Walimu wa sayansi kutoka nje waanza kuajiriwa

mlaizer

JF-Expert Member
Jan 31, 2011
233
41
TANZANIA imeanza kutekeleza mpango wa kuajiri maelfu ya walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa ni njia ya kukabiliana na upungufu wa walimu 85,000.

Akizungumza jana, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa alisema
mchakato wa kuajiri walimu kutoka nchi wanachama wa jumuiya hiyo umeanza na
utakuwa endelevu mpaka hapo watakapojitosheleza.

“Kwa kuwa lengo letu ni kukuza masomo ya Sayansi, tumeanza na tunaendelea kuajiri
katika nchi nne za jumuiya, sitaweza kukupa takwimu kwa sasa maana kila watu wanaajiri
maeneo yao, na naweza kukuambia leo hivi kumbe kesho imebadilika, labda mpaka
baadaye,” alisema.

Mwaka jana, nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki iliipa kipaumbele suala la
elimu kama moja ya sekta ambayo itafaidika na soko la ajira chini ya mpango wa Soko la
Pamoja.

Awali, Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Abdallah Abdullah alisema jijini Arusha hivi karibuni kuwa, Baraza la Mawaziri la jumuiya hiyo limetoa baraka kwa Tanzania kuajiri walimu mwaka huu kwa lengo la kuziba pengo.

Ilielezwa kwamba, Serikali ina mpango wa kuajiri walimu wa Hisabati na Sayansi kwa
shule za sekondari wapatao 3,200 kutoka Kenya na Uganda.

Tanzania inahitaji karibu walimu 31, 000 wapya kwa ajili ya shule za msingi na sekondari ndani ya miaka miwili ya kutoa elimu bora kwa ongezeko la wanafunzi waliojiunga kwa miongo miwili iliyopita.

SOURCE:HABARILEO
MY TAKE:wale walimu wetu tuliokuwa tunawandaa tangu 2005 kutoka DUCE,MKWAWA,UDOM, n.k kama mkakati wa serikali kuondoa tatizo la walimu nchini wako wapi?Serikali haioni kama inajichanganya kimaamuzi?Tanzania kuna walimu wengi lakini walimu hao hawajitokezi kufundisha kutokana na maslahi duni na miundombinu mibovu ktk sehemu za kufanyia kazi.serikali na walimu wana migogoro ambayo mpaka sasa hayajatatuliwa,je kuwaajiri walimu kutoka nje inaweza ikawa ni suluhisho la matatizo?serikali haiwezi kuona kama wanaweza kuongeza mgogoro mwingine kwa walimu wa nchi za jirani(afrika mashariki)ikiwa tu imeshindwa kuwatimizia walimu wazawa?
NAWASILISHA
 
Hivyo hivyo walimu wenyewe wa Kibongo waoga kudai haki zao!! Ngoja waje wenye njaa na watalipwa pesa nyingi, haswa wale walimu hewa. Bomu lingine hilo linatengenezwa!!
 
Ule msoto wa pale udsm hasa department za kemia,botany,zoology,maths,physics,afu wanasiasa wanaleta upuuzi kukulipa kiduchu,hv wanajua ugumu wa kusoma au kufundisha masomo ya sayansi,karibu 80% ya walimu wa sayansi,wanafanya vibarua vngne,hadi pale serikali itakapojielewa.
 
Hao wageni watafundisha shule za private au hizi tulizo soma sie tulikuwa hatuna pesa? Aaaah!!!! Labda wataajiliwa na maabara zao toka nje....ila kama ni za serikali, sayansi bado itakuwa issue kubwa sana. Nimemaliza form four nikiwa na picha kichwani kuwa kipp's apparatus ni kubwa kama sim tank.
 
Back
Top Bottom