Wali Special Thread: Jifunze jinsi ya kupika mapishi mbalimbali ya wali

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,591
Jinsi ya kupika biryani ya kuku, ng'ombe au mbuzi

hqdefault.jpg


Mahitaji

  • 1 kilo mchele wa basmati mrefu
  • 1 kilo nyama iwe ya kuku au ng'ombe au mbuzi kata katika umbo dogo la kutosha kula kisha ichemshe na tangawizi na kitunguu swaumu, unga wa binzari (turmeric powder) pili pili manga na chumvi ili kuweka ladha nzuri. Ikisha iva itoe iweke pembeni na mchuzi wake uweke pembeni utautumia baadae.
  • 1 kilo ya vitunguu kata slice ( mviringo)
  • 1 kilo nyanya nyekudu zilizoiva, osha vizuri kisha katakata saizi ndogo ndogo sana
  • 240 ml ya samli au mafuta yeyote ya kupikia
  • 2 maggi chicken soup cubes
  • 3 kijiko kidogo cha chai unga wa pilipili mwekundu
  • 1/2 kijiko kidogo cha chai unga wa binzari (turmeric powder)
  • 3 kijiko kidogo cha chai unga wa girigilani (coriander powder)
  • 2 kijiko kikubwa cha chakula mchanganyiko wa tangawizi na kitunguu swaumu vilivyosagwa (ginger-garlic paste )
  • 50 gram korosho iliyo kaangwa usizisage zibaki nzima
  • 50 gram majani ya girigilani (fresh coriander leaves, washed and chopped)
  • 8-12 mbegu za nzima ya hiriki (green cardamoms)
  • 4 bay leaves ( sifahamu kiswahili chake)
  • 15 mbegu nzima ya pili pili manga (whole black peppercorns)
  • 30 gram majani mabichi ya minti ( mint leaves )
  • Chumvi kulingana na mahitaji yako

Jinsi ya kupika

  1. Weka mafuta katika sufuria yako iliyokwisha pata moto, kisha kaanga nyama yako iliyokwisha chemshwa mpaka iwe na rangi ya kahawia.
  2. Kisha itoe nyama hiyo na ichuje mafuta na mafuta yanayobaki weka kitunguu na endelea kukaanga kwa dakika 7-10 kisha weka unga wa binzali, unga wa pili pili mwekundu, unga wa girigilani, bay leaves, mbegu za hiliki na nusu ya mbegu za pili pili manga.
  3. Changanya vizuri mpaka utapata mchanganyiko mzuri mkavu miminia humo maji uliyotunza baada ya kuchemshia ile nyama yako na kuiweka pembeni ipoe. kisha weka nyanya fresh ndani ya sufuria yako pika mpaka maji yakauke na mafuta yaanze kuoneka kwa juu ndani ya sufuria.
  4. Kisha weka nyama yako ndani ya sufuria pole pole halafu punguza moto acha ijipike kwa muda mpaka mchuzi wako na nyama viwe na ladha pia usisahau kuweka chumvi kulingana na ladha unayopenda.
  5. Chukua sufuria nyingine weka mafuta ya samli na vitunguu kisha kaanga na majani ya girigilani, majani ya mint na korosho kisha funika kwa dakika 10.
  6. Weka wali wako mkavu uliokwisha oshwa vizuri na uchanganye vizuri. Ongeza vikombe 5 vya maji na chumvi kidogo. M
  7. Mchele ukishaanza kuchemka funika sufuria lako na punguza moto. Maji yakisha kauka kiasi weka mchanganyiko wa ile nyama yako nusu tu juu ya wali wa basmati na acha wali uive kabisa kisha utakua tayari kupakua na kula chakula chako kikiwa cha moto.
 
Jinsi ya kupika wali wa manjano

chef+issa+wali+manjano+%25287%2529.jpg


Mahitaji
  • 1 au 2 Saffron ( zafarani ya orange)
  • 4 kijiko kikubwa cha chakula Olive oil
  • 1 kitunguu kikubwa kata kata
  • 1 pili pli hoho katak kata vipande vidogo vidogo
  • 1 kijiko kidogo cha chai kitunguu swaumu cha kupondwa
  • 240 gram mchele wa basmati
  • 340 ml za maji ya vugu vugu
  • 5 gram ya chumvi
  • Majani kiasi ya giligilani kwa ajili kupambia na kuongeza ladha

Jinsi ya kupika
  1. Washa jiko lako katika moto mdogo, weka kikaango chako kwenye moto kisha weka mafuta, kitunguu maji na safron pamoja na endelea kukaanga pole pole.
  2. Baada ya mafuta kubadilika rangi ya machungwa yatoe katika moto na acha ipoe kwa dakika 10 kisha yachuje hayo mafuta.
  3. Chukua kijiko kimoja kikubwa cha mafuta na weka katika kikaango. Kisha chukua tena kitunguu maji na kitunguu swaumu endelea kukaanga mpaka vilainike. Kisha ongeza pili pli hoho na endelea kukaanga mpaka iwe laini.
  4. Kisha weka mchele na endelea kukaanga pole pole mpaka mchele utaponukia na kubadilika rangi na kulainika.
  5. Ongeza maji na ufunike iendelee kuiva kwa dakika 8-10 kwa moto mdogo mpaka iive.
  6. Baada ya kuiva kataka majani ya corriender na pamba katika wali wako.
  7. Unaweza kuongeza ladha ya chakula hiki kwa kuweka karanga au zabibu kavu au hata korosho kavu.
 
Jinsi ya kupika wali wa njegere

chef+issa+wali+njegere+%25288%2529.jpg


Mahitaji

  • 240 gram mchele wa Basmati
  • 120 gram njegele za kumenywa (chickpeas)
  • 3 majani ya kitunguu maji (spring onions), kata kata
  • 1 fungu la giligilani chop chop
  • 1 fungu la parsley chop chop
  • 1 kijiko kikubwa cha cakula siagi (butter) kwakuongeza ladha ya chakula
  • Chumvi kulingana na ladha upendayo

Jinsi ya kupika
  1. Chukua kikaango weka siagi ikisha ikiyeyuka weka majani kiasi ya kitunguu maji na uendelee kukaanga. Kisha chuja mchelewako wa basmati nao weka ukiwa mkavu na endelea kukaanga mpaka unukie.
  2. Weka chumvi pamoja na njegere koroga kiasi.
  3. Kisha weka maji safi 400 ml (hii inategemea na kiwango cha mchele wako) kisha funika mfuniko wa kikaango au sufuria yako na pika kwa dakika 10.
  4. Weka chop parsley na chop giligilani kisha koroga zichanganyike na wali wako.
  5. Baada ya hapo wali wako utakua umeiva na unaweza kula na mboga yoyote upendayo.
 
Jinsi ya kupika wali wa soseji na mboga za majani

chef+issa+wali+sausage+%2813%29.jpg


Mahitaji

  • 3 vipande vya sausage
  • 1 fungu la majani ya vitunguu
  • 1 kitunguu kikubwa
  • 100 gram njegere
  • 500 gram chele basmati
  • 5 gram chumvi
  • 5 gram pili pili manga

Jinsi ya kupika

  1. Weka mafuta ya kupikia kwenye kikaango chako kisha weka vitunguu maji na uvikaange.
  2. Ongezea majani mabichi ya vitunguu na uendelee kukaanga hadi vitoe harufu na sio kuungua au kubadilika rangi.
  3. Weka mchele na ukaange kwa dakika 3 mpaka 4 kisha weka maji ya wastani yazidi mchele wako kiasi na uendelee kukoroga ili maji yachanganyike na mchele wako.
  4. Funikia na weka moto wa wastani ili wali wako uive taratibu.
  5. chukua sausage zako na kata kata vipande vidogo kisha weka juu ya wali wako njegere zilizochemshwa pamoja na vipande vyoote vya soseji.
  6. Kumbuka kuendelea kukoroga ili kila kitu kichanganyike, pia kama wewe ni mpenzi wa blue band au samli unaweza weka kiasi ili kuongeza ladha na harufu katika wali wako.
  7. Baada ya dakika 45 wali wako utakua umeiva kama haujaiva basi ongezea maji kidogo na endelea kupika katika moto mdogo.
 
Jinsi ya kupika wali wa kukaanga wa kitunguu swaumu

Chef+issa+wali+kitunguu+swaumu+%25287%2529.jpg


Mahitaji
  • 500 gram za wali ulio iva
  • 2 kijikjo kikubwa cha chakula kitunguu swaumu kilichosagwa
  • 4 mbegu nzima za kitunguu swaumu kilichomenywa (sio lazima)
  • 4 miti ya majini ya kitunguu maji chop chop
  • 5 gram chumvi
  • 1 kijiko kikubwa cha chakula cha siagi (butter)

Jinsi ya kupika
  1. Weka siagi kwenye kikaango kilichokwisha pata moto ili iyeyuke kisha weka mbegu za kitunguu swaumu ziendelee kuiva.
  2. Kaanga mpaka iwe ya kahawia hakikisha haiunguwi kisha toa hizo mbegu na weka pembeni..
  3. Katika kikaango hicho hicho, weka kitunguu swaumu cha kusagwa na majani ya kitunguu maji mabichi yalio katwa katwa
  4. Mchanganyiko wako ukishalainika na kutoa arufu nzuri, chukua wali wako na weka katika kikaango na hakikisha una changanya haraka haraka
  5. Weka zile mbegu za kitunguu swaumu ulizokaanga mwanzo na uendelee kuchanganya ili iweze changanyika vizuri.
  6. Chakula hiki unaweza kula na mchuzi au mboga ya aina yeyote.

 
Jinsi ya kupika pilau ya nyama ya kuku, ng'ombe au mbuzi

chef+Issa+-+Pilau++%25288%2529.jpg


Mahitaji
  • 240 gram za mchele
  • 240 gram za nyama iwe ya kuku au ng'ombe au mbuzi kata katika umbo dogo la kutosha kula. Ili nyama yako iwe laini chukua papai lililoiva baada ya kukatakata nyama pondea papai katika bakuli lenye nyama kisha weka chumvi kidogo, soya sauce kidogo, kitunguu swaumu na tangawizi kwa ladha zaidi. Nyama hii iweke kwenye friji kwa dakika 45 tu iwe ndani katika mchanganyiko huu itakua laini sana na utaipika kwa muda mfupi.
  • 1 kijiko kidogo cha chai mbegu za binzali nyembamba (cumin seed)
  • 1 kitunguu kikubwa kata kata
  • Nyanya kubwa kata kata
  • 3 spring onions (majani ya kitunguu)
  • 1 bay leaf
  • 3 cloves (Mbegu za Karafuu )
  • 3 cardamom ( mbegu za hiriki)
  • 1/2 kijiko cha chai kidogo turmeric powder ( Unga wa manjano)
  • 5 gram kitunguu swaumu
  • 1 pilipili mbuzi kata kata
  • 5 gram unga wa tangawizi au ya kusagwa
  • 1 kijiko kidogo cha chai garam masala
  • 600 gram coconut milk (Tui la nazi) sio lazima kama hutumii nazi basi weka maji kawaida
  • 5 gram chumvi
  • 1 fungu la giligilani kwa jili ya kupambia
  • 1 kijko kidogocha chai maji ya limao (sio lazima)

Jinsi ya kupika
  1. Katika sufuria weka kijiko 1 kikubwa cha chakula mafuta kisha kaanga mbegu za binzali nyembemba, bay leaf, karafuu, mbegu za hiriki, kitunguu swaumu, pili pili mbuzi, tangawizi, nyama na chumvi kisha kaanga.
  2. Kitunguu kikishalainika weka nyanya pamoja na unga wa manjano na garam masala. Kaanga kwa dakika 2.
  3. Weka mchele hakikisha unauweka bila maji. Hakikisha una ugeuza geuza mpaka mchele ubadilike rangi na kutoa harufu safi baada ya kuukaanga.
  4. Ongeza tui la nzai au maji kwa wale wasio tumia nazi endelea kukoroga ichanganyik vizuri.
  5. Funika na mfuniko kisha pika kwa dakika 10 au mpaka mchele wako utakapoiva na kuwa wali.
  6. Kisha ugeuze wa chini uje juu na wajuu uende chini.
  7. Kwa kuipendezesha pilau yako sasa mwagia kwa juu majani ya kitungu na majani ya giligilani kisha nyunyizia kwa juu maji ya limao kwa sababu kuu mbili. Moja ni kuongeza ladha. Pili inasaidia kupunguza kiwango cha sodium.
  8. Kwa wale wapenda samli unaweza weka kijiko kimoja pia itaongeza harufu na ladha safi katika pilau yako.
 
Jinsi ya kupika pilau ya njegere

chef+issa+pilau+mboga+%287%29.jpg


Mahitaji

  • 250 gram mchele wa basmati
  • 1 kijiko binzali nyembamba (cumin seeds)
  • 1/2 kijiko kidogo cha chai garam masala
  • 1/2 kijiko kidogo cha chai coriander powder
  • 1/4 kijiko kidogo cha chai turmeric powder
  • 60 gram njegere za kuchemshwa
  • 1 kitunguu maji chop chop
  • 3 nyanya za kuiva nazo chop chop
  • 1 kijiko kidogo cha chai tangawizi ya kusagwa
  • 1kijiko kidogo cha chai kitunguu swaumu cha kusagwa
  • 2 pili pili mbuzi, kisha kata vipande vidogo vidogo
  • 60 gram korosho au karanga za kukaanga (sio lazima)
  • 1 kijiko kidogo cha chai siagi au mafuta ya samli kwa ladhamajani ya giligilani na majani ya mint kwa kupambia na kuongeza ladha

Jinsi ya kupika

  1. Weka kijiko kimoja cha mafuta ya kupikia kwenye kikaango kama ni samli au siagi, kisha garam masala, unga wa manjano, binzali nyembamba na unga wa corienda kaanga kidogo kisha weka kitunguu swaumu, kitunguu maji, tangawizi, pilipili mbuzi na nyanya zote ziwe chop chop vipande vidogo kama inavyoonekana kweny picha. Kisha weka chumvi, karafuu na pili pili manga endelea kukaanga.
  2. Ukishapata harufu ya kunukia na mboga zako ziwe zimeanza kuiva basi mimina mchele na endelea kukaanga wali wako huku ukiuchanganya uchanganyike vizuri kabisa na mboga kwa dakika 2 au 3. .
  3. Weka gram 600 za maji kisha koroga na funika na mfuniko acha iive kwa dakika 10 kwa moto wa wastani.
  4. Baada ya dakika 10 itakua imekaribia kabisa kuiva, kisha weka njegere zilizoiva na koroga kidogo ichanganyike kisha pika kwa dakika 2 tena.
  5. Baada ya pilau yako kuiva basi juu yake weka majani ya mint au giligilani kuongeza uzuri wa rangi, ladha na harufu safi sana katika pilau yako.
  6. pia ukiwa mpenzi wa siagi weka kwa juu kiasi au unaweza mwagia samli hii nikuongeza harufu nzuri na ladha zaidi.
  7. Usisahau kuweka karanga au korosho za kukaanga kwa juu.

 
Good to see you too my dear. Pilika pilika za maisha zimezidi ndio maana nimekuwa adimu mpendwa. But now am back and this time I am fully loaded...:wink2:

i really can see you are fully loaded............

asante sana kwa maujuzi...unapikaga hivyo ama la?
 
i really can see you are fully loaded............

asante sana kwa maujuzi...unapikaga hivyo ama la?

Vyakula vyote ninavyopost huku ndivyo ninavyopika na kupendelea kuvila... Ntakualika siku moja nyumbani nikupikie chakula kizuri na kitamu ambacho nina imani hata wewe utakifurahia.
 
wali umevutia sana,HIV huu mchele wa basmat tunaweza kulima mpunga wake,maana unapendeza kwa kweli
 

Similar Discussions

13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom