Walimu Tz tunapata funzo lipi kwa walimu wa Kenya?

Jstrong

Member
Mar 24, 2011
60
13
Habari kuwa walimu Kenya wamefanikiwa kuongezewa 300% ya mishahara yao ni habari njema na isiishie hivyo tu bali iwe funzo kwa walimu na wafanyakazi wote nchini kuwa tunaposimama kudai jambo tunahitaji kujipanga na kulisimamia.
Je ni kwanini mgomo wa walimu tz haukufanikiwa?
1.Vitisho vya wanasiasa.walimu walitishiwa kufukuzwa kazi na kuambiwa si mgomo halali hizi zilikuwa ni propaganda.
2.Elimu si kipaumbele tz,Hili linajidhirisha pale raisi wa nchi anaposema 'bora madaktari wakigoma watu watakufa lakini mtakachoathiri walimu ni kuchelewa kukamilisha scheme zenu' Analisema hili akiwa haoni kabisa ubaya wa hilo ndo maana anasema hata mkigoma miaka nane hamtolipwa.
3)Uoga wa walimu tz.Walimu tz ni waoga kiasi kwamba maneno ya wanasiasa wasio wataalam yanawayumbisha kiasi cha kukosa msimamo kabisa.
4)Matumizi mabaya ya mahakama.Serikali ktk vpnd tofauti imetumia mahakama kama ngao ya kunyamazisha wadai haki kwa kusema kuwa mgomo ni batiri, nakwa sababu mahakama ni matokeo ya serikali haina ubavu wowote wa kuamua chochote dhidi ya serikali.Mara kadhaa serikali imepuuza amri halali ya mahakama hiyo hiyo ambayo inaikingia kifua serikali wakati wa maslahi yake. Mf mzuri ni machimbo Bulyanghuru ambapo mahakama iliamuru wachimbaji wadogo wasiondolewe migodini lakini kwa kiburi watu walifukiwa udongo na wakauwawa.
4)Udhaifu wa CWT.Nikiwa ni mwalimu kwa dhati kabisa nasema kuwa uongozi cwt ni wanafiki na mafisadi wakubwa,huku walimu tukilazimishwa uanachama,ili wapate fedha zaidi tunakatwa fedha lukuki kila mwezi bila maendeleo,Je ninini mafanikio makubwa ya cwt mpaka sasa?
A)wameshindwa kuwaonganisha walimu,
B)wamekosa mbinu mbadala za kuboresha maslahi ya walimu.
C)Hawakubaliki kwa wanachama kwa usaliti wa kujilipa mishahara mizuri bila kuwajibika ipasavyo kwani walimu wana matatizo kuliko watumishi wengine wowote wa serikali.
D)Walimu kutofahamu wala kutohusishwa kwenye maamuzi mbali*2.Kwa mfano mgomo uliopita walimu wengi tulisikia kwenye vyombo vya habari tu na kukubali au kukutaa mgomo hatukupiga kura hivyo kwa kifupi tunaburuzwa.
5)Watz kutothamini elimu.Wakati mgomo unaendelea watz wapo kimya kanakwamba mgomo uwepo usiwepo ni sawa tu kwao.ndio maana serikali inakiburi cha kujibu vyovyote na audience wakasema ccm oyee. Oyeeee.
Hivyo kwa tz elimu haina mwenyewe ndo maana inageuzwa na wanasiasa vyovyote watakavyo tu tofauti na kenya ambapo elimu kwao ni muhimu na mtu akiichezea atawajibishwa but bongo aah sio ishu.
 
Thread yako ni ndefu mno, sijaweza kuimaliza, hata hivyo; unataka kuwaonea walimu wa Tanzania, hilo swali unatakiwa uwaulize viongozi wako wa kitaifa.
 
Funzo ni kuwa: Walimu wa Tanzania wakigangamala wataongewa mshahara kama wale wa Kenya waliogoma kwa wiki tatu na sasa matokeo yake kima cha chini cha mshahara Kenya ni Sh. 39,000/= (sawa na madafu 700,000/=)
 
Thread yako ni ndefu mno, sijaweza kuimaliza, hata hivyo; unataka kuwaonea walimu wa Tanzania, hilo swali unatakiwa uwaulize viongozi wako wa kitaifa.

Soma tu mkuu, nimeshindwa kufupisha, na pia hii ni positive challenge to teachers and workers of tz 2b strong and with common stand. Na sio lawama kwao.
 
Back
Top Bottom