Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,354
- 1,943
Source: Habari Leo
Shadrack Sagati
Daily News; Thursday,May 15, 2008 @00:01
Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba
Mimi nilikataa kwa sababu kuundwa serikali ya kitaifa ni pale tu ambako kuna mgogoro wa siasa, lakini Zanzibar hakuna kitu kama hicho, kujadili suala kama hili wakati kuna serikali ambayo iko madarakani kwa halali ni sawa na uhaini, alisema Makamba.
Katika watu wanaotia aibu na huruma katika siasa za Tanzania ni huyu Makamba. Sasa angalia hapo juu anasema nini. Kama Zanzibar hakuna mgogoro, kwa nini walikuwa wanakaa kwenye haya mavikao? Hebu tuanze kuwajibisha wanasiasa wetu kwa maneno yao. Kipimo kimojawapo kikubwa sana cha udhaifu wa JK ni kitendo chake cha kumteua Makamba kuwa Katibu Mkuu wa chama chake na sijui itawachukua miaka mingapi CCM kujua kwamba Makamba ni mzigo mzito kwa chama chao. Kwa kweli ilikuwa ni kumuonea sana kumteua Makamba kwenye nafasi hii kwa sababu imefanya hata wale waliokuwa hawajui wajue kiwango cha ununda wake!
Then, CCM wanapenda kutumia maneno loosely tu hivihivi, kila mara wakibanwa wanaibuka na neno uhaini, this is pathetic!