Wale waliofukuzwa na wengine kuhamishwa Tambaza Secondary 1993 mko wapi?

kipusy

JF-Expert Member
May 7, 2010
639
321
Washkaji wote waliosoma Tambaza enzi zileeee big up sana

Mnamkumbuka nyau, Mwl. Mushi, LIle sooo la Kuwatwanga Jitegemee sec, Kakonda kalidanji mitaa ya Keko, Mnakumbuka ile mikanda uliyokua unachapwa pale kantin kugombea menyu? Kina Dictetor mpoo? Kina Kanaluza.

Lile soo la vitabu ni soo babaake, kuna mtu ambaye alikosa volume siku ile kweli?
 
Aisee mambo ya sikonzi kwa chai! Maisha yanasonga ingawa wanasambukile wengine baada ya pale ikawa ndiyo mwanzo wa kuharibikiwa na mpaka leo wanaishi maisha ya taabu,wengine tulikomaa hivyo hivyo hadi kuvaa majoho maisha yanasonga.
 
nawafahamu waliohamishiwa Magamba Secondary (sasa SEKUCO) IPO LUSHOTO, jamaa walikuwa na fujo ile mbaya.
 
Aisee!! nimekumbushwa mbali sana enzi za akina vimto, kuna mwalimu alikuwa vituko kwa sana anaitwa Lulindi, mie mmojawapo nilitupwa mkoani baaada ya
kusimamishwa mwaka nashukuru mwisho wa siku niliweza kusimama tena
 
Kumbukumbu zangu zinaniambia kulikuwa na "ugomvi wa jadi" kati ya Azania na Tambaza mpaka hili suala likaongelewa Bungeni, maana kwa kweli hali ilikuwa mbaya
 
Nakumbuka Nikakutana na Washikaji zangu Umiseta Pale Same Sec i was so Happy....

Mr. D. Mbawala Upo?

Fujo za Tambaza nadhani zilianza enzi za Marehemu Puzzo? aliyejiua... mwishoni wa miaka ya 80 sikuwahi mshuhudia ila Habari zake zilitosha kumuelewa vizuri kwani alikuwa anapiga konda hadi Dereva halipi nauli akimkuta form one anamyang'anya pesa, Alishawahi mtuma mtu Chips na soda akampa shs Kumi kisha akamuambia arejeshe na chenchi wakati Soda ilikuwa ni shs 16 Chips na shs 10
 
Aisee!! nimekumbushwa mbali sana enzi za akina vimto, kuna mwalimu alikuwa vituko kwa sana anaitwa Lulindi, mie mmojawapo nilitupwa mkoani baaada ya
kusimamishwa mwaka nashukuru mwisho wa siku niliweza kusimama tena

Umsikie Lulindi anamsifia Socrates na "Socratic Method", au anakupa stories za Josip Tito, au habari za mkutano wa Bandug kama alikuwapo vile. Lulindi alifundisha historia kama profesa wa chuo O Level. Wakati kila mtu kashikwa na euphoria ya kufunguliwa kwa Mandela Lulindi alitabiri how disappointing the Mandela presidency would turn out to be.

Halafu Lulindi anachat na wanafunzi kama mshikaji tu. Hata njuka.

Umenikumbusha mtu ambaye ningependa kumsikia mazungumzo yake sana.
 
Nawakumbuka wanatambaza walipokuja shuleni kwetu BK, walileta zao za kunyoa vipara vya wembe na kumaliza nywele zote. Walipigwa azabu hadi nywele zilipoota tena...... HATA HIVYO MLITIKISA NCHI.
 
Dah na bro angu nakumbuka alihamishiwa Dom alipo rudi likizo akadata jumla mpaka leo.
 
Nakumbuka Nikakutana na Washikaji zangu Umiseta Pale Same Sec i was so Happy....

Mr. D. Mbawala Upo?

Fujo za Tambaza nadhani zilianza enzi za Marehemu Puzzo? aliyejiua... mwishoni wa miaka ya 80 sikuwahi mshuhudia ila Habari zake zilitosha kumuelewa vizuri kwani alikuwa anapiga konda hadi Dereva halipi nauli akimkuta form one anamyang'anya pesa, Alishawahi mtuma mtu Chips na soda akampa shs Kumi kisha akamuambia arejeshe na chenchi wakati Soda ilikuwa ni shs 16 Chips na shs 10

nilisoma hapo miaka hiyo. Hii ilikuwa shule ya aina yake. Tulikuwa tunakula viazi maganda na mchuzi wa nyama. Halafu unakwenda summit kupiga shule. Ukitoka hapo ngoma Faya au Palm Beach unalamba Riziki kwa Mungu, Dau la Mnyonge, Simba Luwala, Kolombia,n.k. Konda akileta zake anachapwa. Walikuwepo kina Shetani, No Mbungi, DickPapa, hata Ndama Mutoto ya Ngombe maticha wetu Father K, Busianya,Haonga,Kaihula(sasa Mb Cdm), Savimbi,n.k Those old gooddays
 
hizo story sisi tulisikia tu!
mimi niliingia hapo advance level baada ya o level kusambaratishwa shule za bush!
nilipokuja dar last year nilipita hapo mitaa ya tambaza nilikumbuka mambo mengi sana!
nashauri tuanzishe special thread ya tambaza sec school
 
Daah! Umenikumbusha mbali sana unapolitaja hili daladala simba luwala. Nadhani lilikuwa ubungo kariakoo au posta. Ilikuwa miaka ya 1985 na kuendelee. Nakumbuka mechi zilizokuwa zinachezwa pugu sec. Ilikuwa kazi kubwa azania inapocheza na tambaza au tambaza na kinondoni. Bakora na ngumi nje nje. pamoja na fujo zote lakini shule zilikuwa na wanafunzi vichwa na tulikuwa tunajuana nani bingwa wa maths, physics, kemia na biology miongoni mwa wanafunzi wa shule hizo. Namkumbuka Benedict ndomba wa tambaza miaka ya 1984- 1987, modest stanley chindonga azania 1984-1987. wana njawa azania(84-87) Modest ni mhandisi tanesco ila sikui Benedict yupo wapi
 
Back
Top Bottom