao wengi ni butu kabisa,just imagine 244,400/= per month ambayo ni gross salary so bado reduction zingine kama vile income tax,PSPF,NHIF n.k. kinachobakia hapo ndio bado kodi ya nyumba,usafiri na mahitaji mengine binafsi na soko letu lenye mfumuko wa bei kila machweo!!!
lakini pamoja na shida zote bado wanakosa sauti ya pamoja kupinga dhuluma ya wazi hiyo. KAMWE HAKUNA MGOMO KWA HAO VIUMBE AMBAO UTAINYIMA HII SERIKALI RAHA KAMA VILE AMBAVYO MADAKTARI WAMEWEZA