Walidharau Sekta ya Afya sasa Tunabanana Samunge

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,452
Hii Imekaaje Mazee?

Ndugu hao wa Pinda, walifika Samunge saa saba mchana na magari matatu aina ya Toyota Land Cruiser, VX na Prado yenye namba binafsi na walikuwa wamewekewa ulinzi usiokuwa wa kawaida.

Na hii Je?

Ofisa wa Serikali, ambaye alishiriki katika mchakato wa mapokezi ya ndugu hao, alisema ni ndugu wa karibu wa Waziri Mkuu Pinda, ambao wametoka nyumbani kwake na ndio sababu wamepewa upendeleo maalumu katika kupata tiba hiyo.

Sina la Kusema

Hata hivyo, haikuwa rahisi kupata picha zao wakati wakinywa dawa baada ya maofisa wa usalama kuzuia wasipigwe picha kwa maelezo kwamba safari yao hiyo ni ya binafsi.Ujio wa ndugu hao, unafanya iwe familia ya pili ya vigogo wa Serikali kutua Samunge, familia nyingine iliyofika ni ya Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi ambapo watoto wake na wake zao walifika Samunge kupata kikombe cha Babu.

Sasa kwa Nini Wasitangaze Samunge Kama Hospitali ya Rufaa?
 
hao uliowaona ni wachache.....hapa Yaeda mpaka tumeshazoea....mihelkopta kibao kila siku tena yenye reg tofauti tofauti inapita kwenda na kurudi Samunge......na ukiuliza nauli unaweza zimia.....kweli TZ kiboko cha matatizo
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom