Walevi Bana

Buswelu

JF-Expert Member
Aug 16, 2007
1,998
351
Wamekutwa wanakunywa pombe za kienyeji wakati wa kazi....sasa wanaelezewa...mmoja anajifanya yuko busy anachukua notice ha ah...
Mlevi.JPG
Picha kwa hisani ya michuzi blog
 
Huyo anayeandika ni Katibu Mtendaji wa kijiji(VEO)!...Huyo mama aliyevaa t-shirt ya njano na kijani imeandikwa maneno gani eti?
 
Wamekutwa wanakunywa pombe za kienyeji wakati wa kazi....sasa wanaelezewa...mmoja anajifanya yuko busy anachukua notice ha

hivyo ni kosa? Mbona Dar es salaam ni kinywaji masaa 24? Au hii sheria inahusu pombe za kienyeji tu?
 
hivyo ni kosa? Mbona Dar es salaam ni kinywaji masaa 24? Au hii sheria inahusu pombe za kienyeji tu?

Itakuwa vijijini ambako kuna ardhi na shughuli zingine za kilimo na inachukuliwa kama uzembe...na kutoshughulisha kichwa...dar wanaweza uwana...na watu..wengine wana roster za kazi anafanya wiki sita anakuja pumzika mbili...miji mikubwa hili kulitekeleza ni ngumu sana....
 
eti? wanakunywa pombe mida ya kazi? kazi gani?... hao wananchi hapo wana kazi kweli? na ni nani kawaajiri?
but n\serikali inavyofanya ni vema
 
Hiyo sheria ndogo bado inafanya kazi? Labda kama wangekuwa watumishi wa Umma, lakini kwa kuwa wamejiajiri hakuna muda maalum wa kazi kwa watu hao.
 
WATU wanapunguza mawazo maisha magumu afu wanasema eti saa za kazi. kwanini wasiwatafute hao wanaopora mali za umma saa za kazi aka mafis-adi?
 
HAPANA NI KOSA! Nadhani mara nyingi utekelezaji wa sheria unazembea. Kuna sheria za kufungua na kufunga bar. Mi ninafanya kazi maeneo ya mikocheni, kunanyakati ninawaona hawa jamaa wa defender wanapita na kuwasomba watu wanaokunywa pombe wakati wakazi. Bahati mbaya niseme maeneo ambayo wanaya-target ni yale yasio kwenye main road mfano old bagamoyo. Ninahisi kunaweza kukawepo namna ambayo hao jamaa huwa wakikamatwa wanaachiwa. Kenya pia mwaka juzi (au jana- sikumbuki) walikuja na sheria hiyo, na kwa muda imefanyakazi sijui nyakati za sasa! Inatia kichefuchefu kuona jinsi nguvu kazi inavyopotezewa kwenye pombe na mambo kama hayo.
ANGALIZO: Kwa maeneo ya Dar/mijini ugumu wake ni kuwa watu wanafanyakazi kwa shifti na kumwambia mtu mbona hayupo kazini muda wa mchana ni suala gumu kwa kuwa sio wote wameajiliwa kazi za mchana tuuuu!
hivyo ni kosa? Mbona Dar es salaam ni kinywaji masaa 24? Au hii sheria inahusu pombe za kienyeji tu?
 
Back
Top Bottom