Walimu 40 sumbawanga waingia mitini........!

Ochutz

JF-Expert Member
May 21, 2011
465
105
Walimu 40 katika wilaya ya sumbawanga 'wameingia mitini' huku wengine 50 wakiingia kwenye mgomo usio na kikomo wakiishinikiza halmashauri kuwalipa mishahara pamoja na madai mbalimbali wanayodai kwa zaidi ya miezi mitatu sasa. Jamani wenye dhamana uko serikalini timizeni wajibu wenu. Tuache kuwa wabinafsi.
 
Hii serikali haipati akili tu? si wawaandae walimu toka mikoa husika? Ama si wawape maslahi yanayoridhisha? MWalimu ni mtu muhimu sana katika jamii. Mwalimu akiharibu tujue na mwanafunzi ataharibu tu! Na ndio maana tunakuwa na dotcom wengi kwa jamii. katika nguzo mojawapo za uchumi, incentive ni muhimu sana. Nafaidikaje na jambo fulani?

Kila mmoja anahitaji motisha wa namna fulani na sio kudanganyana kujazana uzalendo na wito ambavyo katika hili soko huria ni mambo ya kutiliwa shaka. Wanasema tena hakuna vya dezo dezo. Nipe nikupe. Mwalimu anaizalishia serikali/jamii wasomi. Mpeni mazingira sahihi ya kutekeleza wajibu wake ili mwishho wa siku muweze kumbana. kwamba tulikupa vitendea kazi na rasilimali zote ulizotaka. wapi output yako? Lakini kwa mazingira ya sasa ni vigumu kumbana mwalimu kwa staili hii.

Hata hiyo wanayoita OPRAS-Open Performance Review and Appraisal System haina maana katika mazingira kama haya. Maana ili hiyo OPRAS ifanya kazi kwa ufasaha inabidi mwajiriwa apewe kila kitendea kazi anachohitaji ili mwisho wa siku mkikaa na mwajiri muanze kufanyiana tathmini bila mizengwe. Na hii si kwa walimu tu bali kwa sekta nzima ya umma. Sekta binafsi wanaweza kutekeleza hili maana wao hawana ruzuku toka serikalini.

Serikali inayajua haya yote ila sijui tatizo ni nini. Angalau mi naweza kujitetea sijui mfumo wa nchi unavyoendeshwa. Lakini hata rais hajui matatizo ya watz??????!!!!!!!!
 
umenena mkuu,ktk maisha ya leo(capitalism)ambapo huduma zinauzwa hauwezi tena kutamka kwa mwalimu kwamba ualimu ni wito...kwa sasa hii ni fikra potofu

walimu wa sasa wanahitaji pesa kama watumishi wengine na pasipo pesa nzuri na maisha mazuri kwa ujumla hatuwapati tena waalimu,watakimbia wote na serikali itabaki na adithi zake za ualimu ni wito,na iweje mtu aendelee kufanya kazi ambayo badala ya kukutoa kimaisha inakuletea umasikini,ya nini??
 
na huko sumbawanga kulivyo mbali na shida kufika halaf bado mnawanyanyasa hao walioamua kuja huko
wakiondoka hao imekula kwenu, tuseme ukweli tu ni wangapi wakipangiwa vituo vya kazi sumbawanga watafurahia
sasa hao inabidi muwape haki zao haraka sana
 
lakini si walishaambiwa sirikali haina bingo....acha tu watoke mbio!!
 
Mwalimu na kamshahara kake kadogo wanashindwa kumlipa,mbunge aliyeishia darasa la saba na mwenye fani ya kusinzia bungeni anapewa mamilioni,tunatumia mamilioni kwenye bites ofisini,mamilioni kuwapiga picha waheshimiwa utafikiri wao hawawezi kutumia hela zao kupiga hizo picha,kununua ma bmw x5...nk...kweli serikali haina hela
 
tutemee nini toka kwa serikali isiyo na vipaumbele? Chiligati anampinga zitto kwa macho makavu eti ccm watachukua posho hata kama wapinzani watazisusia. Ukichukua hizo posho ukachanganya na bajeti za chai na per diem na posho za vikao pamoja na semina, ukachanganya na za epa et al pamoja na bajeti halali za sekta husika unapata hela ya maana ya kuwalipa bila mizengwe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom