macho_mdiliko
JF-Expert Member
- Mar 10, 2008
- 21,766
- 39,536
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Bw. Lawrence Masha ametakiwa kujiuzulu kutokana na kauli anayodaiwa kuitoa hivi karibuni juu ya mauaji ya albino alipohojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa mauaji ya albino ni kitu kidogo.
Wakizungumza jijini jana katika mdahalo wa watu wenye ulemavu, washiriki wa mdahalo huo walisema kutokana na kauli hiyo albino pamoja na walemavu wote nchini walitangaza kutokuwa na imani naye na kumtaka awapishe wengine.
Wadau hao pia walisikitishwa na jinsi Serikali inavyoshindwa kuwalinda albino huku wanyama walioko katika mbuga mbalimbali wakipatiwa ulinzi wa kutosha.
"Vifaru na wanyama huko porini wanalindwa na helkopta ili wasizidi kuuawa, lakini albino wameshindwa kuwekewa walinzi na huku kila siku vifo vyao vinaripotiwa, hii inaonesha wazi kuwa suala la mauaji ya albino halishughulikiwi ipasavyo na mwenye dhamana ya kuhakikisha usalama wao ni Waziri wa Mambo ya Ndani, sasa leo hii anasema mauaji hayo ni kitu kidogo, jamii imueleweje?" walihoji.
Mtaalamu wa ushauri wa Jamii ya Albino Tanzania (TAS), Bw. Kondo Seif alisema kuwa ni lazima watahakikisha kuwa Bw. Masha anawajibishwa kwa kauli yake hiyo na kuahidi kuwa 'asipokufa' na waziri huyo basi atauawa na wauaji na kumtaka Rais Jakaya Kikwete amwajibishe waziri wake huyo haraka.
Aliongeza kuwa mpaka sasa hakuna takwimu sahihi za mauaji ya albino, ambapo kwa makadirio ni 32 tu ndio wanaotambulika kuuawa kinyama, lakini idadi hiyo ni ndogo sana kutokana na idadi kubwa ya albino wanaouawa kutotolewa taarifa iwe kwa makusudi au kwa bahati mbaya.
"Tulisikia kauli ya Mheshimiwa Rais Kikwete katika kilele cha maadhimisho ya kulaani mauaji ya albino kuwa ni lazima atasambaratisha mtandao wa wauaji kama dola lilivyofanikiwa kusambaratisha mtandao wa majambazi nchini.
"Kauli hii ilileta faraja kwa albino, lakini kwa bahati mbaya kuanzia siku ile hadi leo, albino kadhaa wamepoteza maisha yao na wengine kuongezewa kiwango cha ulemavu kwa kunyofolewa viungo vyao, jamii ya albino imepungukiwa imani kwa viongozi wao na vyombo vya dola kwa ujumla," alidai Bw. Seif.
Akizungumza kwa upande wa walemavu wote nchini, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Walemavu la DOLASED, Bw. Gideon Mandesi alisema kuwa rasilimali fedha ni muhimu kuwepo ili kuhakikisha mchakato wa utekelezaji wa sera unafanikiwa na ubora wa maisha ya kila mtu mwenye ulemavu unapatikana Tanzania.
Hata hivyo alipotakiwa kufafanua juu ya kauli hiyo Waziri Masha alikanusha kusema hivyo badala yake alifafanua kuwa alieleza Serikali kusikitishwa na mauaji hao na kulaumu tu kuwa vyombo vya habari vimekuwa vikilikuza suala hilo.
"Sijawahi kuzungumza kitu kama hicho, isipokuwa nilisema kuwa serikali inasikitishwa sana na mauaji hayo na tunafanya juhudi kukomesha, ila baadhi ya waandishi wa habari wanataka kukuza mpaka suala hili kuonekana kuwa ni watanzania wote ndio wanaohusika kitu ambacho si kweli," alisema Bw. Masha.
Kutoka Majira
Majira