Walichokifanya Baraza la Mawaziri Linalovunjwa/Sukwa upy

kibananhukhu

JF-Expert Member
Jul 6, 2009
366
161
Wana JF, Naomba someni hii kwani itaweza kumsaidia kila mmoja wetu. Walichokifanya Baraza la Mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Kwanza Ni sawa na mfano wa Muhogo hapa chini: -

Jamaa mmoja alikufa akiwa na miaka 65. Alipokelewa motoni na aliwakuta watanzania wengi sana wako PEPONI kwa jinsi walivyohukumiwa kwa huruma ya kuishi kwa umasikini wake hapa duniani.Kule motoni kulikuwa na mawaziri wengi sana marehemu, wafanyabiashara wakubwa, na baadhi ya watumishi wa Mungu wakiungua na kupata mateso makubwa sana.Kukawa na waziri mmoja ambeye alishindwa kabasa kuvumilia matesa yale, na muda wote alikuwa akilia sana kwa mayowe ambayo yalifanya Mbinguni kusikalike.

Hapo ndipo Mungu Mwenye Huruma akaamua kumtuma Malaika wake ili aende akamuulize yule waziri, kwanini alikuwa anapiga kelele nyingi sana hadi mbinguni hakukaliki?
Jamaa akajibu akasema eti anaonewa, na watanzania wengine kule peponi alikuwanao hivyo alipaswa awe nao kwenye maraha. Hapo Mungu akamtuma malaika amuulize, “Je? Ana “jema” au wema au jambo zuri lolote ambalo amewahi kulifanya katika maisha yeke duniani? Yule jamaa akakumbuka kuna siku eti alikuwa anatembelea baadhi ya mahekari yake ya mashamba na alipolitembelea shamba lake la mihogo akakutana na mama mmoja masikini wa kutupwa.

Yule mama akamuomba waziri mihogo ili watoto wake wasiendelee kufa njaa.
Jamaa alimrushia usoni yule mama kipande cha muhogo chenye ukubwa “size” ya kiberiti, hakifai kwa udogo wake hata kwa kutafuna. Na huo ndo ukawa wema ambao jamaa, Waziri aliikumbuka kuufanya duniani.Basi, Mwenye Enzi Mungu akamtuma malaika kuwa, kwa kuwa jamaa alitoa kipande kidogo cha mhogo basi wewe malaika mpelekee muhogo mkubwa. Wakamrushia mhogo mkubwa sana kule motoni.Jamaa baada ya kuudaka ule muhogo, Muhogo ule ukaanza kunyanyuka, kuelekea peponi, Waziri akagundua kuwa ile ni “lift”. Akafurahi sana kuona anainuliwa kuelekea peponi.

Basi baadhi ya mawaziri na watu wengine waliokuwa nao kule motoni wakamshika na kila aliyemgusa, alinasa na alianza kuinuka nao.
Mheshimiwa yule akahamaki, akawaambia, siyo ninyi mnaotakiwa kule. Shuka, tena shukeni haraka. Akaanza kuwapukutisha, akaanza kutumia mkono mmoja kuwagagadua kutoka katika mwili wake. Muda mfupi kabla ya kuingia peponi, jamaa akawa amebaki na watu watatu, wanamsihi sana awaache nao waingie peponi, lakini wapi. Mh. Aligoma hadi alipoona wanampotezea na hawamuachii akalazimia kutumia mikono yote miwili, akaachia mhogo wakati akiwa amebakiza mita moja tu kuingia Mbinguni, Na wakati “masela” wote wa mbinguni waliokuwa peponi wamekwishamuona na wanamshangilia kwa furaha.Yeye akawa bize, kutaka kuhakikisha anaingia peponi peke yake.

Akauachia mhogo, akafanikiwa kuwashusha wote motoni PAMOJA NA YEYE MWENYEWE Kwani Mhogo haukuwasubiri, Wakazama Hadi hii leo, wote wanateseka MOTONI.
Hii tabia itaweza kutuponza watanzania wengi kwani hakuna hasara yeyote mtanzania ataweza kupata kwa KUMPENDA jirani au jamaa yeke. Hakuna Hasara mtanzania anaweza kuipata kwa KUMSAIDIA AU KUMKOMBOA Mtanzania. Lakini kuna hasara kubwa sana, na madhara makubwa sana yanayowezapatikana kwa kutowapenda watu na kuto wasaidia watanzania kufanikiwa.
 
Hii ni kwa wale wenye matatizo ya kusoma haya maandishi kama mimi.

Nilipoona Sukwa nikamkumbuka mtu mmoja alikuwa UVCCM akiitwa Sukwa Said Sukwa.
 
Back
Top Bottom