Walimu mwaka huu nje kusimamia uchaguzi?

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Jul 27, 2008
3,173
481
Wandugu salamu,

Katika pitapita yangu nimekutana na hii.
ETI MWAKA HUU TUME YA UCHAGUZI HAITATUMIA WAALIMU KUSIMAMIA UCHAGUZI!
Je haya ni ya kweli? Na kama ni ya kweli, Je ni kuthibitisha kuwa bifu kati ya serekali ya JK na wafanyakazi inaendelea? Je JK anaogopa kuhujumiwa na waalimu?
Miaka nenda rudi tulizoea kuona serekali ikitumia nguvu kazi hii.
Ni nini mtizamo wako kuhusu hili?
 
Wanaandikishwa vijana wanaokunywa mbege huko mtaani. Tena ni lazima watoe kitu kidogo kwa watendaji. Watarudishaje hicho kitu kidogo bila kupewa nao kitu kidogo?
 
TISS watasimamia ili waibe kura.....

TISS watatosha TZ nzima? mwka huu kitaeleweka, labda tume ya uchguzi wameze maneno yao kura zisihesabiwe vituoni na kutangazwa hapo hapo.. ama la ya KIVUITI yanakuja bongo mwaka huu!
 
kwani wasimamizi wa uchaguzi wameshatangazwa? Na je walimu wana makubaliano na serikali kusimamia uchaguzi?
 
Serekali chini ya tume ya uchaguzi ilikwa na utaratibu wa kuwatumia waalimu kipindi cha uchaguzi, kuanzia kuandikisha hadi siku ya uchaguzi. Sasa mwaka huu inasemekana kuwa tume itatumia wanakijiji kufanya kazi hii. Swali ni je NI ILE BIFU YA JK NA WAFANYAKAZI AMA?
 
Thanks kwa ufafanuzi mkuu ila swali jengine ni inakuwaje sasa watumie wanakijiji vigezo vipi walivyovitumia kutumia walimu before na sasa wanatumia wanavijiji huoni kama ile hoja ya jamaa kuwa TISS watatumika sasa hivi kufanya ufisadi....
 
TISS nchi nzima hawapo na hawataweza. Wasiwasi ni kuwa JK alishawaambia kuwa "HAITAJI KURA ZA WAFANYAKAZI" waalimu ni jamii hiyo ya wafanyakazi. Sasa kama watawekwa kusimamia si watamhujumu? Na si inawezekana kuwa wakakataa chochote ili wakubali kura kuibwa?
Dawa waliyoiona ni kuwaweka pembeni tu.
 
Mie naona kama CCM inaelekea kushindwa unless watumie force maana hao TISS watafanya mangapi? Wasimamie uchaguzi, wasimamie nani anatoa siri za CCM, wasimamie kama informer wa rais, wamshughulikie Dr Slaa. Kwa sie wengine tunaona dalili kwa mbali either CCM itumie nguvu kushinda au watashindwa mwaka huu only time will tell
 
Kutokana na hali ngumu ya maisha ya walimu hasa vijijini, si rahisi wao kuacha posho ya kusimamia uchaguzi. Kumbuka walimu wameenea Tz nzima tofauti na wafanyakazi wa taasisi nyingine na kwamba kama hawatashirishwa wataharibu sana.
 
Kwani ni lazima wawatumie waalimu? Kuna maafisa mifugo, shamba na watu kibao. Walimu siyo sheria kuwatumia
 
Labda tungeweka wazi! JK ametamka hataki kura za wafanyakazi ambao wanakadiriwa kuwa zaidi ya 300,000. Afisa mifugo, bwana/bibi shamba wote wafanyakazi. Wanachojaribu kukwepa ni kuhujumiwa na hawa wanaoitwa wafanyakazi.
 
Kwani ni lazima wawatumie waalimu? Kuna maafisa mifugo, shamba na watu kibao. Walimu siyo sheria kuwatumia

Wote hao katika jimbo moja hawafiki hamsini wakati vituo vya kupigia kura ni zaidi mia tatu kwa jimbo moja la TZ bara. LAZIMA tu atawatumia. TISS itasaidia tuu kuselect walimu wenye msimamo chanya dhidi ya serikali na kuwatumia kama wawakilishi/maafisa wa tume.
 
Sasa huu ni wakati wa Lewis Makame kumuuliza Kivuitu wa kenya alijisikia je wakati ule alivyotangaza matokeo ndivyo sivyo? Maana huenda hali kama hiyo ikamtembelea mwaka huu. Dalili zote za Jk kuanguka mwaka huu zipo wazi.
 
Wandugu salamu,

Katika pitapita yangu nimekutana na hii.
ETI MWAKA HUU TUME YA UCHAGUZI HAITATUMIA WAALIMU KUSIMAMIA UCHAGUZI!
Je haya ni ya kweli? Na kama ni ya kweli, Je ni kuthibitisha kuwa bifu kati ya serekali ya JK na wafanyakazi inaendelea? Je JK anaogopa kuhujumiwa na waalimu?
Miaka nenda rudi tulizoea kuona serekali ikitumia nguvu kazi hii.
Ni nini mtizamo wako kuhusu hili?

sasa unatuletea habari za kupitapita mitaani kweli hiyo inaingia kichwani kwa hapa jf?
binafsi sitaki kujadili fitina.
 
Wandugu salamu,

Katika pitapita yangu nimekutana na hii.
ETI MWAKA HUU TUME YA UCHAGUZI HAITATUMIA WAALIMU KUSIMAMIA UCHAGUZI!
Je haya ni ya kweli? Na kama ni ya kweli, Je ni kuthibitisha kuwa bifu kati ya serekali ya JK na wafanyakazi inaendelea? Je JK anaogopa kuhujumiwa na waalimu?
Miaka nenda rudi tulizoea kuona serekali ikitumia nguvu kazi hii.
Ni nini mtizamo wako kuhusu hili?

Kama siku zote ilivyo. Thread kama hizi ni umbeya mtupu. Mara zote huwa tunasemaga unapoleta thread hapa iwe na chanzo kinachoeleweka, Sasa wewe bwana mkuu umetoka sijui kulewa zako mbege unakuja na vitu ambavyo havina kichwa wala miguu na kwa sababu wana JF wengi wapo ant-jk, walichofanya na wanachofanyaga ni kuanza kuponda tu hata kama ni pumba iliyoletwa. Lets we talk facts na sio umbea. hautatufukusha popote.
 
Wameamua kuwatumia wanafunzi wa vyuo vikuu. Hivi sasa wapo Zanzibar, baada ya kusimamia zoezi la kura ya maoni sasa wanapata training kidogo...
 
Back
Top Bottom