Wali Uliwe kwa Mikono au Kijiko?

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,452
Ninalo Swali jamani, linalotatiza kichwa changu
Kila lijapo mawazoni,laniongezea wazimu
Nashindwa niseme nini, nabaki ni kama bubu
Wali uliwe kwa mkono, au Kijiko Jamani?

Wa maharage fikiria, wengine wasema mandondo
Upikwe kwa jiko la mkaa, si la gesi hata oven no
Kwa nazi ukachuriziwa, watamanisha kwa Uhondo
Wali uliwe Kwa mikono , au kijiko Jamani?

Ha ha ha Wanajamvi, Naomba Mnisamehe
Nimeyataja Mandondo, Mate yawatirirka
Keyboard zapiga short, kwa Mate yatiririkayo
Wali Uliwe Kawa mikono, au kwa Kijiko Jamani?

Wali uwe wa Kyela, wa Kamsamba hata wa Rukwa
Utiwe nazi hata mafuta, wanukia kwa Maraha
Si kwa Mandondo peke yake, Dagaa nao watia For a
Wali Uliwe kwa Mikono, au kwa Kijiko Jamani

Wengine wauta pilau, wengine sijui biriani
Uwe wa Kempisk hata Royal palm, Mama Cheusi naye anatisha
Mhhh jamani wali mtamu, upikwe na fundi kweli
Wali Uliwe kwa Mikono, au kwa Kijiko Jamani?

Malenga nawachia swali, naombeni jibu haraka
Nashikwa na Kigumumuzi, maana sahani I mezani
Nipeni jibu Haraka, Nianze kuufakamia
Niule wali kwa Mkono, au Kijiko cha nauliza?
 
Naja kwa mbwembwe, mikono ndo yenyewe Ndege
Vijiko ni kwa wakolembwe, faidi wali kwa raha muulize rage
Wali lazima ukombwe kombwe, Mikono kazi yake wewe Mkelege
Mikono ina kazi nyingi, moja wapo kulia peku peku wali
 
Naja kwa mbwembwe, mikono ndo yenyewe Ndege
Vijiko ni kwa wakolembwe, faidi wali kwa raha muulize rage
Wali lazima ukombwe kombwe, Mikono kazi yake wewe Mkelege
Mikono ina kazi nyingi, moja wapo kulia peku peku wali

Ha ha Mkuu Masanilo Rage anaifahamu raha yake siyo ee teh teh teh
 
Ndege ya Uchumi nimependa jinsi ulivyopanga vina na mizani kwenye hili shairi lako
 
Ingekuwa umesema pilau, ningekwambia iliwe kwa mkono kwani pilau inakuwa imechanganyikana na nyama, so inakuwa rahisi kusearch nyama kwa mkono kuliko kwa kijiko !
 
Ingekuwa umesema pilau, ningekwambia iliwe kwa mkono kwani pilau inakuwa imechanganyikana na nyama, so inakuwa rahisi kusearch nyama kwa mkono kuliko kwa kijiko !

Ha ha ha Mkuu Sinkala Kuku nini Kuku tu Jogoo Jina, Wali ni wali tu Pilau Jina. Thanx
 
Wali wa jamvini shurti ulime kwa mkono, lakini ule wa buffet kijiko ndio hakimu wake!!
 
Hodi hodi bwana ndege, Kompaki nimeingia
nimekuja na perege, wali kuufakamia
natumai si kama zege, umepikwa wajiachia
yaonesha huna njaa, wacha tukusaidie!

Kwa mikono kwa kijiko, haijalishi jamani
labda mfungwa wa keko, asiyechagua maini
kipi kizuizi chako, kujua utumie nini
yaonesha huna njaa, wacha tukusaidie!

Hebu fungua mlango, sato wangu yuapoa
kwako ninagonga ngogo, mwenye njaa meingia
staha nazipa mgongo, kijoko sitatumia
yaonesha huna njaa, wacha tukusaidie!

*NB: nimejibu from direct/literal translation...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom