Walimu waahidi makubwa - Lazima kitaeleweka

Ngoja niwaeleze walimu nguvu yenu mlionayo while you don't know; mwanzoni mwa miaka ya 90 nilikuwa nasoma secondary, i mean "O" level, nakumbuka kwenye uchaguzi wa rais na ubunge (rais tulikuwa tunapambanishwa na kivuri, mliokuwepo enzi hizo mnakumbuka), bwana Josephat Mungai alipambana na bwana mmoja namkumbuka kwa jina 1 tu, alikuwa anaitwa Mpiluka, nadhani alikuwa anafanya kazi CRDB (wakati huo ilikuwa ikimilikwa na Wakulima), bwana Mungai aliyafanya vizuri sana katika sekta ya Elimu, kule kwao Mufindi (kumbukeni pia enzi hizo kulikuwa hakuna majimbo ya ucgauzi, kila wilaya na mbunge wake, sio kama leo, wilaya 1 inaweza kuwa na wabunge hadi 4, full ufisadi) aliweka shule za sekondari kila tarafa na aliziwekea mawasiliano ya radio calls (hiyo ndo technolgy iliyokuwepo) hizi shule ziitwa za wazazi, mkewe Mungai alikuwa ndiye afisa elimu wa Wilaya, huyu mama alikuwa na jeuri ya ajabu, walimu walipokuwa na shida yeyote kwake, uwe mwanaume au mwanamke, lazima akuchefue roho kwa maneno yake, Sophia Simba hamfiki, sasa kwenye uchaguzi mwaka huo, walimu walikubaliana wang'oe mzizi, hilo ndio neno walilokuwa wakilitumia hizo enzi, kila vijiwe vya pombe (Ulanzi na komoni, sometimes Kangara) topic ilikuwa hiyo tu, kweli Mungai aling'olewa kwenye Ubunge, wazee wa Mafinga, hasa Malangali, mahali alipokulia huyu bwana walimwita kijana wao na kumwambia nini kilichomtokea, aliambia na hao wazee aende aka mdisplini mkewe, kweli mwaka 1995 Mungai alirudi tena, kumbuka amekuwa Mbunge wa huko since 1970, point yangu hapa nataka niwaambie walimu, wanayo nguvu kubwa sana kama wakiamua, wao ndo wanashughulikia kila kitu kinachohitaji man power kubwa katika nchi hii, kusimamia Kura, kuhesabu watu (sensor) kila kitu kinachohitaji manpower kubwa hapa nchini is Walimu, hawa wanaouwezo hata wa kuitoa ccm ikulu, issue tu, waweke uamuzi basi!

Migogoro hii walimu mnajitakia tu, mkiamua 2015 ccm bye bye!
 
ha ha ha ha .....
hiyo ni hisabati....
sipati picha ticha wa geography atakavyokuwa anafundisha "nchi ya Tanzania iko barani Msumbiji, upande wa kaskazini imepakana na Marekani upande wa kusini imepakana na Ivory Cost..........na mengi tu yanayofanana na hayo"
Kazi ipo..........

Pia atafundisha jua linatoka kusini kuelekea kaskazini. kazi kweli kweli
 
Jamani hili ni janga la Taifa....
Linatakiwa kushughulikiwa haraka sana na angalau wachache wenye akili waliobaki ..
 
mtoto wa mlalahoi ndiye anayedhurika at last! wakwao wanasoma kwenye ma-academy na ma international schools! au nje ya nchi kabisa! stupid president ever! thats kikwete!
punguza munkali mkuu, tutafika tu.
 
mtoto wa mlalahoi ndiye anayedhurika at last! wakwao wanasoma kwenye ma-academy na ma international schools! au nje ya nchi kabisa! stupid president ever! thats kikwete!

Walala hoi ndio wanaowapeleka hao watoto wa vigogo kwenye mashule mazuri kwa kodi zao. Hivyo lazima wakome ili wajifunze kuchagua viongozi watakao wajali.
 
Bora hawa mgomo wo uko hivi ila Daktar akiamua kukuandikia vipimo na dawa zenye hesabu sawa na hizoni balaa...
 
shule za serikali ni janga la kitaifa,wakati wao wanagoma private wanasoma kama kawaida,watanzania tutegemee gap kubwa la waliokuwa nacho na ambao hawana,shule za serikali ndio zinaongoza kwa kuferisha
 
Wanafunzi wakipotoshwa kwa njia hii, athari yake itawarudia wao wenyewe, kwa maana kwamba wadogo zao, watoto wao, ndugu zao watafundishwa hivi na walimu wengine sehemu nyingine itakuwaje?? Ni heri wasifundishe kuliko kupotosha, ni sawa na kupiga ngumi ukuta.
 
safi sana.



hapanaaaaaaaaaaaa!!! Kwa nini mfanye kosa ambalo hamtasamehewa na wanenu??? Wakati dawa ipo 2015?????????. Kataeni kuingizwa dhambini na serikali dhaifu isiyokuwa na hofu ya mungu.
 
Nimeipenda hii sana .Naamini baada ya kuwatumia wakaguzi next itakuwa kuleta waalimu toka nje ya Nchi kama China kuja kufundisha na watawatumia wanajeshi na kanda maalimu ya Kova na Rorya kufundisha
 
So madaktari wataendelea kuua.
Walimu watafundisha kwa kumislead.
Huu utamaduni unaojengeka ni wakijinga sana.
Hivi wanadhani wanamkomoa nani?AU SEREKALI?
Kwa akili zao wanadhani huyo serikali ninani?
 
Wanajamii ni vema tujadili jinsi ya kuwasaidia na kuacha matusi yasiyo na faida kwa watoto wetu kwani wao ndio waathirika .sasa tunapoporomoa matusi tanapata faida gani
:sad:
 
Sasa atakapokuwa anafundisha Biology nadhani ndio atawaambia wanafunzi wa-copy from the Original
hata sipati picha itakavyokuwa!!
 
Wanafunzi wakipotoshwa kwa njia hii, athari yake itawarudia wao wenyewe, kwa maana kwamba wadogo zao, watoto wao, ndugu zao watafundishwa hivi na walimu wengine sehemu nyingine itakuwaje?? Ni heri wasifundishe kuliko kupotosha, ni sawa na kupiga ngumi ukuta.

hao watoto wakijakuwa vibaka na kukaba watu sijui hasara inakua kwa ccm au jamii nzima kwa ujumla akiwemo mwalimu.
Ndo maana nasema watanzania tuna akili za kijinga sana.ni upuuzi huu unaweza kukuta tanzania peke yake.
 
ndio hapo sasa...huwezi mlazimisha mtu afanye kazi...maana walimu wataanza kufundisha utumbo huko darasani
 
So madaktari wataendelea kuua.
Walimu watafundisha kwa kumislead.
Huu utamaduni unaojengeka ni wakijinga sana.
Hivi wanadhani wanamkomoa nani?AU SEREKALI?
Kwa akili zao wanadhani huyo serikali ninani?

serikali ni mimi na wewe . na ni sisi tumechagua watu wachache waweze kutuongoza ili tuweze kufikia malengo fulani. lakini shida inatokea pale hao wachache wanavyo tumia rasilimali tulizo pewa bure na Mungu kwa faida yao binafsi. kwanini hiyo keki tusigawane sawa. au ni ule usimi kuwa all human being are equal but some are more equal.
my note
viva walimu. lazima kieleweke.
 
Back
Top Bottom